Panya Magawa astaafu kazi ya kufichua mabomu kimataifa

Ben Zen Tarot

JF-Expert Member
Dec 13, 2014
1,773
2,000
Panya wa Tanzania mwenye sifa ya kufichua mabomu kimataifa astaafu Cambodia Magawa (panya) aliyejishindia tuzo kwa ushujaa wake anastaafu katika kazi yake ya kufichua mabomu yaliotegwa ardhini.

Kila ugunduzi alioufanya ulipunguza hatari ya kuumia au kifo kwa watu wa Kambodia. Katika kazi ya miaka mitano aliyofanya Hadi leo Magawa amefanikiwa kugundua mabomu 71 yaliotegwa ardhini pamoja na vilipuzi kadhaa nchini Cambodia na kumfanya kuwa HeroRAT aliyefanikiwa zaidi wa APOPO

Wasimamizi wake wanasema kwamba panya huyo mwenye umri wa miaka saba ameanza kupunguza kasi yake akielekea kuwa mzee na anahitaji kuheshimu mahitaji yake

Magawa ni panya mkubwa wa kijeshi wa kiafrika aliyezaliwa nchini Tanzania mnamo Novemba 2014. Alikulia katika kituo cha Mafunzo na Utafiti cha APOPO nchini Tanzania ambapo alijifunza jinsi ya kupata vilipuzi kwa kutumia hisia zake za ajabu za kunusa. Magawa kisha alihamia Siem Reap huko Cambodia mnamo 2016, ambapo alianza kazi yake yenye mafanikio.

FB_IMG_1622876996965.jpg
 

Alexander The Great

JF-Expert Member
Aug 28, 2018
4,076
2,000
Dah kama namuona na miwani yake puani akipanga foleni "NSSF na PSSSF" kusubiri mafao yake ya uzeeni.

Luteni Magawa kwa umri aliokua nao wa miaka 7 pamoja na asili yake (Panya), anaweza akawa na mzigo wa kilo 5 za pum*u .

Hawa panya wa majumbani tu huwa wana vifurushi nyuma kisawasawa kama amefunga tela. Akikupita wakati mwingine mpaka unajitafakari mara mbili mbili kwa jinsi anavyopita taratibu tena kibabe kweli kweli huku mzigo nyuma ukining'inia. Paka mwenyewe kuna wakati anasita hata kumfukuza anazuga zake kama hajamuona (Na kama hamna mtu nyumbani basi paka anatoa na "Shikamoo Mzee" au anapiga "Mkuu pole na majukumu", imagine na hawafikishi hata mwaka kabla ya kutangulizwa mbele ya haki.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom