Jinsi ya kujiandaa kujibu maswali ya BBC Hard talk kwa wanasiasa

YEHODAYA

JF-Expert Member
Aug 9, 2015
36,911
51,889
Kwa mwanasiasa iwe upinzani au chama tawala ukiitwa kuhojiwa BBC Hard talk unatakiwa ujiandae na ujue kuwa maswali utakayoulizwa yameandaliwa na jopo la watu wengi wakiwemo donors wa chama chako au serikali na wabobezi kwenye siasa na taaluma yako ambao hutaka kukujua hasa undani wako na wa chama chako kupata undani kwa ajili ya maamuzi yao katika mambo.Mwandishi anawakilisha tu yale maswali .

Maswali hujikita Kwenye udhaifu wa kwako na wa chama chako sio wa mwingine au chama kingine . Uwe tayari kwa hilo maswali huulizwa kimtego sana mfano wewe unatuhumu serikali ya Magufuli uko opposition na ni mwanasheria Hard talk watakuhoji do you have legal evidence kwenye tuhuma zako wewe au chama chako?

Ukiwa huna ukajikanyaga anakuacha anaenda swali lingine lakini Meseji send kwa waliomtuma kuwa huyu mtu na chama chake hawana legal evidence pamoja na sifa zote wanazojitia kuwa nazo na hawajachukua any legal steps.Hivyo ukienda hojiwa jiandae barabara maeneo yako ya udhaifu wako binafsi na wa chama chako au serikali kama ni kiongozi wa serikali.

Ujue hutahojiwa kuhusu udhaifu wa mwingine au chama kingine nje ya cha kwako watajikita kuhoji udhaifu wako na chama chako.Hili hubeba asilimia 90 ya mahojiano. Asilimia kumi inayobaki ni ya kukihoji maswali laini ili u relax yaweza asilimia tano yakawa mwanzo wa mahojiano na asilimia tano mwisho wa mahojiano ili walau upumue mnapoagana .Pili jizatiti na takwimu za kuaminika sio newspaper cuttings au taarifa za jamii forums.

Sababu wao huwa na takwimu toka credible sources za kimataifa. Tatu wenzetu mtu akifanya vizuri hata akiwa opponent wako wana tabia ya Ya ku appreciate hilo zuri la opponent wako unajibu yes kuna mazuri kafanya unatoa mifano mizuri miwili mitatu halafu kama una reservation unasema lakini angefanya vizuri zaidi angefanya moja, mbili tatu.

Usiseme aah hamna kitu alichofanya!!!!!! Mwandishi ataruka haraka kwenda swali lingine kuwa meseji send kuna mema yapo lakini huyu ninayemhoji hajui kitu hayuko informed ni mweupe kichwani!!!
 
Tatizo la Lisu alikwenda kwa kupania kuichafua Serikali na JPM na inaonekana ali ipania siku ile na kuisubiri kwa hamu kubwa.
Matokeo yake kila akiulizwa kama anao ushahidi usio na shaka, Anabaki kusema kuna ushahidi wa mazingira.
Pale ndipo Dunia ilipo muona anahasira na mihemko mingi kuliko anacho taka kuwaaminisha wanao mwangalia.
Baati mbaya ata mwenyekiti wa chamachake anahusishwa na matukio ya kuwafanyia uharifu wale ambao waanaonekana tishio kwake na ata yeye Tundu inawezekana akawa mwasilika wa hayo. Yote ni kutokana na ushahidi wa kimazingira hususan unapokaribia uchaguzi ndani ya chama chao. Mfano Chacha Wangwe na Zito kabwe pale walipo jaribu ku challenge nafasi ya Mwenyekiti wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwaiyo Lissu unampa maksi ngapi mkuu?
Ten percent. Alijibu vizuri mwanzo kwenye kujitambulisha na mwishoni alipoonyesha nia ya kugombea uraisi alijibu vizuri kuwa chama na wanachama wakipendekeza yuko tayari lakini maswali ya katikati hakuambulia kitu yalimshinda yote
 
Mwambie Jiwe ajiandae
Kwa mwanasiasa iwe upinzani au chama tawala ukiitwa kuhojiwa BBC Hard talk unatakiwa ujiandae na ujue kuwa maswali utakayoulizwa yameandaliwa na jopo la watu wengi wakiwemo donors wa chama chako au serikali na wabobezi kwenye siasa na taaluma yako ambao hutaka kukujua hasa undani wako we went na chama chako kupata undani kwa ajili ya maamuzi yao katika mambo.Mwandishi anawakilisha tu yale maswali . Maswali hujikita Kwenye udhaifu wa kwako na wa chama chako sio wa mwingine au chama kingine . Uwe tayari kwa hilo maswali huulizwa kimtego sana mfano wewe unatuhumu serikali ya Magufuli uko opposition na ni mwanasheria Hard talk watakuhoji do you have legal evidence kwenye tuhuma zako wewe au chama chako? Ukiwa huna ukajikanyaga anakuacha anaenda swali lingine lakini Meseji send kwa waliomtuma kuwa huyu mtu na chama chake hawana legal evidence pamoja na sifa zote wanazojitia kuwa nazo na hawajachukua any
legal steps.Hivyo ukienda hojiwa jiandae barabara maeneo yako ya udhaifu wako binafsi na wa chama chako au serikali kama ni kiongozi wa serikali. Ujue hutahojiwa kuhusu udhaifu wa mwingine au chama kingine nje ya cha kwako watajikita kuhoji udhaifu wako na chama champ.
Hili hubeba asilimia 90 ya mahojiano. Asilimia kumi inayobaki ni ya kukihoji maswali laini ili u relax yaweza asilimia tano yakawa mwanzo wa mahojiano na asilimia tano mwisho wa mahojiano ili walau upumue mnapoagana .Pili jizatiti na takwimu za kuaminika sio newspaper cuttings au taarifa za jamii forums. Sababu wao huwa na takwimu toka credible sources za kimataifa. Tatu wenzetu mtu akifanya vizuri hata akiwa opponent wako wana tabia ya Ya ku appreciate hilo zuri la opponent wako unajibu yes kuna mazuri kafanya unatoa mifano mizuri miwili mitatu halafu kama una reservation unasema lakini angefanya vizuri zaidi angefanya moja, mbili tatu.Usiseme aah hamna kitu alichofanya!!!!!! Ataruka haraka kwenda swali lingine kuwa meseji send kuna mema yapo lakini huyu hajui kitu hayuko informed ni mweupe kichwani!!!

In God we Trust
 
Tatizo la Lisu alikwenda kwa kupania kuichafua Serikali na JPM na inaonekana ali ipania siku ile na kuisubiri kwa hamu kubwa.
Matokeo yake kila akiulizwa kama anao ushahidi usio na shaka, Anabaki kusema kuna ushahidi wa mazingira.
Pale ndipo Dunia ilipo muona anahasira na mihemko mingi kuliko anacho taka kuwaaminisha wanao mwangalia.
Baati mbaya ata mwenyekiti wa chamachake anahusishwa na matukio ya kuwafanyia uharifu wale ambao waanaonekana tishio kwake na ata yeye Tundu inawezekana akawa mwasilika wa hayo. Yote ni kutokana na ushahidi wa kimazingira hususan unapokaribia uchaguzi ndani ya chama chao. Mfano Chacha Wangwe na Zito kabwe pale walipo jaribu ku challenge nafasi ya Mwenyekiti wao.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alitegemea mahojiano yale yamjenge kisiasa, kumbe yamefichua udhaifu mwingine. Kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya masuala unayoyaongelea.

Hardtalk sio sawa na huu uandishi wa habari wa kibongo wa kujiendea tu kwa kuyasikiliza majungu na umbeya.
 
Kwa hiyo mkuu unakubaliana na polepole ya kuwa Stephen Sucker ni mwanachama wenu ama laa???
mimi Hilo sijui .Nilichoeleza ndicho hicho kuwa BBC hard talk sehemu kubwa hushughulika na udhaifu wako na chama chako kwenye mahojiano Lisu nadhani hakuwa akijua hilo alifanya kushtukizwa alitarajia BBC hard talk wajikite udhaifu wa CCM au serikali mwandishi akawa anamkwepa na kuendelea kumkomalia tu Lisu kwenye ya kwake na chama chake tu.Kila mtu na tafsriri yake na maoni yake siingilii uhuru wa mtu kutoa maoni yake ndio maana nikasema hata mtu awe CCM akienda BBC Hard talk ajiandae
 
mimi Hiro sijui .Nlikichoeleza ndicho hicho kuwa hard talk sehemu kubwa hushughulika na udhaifu wako na chama chako kwenye mahojiano Lisu nadhani hakuwa akijua hilo alifanya kushtukizwa alitarajia BBC hard talk wajikite udhaifu wa CCM au serikali mwandishi akawa anamkwepa na kuendelea kumkomalia tu Lisu kwenye ya kwake na chama chake tu.Kila mtu na tafsriri yake na maoni yake siingilii uhuru wa mtu kutoa maoni yake ndio maana nikasema hata mtu awe CCM akienda BBC Hard talk ajiandae

Nimekuelewa mkuu, kwa kweli hata akienda mheshimiwa Rais John Joseph Pombe Magufuli lazima akutane na maswali magumu kwa mfano ataulizwa

kwa mujibu wa katiba inaruhusu mikutano ya vyama vya siasa, na wewe uliapa kuirinda na kuitetea katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania je kwa kuzuia mikusanyiko ya vyama au mikutano ya vyama vya siasa huoni unapingana na katiba uliyoapa kuirinda na kuitete?? swali litakalofuata sasa,

kwa mujibu wa sheria za Tanzania ni lazima matumizi na pesa za serikali za kutekeleza miradi mbali mbali lazima pesa hizo ziizinishwe na Bunge, je pesa za kununulia ndege, na pesa za ujenzi wa uwanja wa ndege wa chato ziliidhinishwa bungeni au ulijiamlia tu kuchukua pasipo idhini ya bunge?? Je kufanya hivyo huoni kama unavunja sheria uliyoapa kuirinda??
kile kipindi kitamu sana hakina upendeleo ni fact tu.
 
Kipengele cha pili kinamruhusu rais kuidhinisha matuminz yoyote kutoka mfuko wa rais sio lazima aonane na bunge dhaifu.
Rais ashajua bunge dhaifu so hawezi kulishilikisha katika mambo ya msingi isipokuwa yale ya ndio tu.
 
Alitegemea mahojiano yale yamjenge kisiasa, kumbe yamefichua udhaifu mwingine. Kutokuwa na vyanzo vya uhakika vya masuala unayoyaongelea.

Hardtalk sio sawa na huu uandishi wa habari wa kibongo wa kujiendea tu kwa kuyasikiliza majungu na umbeya.
Tanzanian asilimia kubwa hatuna waandishi wa habari Tuna reporters wa habari. Kazi yao kuripoti tu.Mtu akitukana serikali wanaripoti atukana serikali. Wengi reporters tu
 
Tanzanian asilimia kubwa hatuna waandishi wa habari Tuna reporters wa habari. Kazi yao kuripoti tu.Mtu akitukana serikali wanaripoti atukana serikali. Wengi reporters tu
ingependeza zaidi kama uchambuzi ungetoka kabla ya mahojiano zaidi ya hapo ni uchochezi
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom