Jinsi panya wanavyofundishwa kugundua mabomu SUA Morogoro kitengo cha APOPO

wanachonifurahisha watu wa SUA, akifundisha hata panya tu, tayari profesa. hao wote ukichunguza uprof wao, utavunjika mbavu. nina jamaa yangu mmoja alisoma pale, akawa mganga wa kuku...hahaha, amesomea kozi nyingine sasaivi yupo kwenye kushauri watu wa ukimwi...akili zao ndogo mno.

wameshindwa kusaidia tz na kilimo kwanza, hatuna vitabu vingi vya kiswahili vinavyoweza kuandikwa hata na mwanafunzi wa mwaka wa mwisho tu mfano: jinsi ya kufuga kuku, jinsi ya kufuga nguruwe, jinsi ya kufuga ng'ombe etc, jinsi ya kulima mahindi, mpunga, migomba, miwa etc....wavisambaze kwa watu ordinary huko mtaani, sio lazima viende kwa wasomi wa chuoni hapo tu au kwenye shule zinazofundisha agriculture tu.....mambumbumbu yanang'ang'ania kuuza madawa ya kilimo tu. hayagundui dawa hata moja, hayagundui mbegu bora hata moja,

mbona kenya wenzetu wanagundua mbegu bora ya wanyama na mimea sana? chuo cha SUA kina faida gani hapa tz? mtanai kumejaa mbegu feki, wananchi wengi hawatumii mbegu bora kwasababu hazipo, livestock ni mbegu mbaya ya kizamani iliyodumaaa....
 
attachment.php
 
huyu sio panya ni mnyama fulani jamii ya tumbili na mara nyingi huishi kwenye
mashimo ya vichuguu au miti .na kwa wenzetu wanamwita squirrel.

wNxNVfORSnsTwAAAABJRU5ErkJggg==
 
SHIRIKA moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini.

Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania.


attachment.php


Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa na hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi, hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.

Uwezo kutokana na maumbile ya pua

Panya wanafundishwa jinsi ya kunusa wakiwa wadogo, kwa kuwekewa vitu vyenye madini ya milipuko. Tangu mwaka 2000, APOPO imekuwa ikiwafunza panya kwenye chuo cha Sokoine, Morogoro. Mwaka 2006 panya wa hao walianza zoezi la kutafuta mabomu ya ardhini huko Msumbiji.

attachment.php


Kabla ya panya kuanza kazi ya kunusa wapi mabomu yalipo, lazima wafuzu mtihani kutimiza viwango vya kimataifa vya kutambua mabomu ardhini.

Zawadi kwa ufanisi

Wakati wa mafunzo panya hupewa zawadi kwa kufuzu vizuri kwa sauti maalumu ambayo inaashiria kufuzu kwake na kupewa kipande cha ndizi kama zawadi.

Panya aliyefuzu vizuri huwa ana uwezo wa kuzunguka mita 400 za mraba kwa siku, wakati eneo kama hili litamchukua binadamu wiki mbili ili kuweza kugundua wapi kumefukiwa bomu.

Pua za kunyumbulika

Kulinganishwa na mbwa, panya wanaweza kutumiwa na mtu yeyote kwani hawana tabia ya kutokuwa na mahusiano ya karibu na mtu aliyemfundisha kama walivyo mbwa.

attachment.php


Panya anaweza kufanya kazi ya kufichua mabomu, hata kama aliyemfundisha hayupo na huwa wanafanya kazi vizuri kwa ufanisi na mtu yeyote hakuna shida kwa panya aliyefundishwa Tanzania, kwenda kufanya kazi Msumbiji, Angola, Thailand na Kambodia.

Kazi nchini Msumbiji

Hadi kufukia sasa nchini Msumbiji, zaidi ya mita za mraba milioni 6,5 za ardhi zimeshachunguzwa na mabomu 2,000 yaliyotegwa ardhini yamepatikana na kuharibiwa, pia bado mabomu 1,000 kuteguliwa na bunduki na silaha nyingine ndogo 12,000 zilipatikana.

Na mpaka sasa kuna makundi saba yenye watu 54 ambayo yanashughulika na kazi ya kutegua mabomu kwa kuwatumia panya.


Chanzo: APOPO
 

Attachments

  • Panya.jpg
    Panya.jpg
    39.2 KB · Views: 601
  • Panga 2.jpg
    Panga 2.jpg
    54.6 KB · Views: 590
  • Panya ardhini.jpg
    Panya ardhini.jpg
    49.7 KB · Views: 589
Sasa hizi taasisi zisizo za kiserikali zitaanza kubezwa kama Twaweza hahahah Tanzania yangu eeeehh
 
Wafundishwe pia kunusa "sembe". Wapige kambi pale uwanja wa ndege kwa kuanzia; unga ni janga kwa kizazi chetu cha sasa na kijacho...
 
Mbona hawa panya wapo siku nyingi sana, zaidi ya miaka 5 iliyopita!

Ni kweli Mkuu. Hii habari pale SUA ni ya kitambo. Niliwahi soma mahali kwamba hata utambuzi wa magonjwa kama TB wameanza kufanya utafiti kubaini kama wanaweza. I stand to be corrected.
 
Back
Top Bottom