Panya "Ronin" kumpiku magawa kwa uteguaji mabomu

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kimesema panya dume "Ronin" anayefanya kazi ya kutafuta mabomu na vilipuzi nchini Cambodia, uwezo wake ni mkubwa unaokaribia kumzidi mtangulizi wake panya Magawa.

Ofisa Mawasiliano wa Mradi wa Apopo SUA, Humphrey Makusa, alisema hayo juzi katika kituo cha mradi huo kilichopo chuoni hapo kwamba panya Ronin aliyezaliwa Augosti 19, 2019 ana uzito wa kilo 15 na kwamba alipelekwa Cambodia Machi 6, 2021 baada ya kufuzu mtihani.

Kupitia mradi huo, alisema SUA wanafanya utafiti na kuwafundisha panya namna ya kutafuta mabomu yaliyotegwa ardhini na vipulizi kisha wanaofuzu wanasafirishwa kwenda kufanya kazi katika maeneo yaliyoathiriwa.
Makusa alisema kituo hicho kinafanya utafiti wa panya na kutoa mafunzo ambapo hadi sasa kina panya 164 na 64 kati ya hao wapo kwenye mafunzo ya kubaini mabomu.

Mkufunzi wa panya katika kituo hicho, Abouswai Msuya, alisema kwa zaidi ya miaka 30 wamefundisha panya kugundua mabomu yaliyotegwa ardhini. Alisema mafunzo huanza wakati panya akiwa na umri mdogo wa wiki nne kwa kuwaweka katika mazingira ya kuishi na binadamu ili kuwatoa uwoga.

Msuva alisema kuwa panya hao hufundishwa kusikia mlio fulani ambao unaashiria kuna chakula kimewekwa mahara na pia hufundishwa kutofautisha harufu ya mabomu chini ya ardhi ya TNT na harufu nyingine.
"Panya tunaowafundisha wanaweza kugundua mabomu hata yakiwa yamekaa kwa miaka 30 ardhini na kwamba mbali na Cambodia pia. panya hao wamefanya kazi nchi mbalimbali ikiwemo Msumbiji na Angola," alisema Msuya.

Panya Magawa alifuzu mitihani mwaka 2016 kisha kupelekwa kufanya kazi ya kutafuta mabomu na vipulizi nchini Cambodia ambapo akiwa huko alisifika katika kusaidia kugunduliwa zaidi ya mabomu 108 ya kutegwa ardhini. Septemba 2020, Shirika lisilo la kiserikali la Matibabu ya Wanyama la Uingereza (PDSA) lilimtuza panya Magawa medali ya dhahabu kutokana na ushujaa na kujitolea kuokoa maisha ya watu nchi ya Cambodia.

Magawa alistaafu kazi mwaka 2021 na baada ya hapo kituo cha Apopo kilipeleka panya wengine 45 nchini humo akiwemo Ronin ambaye alifundishwa kwa mwaka mmoja kisha kuanza kazi Machi 6, 2021 na hadi sasa juhudi zake zinakaribia kumpita Magawa.

Soma:

- Panya Mtanzania atunikiwa nishani ya Dhahabu kwa umahiri wake wa kubaini mabomu ya kutegwa ardhini
 
Back
Top Bottom