Jinsi unavyoweza kuandaa fomu za Ukaguzi wa viwanja na ukaguzi wa nyumba kabla hujanunua

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Ukaguzi wa nyumba ni sehemu muhimu sana kwenye mchakato wa kununua kiwanja au kununua nyumba. Fomu ya ukaguzi wa kiwanja au nyumba inatakiwa kuwa na vipengele vifuatavyo;-

✓ Taarifa za nakala za umiliki wa ardhi au umiliki wa nyumba.

✓ Taarifa za usalama wa mazingira ya kiwanja au nyumba.

✓ Taarifa ya faida au kipato endelevu cha kiwanja au nyumba.

✓ Taarifa za historia ya umiliki wa kiwanja au nyumba.

✓ Taarifa za makisio ya gharama za ukarabati na maboresho.

✓ Taarifa za makisio ya gharama za uendelezaji wa ardhi.

✓ Taarifa za makisio ya thamani ya ardhi au nyumba.

Ripoti ya ukaguzi wa ardhi na majengo ni nakala ambayo ni lazima uwe nayo kama kweli unahitaji kujenga au kutunza utajiri kupitia ardhi na majengo.

Kwenye makala hii nimekuandalia mambo ya taarifa muhimu ambazo unatakiwa kuzifahamu kabla hujafanya maamuzi ya kuanza kukagua nyumba au ardhi unayotaka kununua.

Pia, taarifa hizi zinaweza kuboreshwa kidogo na madalali kisha kutumiwa kutangaza na kuwavuta wanunuzi wa ardhi au nyumba wanazouza.

MFANO WA TAARIFA ZA KIWANJA/SHAMBA LINALOUZWA.

Utangulizi.

Mkoa =Mbeya.

Wilaya =Mbeya vijijini.

Kata = Ifisi.

Muuzaji =Atupele Mwansasu.

Bei =Tshs.2,500,000/=.

Ukubwa =mita za mraba 550.

Namba ya simu =+255 685 33 34 95.

TAARIFA MUHIMU.

✓ Kimepimwa = NDIYO.

✓ Matumizi ya ardhi =Makazi na biashara.

✓ Hati = HAIPO.

✓ Nakala za kuombea hati =ZIPO.

✓ DENI serikalini (Kilichopimwa) =HAKUNA.

✓ Hali ya ardhi =Tambarare na miti 2 mikubwa.

✓ Tarehe ya kuanza kutangaza = 02-Jan-2023.

✓ Nishati =Umeme TANESCO.

✓ Maji = DUWASA.

✓ Afya = Hospitali isifi na Kliniki mseto (Polyclinic), mita 400 kutoka kiwanja kilipo.

✓ Elimu = Chuo cha madaktari wa diploma cha Ifisi (mita 200 kutoka kiwanja kilipo).

✓ Usafiri = Barabara kuu (mita 300).

✓ Historia ya umiliki = Mmiliki alinunua kutoka Kampuni ya NUHU REAL ESTATE COMPANY LIMITED.

Muhimu: Hapo chini ni picha 2 za kiwanja/shamba.


TAARIFA ZA NYUMBA INAYOUZWA.

Utangulizi.

Mkoa = Dodoma.

Wilaya = Dodoma mjini.

Kata = Mbuyuni.

Muuzaji = AMANI PROPERTIES LTD.

Ukubwa =mita za mraba 600.

Bei = Tshs.30,000,000.

Umri wa nyumba = Miaka 5 tangu kukamilisha ujenzi wake.

Namba ya simu = +255 752 413 711


TAARIFA MUHIMU.

✓ Idadi ya vyumba vya kulala = Vinne.

✓ Idadi ya bafu =Moja.

✓ Idadi vyoo vya umma (Public toilets) =Kimoja.

✓ Ina wapangaji 4 =Walipia jumla ya Tshs.320,000/=.

✓ Kimepimwa = NDIYO.

✓ Matumizi ya ardhi =Biashara.

✓ Hati = IPO.

✓ Nakala za kuombea hati =ZIPO.

✓ DENI serikalini (Kilichopimwa) =LIPO.

✓ Hali ya ardhi =Maua ya kuvutia.

✓ Tarehe ya kuanza kutangaza = 02-Jan-2023.

✓ Nishati = Umeme TANESCO.

✓ Maji = DUWASA.

✓ Afya = Zahanati (mita 300).

✓ Elimu = Sekondari ya Mbuyuni (mita 3000).

✓ Usafiri = Barabara kuu (mita 600).

✓ Historia ya umiliki =Mmiliki alinunua kutoka kwa benki ya NMB kwa njia ya mnada.

Muhimu: Hapo chini ni picha 5 za nyumba (upande wa juu, mashabiki, magharibi, kusini, na kaskazini).

🔥 Mafunzo huanza tarehe 05-Januari-2023.

🔥 Mafunzo huisha tarehe 15-Jan-2023.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp: +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom