Maswali 5 ya kusisimua zaidi duniani ambayo sayansi haijaweza kujibu

run CMD

JF-Expert Member
May 31, 2015
2,827
3,136
Ni vitu vichache ambavyo vinasisimua zaidi kuliko kuwa na uelewa wa mambo fiche ya ulimwengu kama ulivyo na umbo lake. Na vitu hivyo sio vya watu werevu tu, bali pia ni vya kila mtu kuviwaza na kuvifikia.

Hebu tafakari pale ambapo kwa mara ya kwanza unafaulu kulifumbua fumbo, sana sana kwa sababu mtu mmoja mwerevu au zaidi wamewekeza maisha yao katika kulielewa na kulifumbua.
Baadhi ya mafumbo ni ya kale, na mengine ni mapya; kwasababu kadri unavyoendelea kupata ujuzi na maarifa, ndio kadri unavyoanza kuelewa ni nini ambacho hukijui.
Kuanzia swali la ni kwanini baiskeli zinaweza kusimama wima wakati zinaendeshwa hadi nambari za hesabu ambazo ni ngumu kuelewa, bahari ya mambo yasiyojulikana ni pana.

Mwanafalsafa Thomas Hobbes analiwahi kusema kwamba ni sharti maswali yaendelee kuwepo – ili watu waendelee kutafuta majibu na hivyo kuusisimua ubongo.

Lakini unawezaje kuamua ni maswali gani yenye kuulizwa zaidi duniani iwapo unaambiwa uchague matano tu?

Naam, baada ya kufikiria sana, tuangalie baadhi yake…

1. Ulimwengu, anga zimetengenezwa na nini?​

Ulimwengu wenyewe na umbo lake huibua maswali mengi: Nini kilikuwepo kabla yake, je ukubwa na upana wake ni upi, kuna ulimwengu mwingine kama huu ama huu ndio wa aina hii pekee?

Wanasayansi kwa sasa wameweza kuelewa tu asilimia 5% tu ya umbo la ulimwengu. Tunazungumza kuhusu atomu, protoni, nutroni na vipande vingine vidogo vya vitu ambavyo viko duniani lakini havionekani.

Leo hii unaweza ukadhani ni jambo la kawaida tu kuifahamu atomu, lakini wazo lake lilinakiliwa katika karne ya 5 BC na kupewa jina hilo na Wagiriki. Hata hivyo ni katika karne ya 19 ambapo mkemia John Dalton alifanya utafiti uliotoa hoja ya kushangaza kwamba vitu vyote vinavyoonekana vimeundwa kwa kutumia vipande vipande vidogo sana vya atomu ambavyo haviwezi kugawanyika.

Tangu hapo, maswali mengi yamepata majibu. Lakini maswali mengi bado yapo kuhusu asilimia 95% iliyosalia ya ulimwengu usiojulikana.

Tunachojua hata hivyo ni kwamba 27% inajumuisha giza. Hili liligunduliwa mnamo 1933, na zaidi ni kwamba giza ndio gundi inayozishikanisha sehemu tofauti za anga.

Lakini baada ya miongo kadhaa ya utafiti, maswali bado ni mengi kuhusu anga.

2. Maisha yalianza vipi?​

Wengi wamejaribu kujibu swali hili.
Mojawapo ya dhana zilizojaribu kujibu inajulikana kama “Primordial soup” kutoka miaka ya 1920s iliyotolewa na raia wa USRR Alexander Oparin pamoja na mtaalamu wa vinasaba kutoka Uingereza JBS Haldane.

Wanadai kwamba chanzo cha maisha ni wakati dunia ikiwa changa miaka mingi iliyopita, bahari ilikuwa na kemikali nyingi muhimu kwa maisha kuwepo ambazo zilichanganyikana na gesi zilizokuwepo angani kama vile kaboni, haidrojeni pamoja na nguvu ya radi.

Hii ndio dhana ambayo inakubaliwa na wanasayansi wengi kuhusu chanzo cha maisha duniani. Lakini sio kila mtu anakubali hili, na kuna dhana zingine pia.

Ki hakika kuhusu maisha, hakuna makubaliano yoyote kuhusu je, maisha hasa yalianza vipi? Baadhi ya watafiti wanaamini yalianzia baharini, wengine kwenye barafu au hata sehemu ya mbali sana kutoka duniani.

Na pia haijulikani yalianza wakati gani, na kwanini?
Tunachokijua kwa hakika ni kuwa maisha yalianza baada ya dunia kuwepo, zaidi ya miaka bilioni 4.5 zilizopita, na kabla ya miaka bilioni 3.4 zilizopita kwani kuna visukuku (yaani fossils) ambavyo vimedhibitiwa kuwepo wakati huo.
Kuna dhana kuwa aside za amino zilichanganyika na kuwa protein, na pia kuna dhana kuwa maisha yalianza na RNA ambayo ni karibu na DNA ambayo inaweza kubeba vinasaba.

Pia kuna wale wanaodhani kwamba viumbe wa kwanza walikuwa vyombo tu vya kubeba vitu ambavyo vinahusisha maisha.

3. Ni nini kinatufanya kuwa binadamu?​

Awali, kuna vitu ambavyo vilikuwa vinadhaniwa ni maalum tu kwa binadamu: kama vile lugha, kujitambua tunapojiangalia kwa kioo, uwezo wa kuvumbua na kutumia vifaa kusuluhisha matatizo na changamoto ngumu.

Lakini wanyama kama vile pweza, kunguru na wengine wamekuwa na baadhi ya vitu hivi na hivyo kuondosha dhana hiyo.
Na je, vipi kuhusu DNA?
Imebainika kuwa vinasaba vya wanadamu vinafanana asilimia 99% na vile vya sokwe, mnyama ambaye mwanajiolojoa Charles Darwin alijaribu kudokeza kuwa ni sehemu ya familia hii.

Ni kweli kwamba ubongo wa binadamu ni mkubwa kuliko wa wanyama wengi, lakini baadhi ya wanyama kama ndovu wana ubongo mkubwa kutuliko – kwa hivyo dhana hii nayo ina utata.

Kwa hivyo ni nini kinatufanya tuwe binadamu? Ni utamaduni wetu, au uwezo wetu wa kupika au hata kuwasha moto, au uwezo wa kuhurumiana? Bado haijulikani…

4. Fahamu ni nini?​

Bila shaka fahamu ni baadhi ya vitu muhimu vinavyotufanya kuwa binadamu. Lakini fahamu yenyewe ni nini?

Wataalamu wanasema kuwa akili ndio kitu ambacho kinadhibiti fahamu. Lakini akili yenyewe nayo ni kitu kigumu kuelewa jinsi kinavyofanya kazi na kutusaidia kufikiria na kufanya maamuzi.
Fahamu inatusaidia kutambua sauti, harufu, kuelewa mazingira yetu na pia kuhifadhi taarifa muhimu akilini.

Aidha inasaidia kukadiria matukio na kuchukua tahadhari.

Lakini ni zaidi ya kompyuta. Sio tu kwamba tunafikiria, tunafahamu kiundani kuwa tunafikiria.

Fahamu ni kitu cha kushangaza sana cha ubongo na labda ni swali ambalo hatutawahi kulitatua.

5. Kwanini huwa tunaota?​

Wanasayansi na wataalamu wa usingizi wanafahamu kuwa huwa tunaota sana sana wakati macho yanapepesa pepesa (rapid eye movement phase REM) tukiwa tumelala.

Lakini hawajafahamu ni kwanini tunaota.
Sigmund Freud aliamini kuwa ndoto huwa zinaashiria matamanio yetu (ikiwemo ya kingono) ambayo hayajatimizwa; lakini wengine wanaamini kuwa ndoto ni picha tu ambazo hutokea kwa akili ambayo imepumzika.

Baadhi ya tafiti zinaashiria kuwa ndoto huchangia katika kumbukumbu, masomo na pia kudhibiti hisia. Na pia zinaweza kusaidia kupunguza msongo wa mawazo kutokana na ugumu na uhalisia wa maisha.

Pia ndoto zinaweza kutusaidia kuepuka hatari kwa kuonyesha hali ambayo huenda ikatokea katika mahusiano na hata maisha kwa jumla.

Lakini pia huenda ndoto zikawa hazina maana yoyote. Inawezekana kuwa ni shughuli tu ya akili wakati imepumzika.

Na kwa kumnukuu Calderon de la Barca; ndoto ni kama maisha tu, ndoto ni ndoto.

Also

Credit:BBC

Jibu la uhai

Uhai Ulianzaje?
 
1. Chanzo cha ulimwengu hakijulikani bado

2. Nadharia mbili nzito kuliko zote kuhusu mwanzo wa maisha, hazisemi maisha yalianzaje haswa

3. Utashi, uwezo wa kufikiri na kuvumbua mambo unatutofautisha na wanyama wengine. Tuna uwezo mkubwa wa kiakili kuliko wanyama wote

4. Fahamu ni jinsi ubongo wako unavochanganua mazingira yanayokuzunguka, hapa 'mazingira' nimemaanisha hadi binadamu wenzako

5. Sababu ya kuota haijulikani ila nadharia pendwa ni kwamba ubongo wako unachanganua matukio, na mawazo mbalimbali uliyokuwa nayo kwenye siku
 
Maneno mengi ya mtoa mada yamebebwa hapa 😂
 
Hivi ulimwengu ndio universe???
Na je maisha ninini? Lengo kuu la maisha ninini??
Na uhai ukiondoka Leo unaweza kurudi baadae kama species tofauti( mnyama mmea etc) au kama binadamuu mwingine ambaye anaanza Ku feed data mpya?
Na kama yameanzia baharini, hivi mechanism gani ilitumika kupata hizi species??? Maana kuna viumbe Aina nyingi Sana.
Na hizi species mpya kama Corona virus zimetoka wapi?
Je kuna siku zitakuja species za binadamu ambazo zipo more advanced?
 
Back
Top Bottom