Mbinu Bora ya Kutumia Kujenga Himaya ya Utajiri Wako Kupitia Ardhi na Majengo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Lengo kuu la huduma zangu za uandishi kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo ni:

✓ Kuwasaida watu kutunza fedha zao kupitia ardhi na majengo.

✓ Kujenga himaya ya utajiri kupitia ardhi na majengo.

Nimekuwa nikiulizwa mara kwa mara swali kuhusu ni mbinu gani ya kujitengenezea kipato kutokana na uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Ndipo nikaanda kitabu changu kiitwacho NJIA 120 ZA KUTENGENEZA PESA KWENYE ARDHI NA MAJENGO.

Kwenye kitabu hicho kuna njia tofauti tofauti za kumwezesha mwekezaji kutengeneza fedha kwenye uwekezaji huu. Lakini nikaongezea jambo lingine linalohusu kutunza utajiri ambao mtu tayari anao kupitia umiliki wa ardhi na majengo.

Njia kuu 2 za kutengeneza fedha kupitia uwekezaji kwenye ardhi na majengo ni:

✓ Kuwa na kipato endelevu.

✓ Faida ya wakati mmoja.

MOJA

Kipato endelevu.

Mbinu ya kweli ya kujenga utajiri kwa uwekezaji wa moja kwa moja kwenye umiliki wa ardhi na majengo ni kutumia njia za kutengeneza kipato endelevu. Njia zinazo ingiza kipato endelevu cha kila mwezi zipo katika makundi 3;

✓ Kuipangisha nyumba au viwanja/shamba.

✓ Kununua na kumiliki nyumba au ardhi kwa zaidi ya miaka 2.

✓ Kununua, kuboresha/kuendeleza na kumiliki ardhi au nyumba kwa zaidi miaka 2.

Makundi haya matatu yanatofautishwa na mambo 2. Nayo ni;

✓ Kiwango cha kodi iletayo kipato endelevu na.

✓ Uwingi wa idadi ya nyumba au viwanja unavyotakiwa kumiliki ili kujenga utajiri.

Mbinu ya kupangisha nyumba/ardhi huhitaji idadi chache za nyumba au ardhi ili kujenga utajiri ukilinganisha na mbinu ya kununua na kumiliki ardhi au nyumba na mbinu ya kununua, kuendeleza na kumiliki ardhi au nyumba.

Mbinu ya kupangisha nyumba au ardhi huleta kiasi kidogo cha kodi ya mwezi ukilinganisha na mbinu ya kununua, kuendeleza na kumiliki nyumba au ardhi.

Mbinu ya kununua na kumiliki ardhi au nyumba huhitaji idadi kubwa ya nyumba/vipande vya ardhi ili kutengeneza kipato endelevu hatimaye kujenga utajiri. Hii ni sahihi kwa kulinganisha na mbinu ya kumiliki nyumba za kupangisha.

Mbinu ya kununua na kumiliki nyumba au ardhi huleta kiasi kikubwa cha kodi ya kila mwezi ukilinganisha na mbinu ya kupangisha nyumba tu.

Mbinu ya kununua, kuendeleza na kumiliki ardhi au nyumba ndiyo mbinu bora sana kutoka katika njia zote 3 za kutengeneza kipato endelevu. Hii ni kwa sababu;-

✓ Inaweza kuingiza kiasi kikubwa cha kipato endelevu kwa sababu ongezeko la thamani ya ardhi au nyumba husika.

✓ Unahitaji idadi ndogo ya vipande vya ardhi/nyumba ili ujenge utajiri wako.

Hivyo, kutumia mbinu ya kipato endelevu kujenga utajiri kupitia umiliki wa ardhi au nyumba ni mbinu bora sana ukilinganisha na mbinu zingine. Katika mbinu hii, kununua, kuendeleza na kumiliki ardhi ya kukodisha au majengo ya kupangisha ndiyo njia bora zaidi kati ya njia zinazoingiza kipato endelevu.

Zipo njia nyingi zinazoingiza kipato endelevu cha kila mwezi. Lakini hazihushi umiliki wa ardhi na majengo. Njia hizo ni kama ifuatavyo:

✓ Kununua, kuboresha na kuuza mikopo ya majengo.

✓ Kutoa huduma za uwekezaji kwenye ardhi na majengo kama vile vitabu, kozi za mtandaoni, kumiliki blogu ya kulipia, na kadhalika.

MBILI

Faida ya wakati mfupi.

Hii hupatikana kwa wakati mmoja pale ambapo mnunuzi hulipia huduma au bidhaa (ardhi/nyumba). Njia kuu 4 za kupata faida ni:

✓ Tafuta na toa rufaa. Hii uhusisha kutafuta mtandao au huduma na kuitangaza kwa wengine kwa kuwatoza ada kipindi wanachohitaji.

✓ Kudhibiti na kusaini mikataba ya mauzo ya ardhi na majengo. Hapa inaingia ile mbinu ya kununua na kuuza mikataba ya mauzo ya ardhi na majengo bila kuyamiliki.

✓ Kununua na kuuza ardhi na majengo ndani ya miaka 2 tu.

✓ Kununua, kuendeleza na kuuza ardhi na majengo.

Kati ya njia hizi 4 za kutengeneza faida baada ya kukamilisha mauzo ni ile mbinu ya kununua, kuendeleza na kuuza ardhi au majengo ndani ya miaka 2 tu. Na mbinu hii ya kununua, kuendeleza na kuuza ardhi au majengo ndani ya miaka 2 inakupa ufanisi mkubwa sana endapo utafanya yafuatayo;-

✓ Utatumia njia zote muhimu za kuongeza thamani ya ardhi au nyumba yako wakati wa uendelezaji.

✓ Utatumia kanuni ya Mwanauchumi Vilfredo Pareto isemayo kuwa matokeo ya uwekezaji wako kwa 80% huchangiwa na 20% ya njia ya mbinu unazotumia. Hivyo wakati wa uendelezaji unatakiwa kuweka nguvu, muda na fedha kwenye njia za kuongeza thamani ambazo zitakupa matokeo chanya makubwa sana.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp: +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom