Ngalikihinja
JF-Expert Member
- Sep 1, 2009
- 32,824
- 34,758
Hivi wale panya waliotangazwa kuwa wana uwezo wa kutegua mabomu ni kweli walikuwepo/wapo au au yalikuwa mambo ya wanasia tuuu? Kama wapo kwa nini wasipelekwe Mbagala wakafanye kazi yao? Saidia mimi jamani.
---------
SHIRIKA moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini.
Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania.
Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa na hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi, hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.
Uwezo kutokana na maumbile ya pua
Panya wanafundishwa jinsi ya kunusa wakiwa wadogo, kwa kuwekewa vitu vyenye madini ya milipuko. Tangu mwaka 2000, APOPO imekuwa ikiwafunza panya kwenye chuo cha Sokoine, Morogoro. Mwaka 2006 panya wa hao walianza zoezi la kutafuta mabomu ya ardhini huko Msumbiji.
Kabla ya panya kuanza kazi ya kunusa wapi mabomu yalipo, lazima wafuzu mtihani kutimiza viwango vya kimataifa vya kutambua mabomu ardhini.
Zawadi kwa ufanisi
Wakati wa mafunzo panya hupewa zawadi kwa kufuzu vizuri kwa sauti maalumu ambayo inaashiria kufuzu kwake na kupewa kipande cha ndizi kama zawadi.
Panya aliyefuzu vizuri huwa ana uwezo wa kuzunguka mita 400 za mraba kwa siku, wakati eneo kama hili litamchukua binadamu wiki mbili ili kuweza kugundua wapi kumefukiwa bomu.
Pua za kunyumbulika
Kulinganishwa na mbwa, panya wanaweza kutumiwa na mtu yeyote kwani hawana tabia ya kutokuwa na mahusiano ya karibu na mtu aliyemfundisha kama walivyo mbwa.
Panya anaweza kufanya kazi ya kufichua mabomu, hata kama aliyemfundisha hayupo na huwa wanafanya kazi vizuri kwa ufanisi na mtu yeyote hakuna shida kwa panya aliyefundishwa Tanzania, kwenda kufanya kazi Msumbiji, Angola, Thailand na Kambodia.
Kazi nchini Msumbiji
Hadi kufukia sasa nchini Msumbiji, zaidi ya mita za mraba milioni 6,5 za ardhi zimeshachunguzwa na mabomu 2,000 yaliyotegwa ardhini yamepatikana na kuharibiwa, pia bado mabomu 1,000 kuteguliwa na bunduki na silaha nyingine ndogo 12,000 zilipatikana.
Na mpaka sasa kuna makundi saba yenye watu 54 ambayo yanashughulika na kazi ya kutegua mabomu kwa kuwatumia panya.