Jinsi panya wanavyofundishwa kugundua mabomu SUA Morogoro kitengo cha APOPO

Wanasayansi wa Kitanzania ktk Chuo Kikuu cha Sokoine Morogoro wakishirikiana na Jeshi la Wananchi wa Tanzania, JWTZ wamefanikiwa kufanya yale ambayo kabla ya hapo yaliwezekana kwenye science fiction movies tu!
Wameweza kuwadilisha Panya Buku kutoka kuwa wanyama waharibifu kwa binadamu kwenda kuwa wanyama wenye manufaa!

Wamefanikiwa hili kwa kuwalea na kuwafundisha Panya Buku hawa kugundua vijidudu aina ya Bakteria ambavyo husababisha ugonjwa wa Kifua Kikuu (TB), na hili hufanyika kama ifuatavyo; Sampuli mbalimbali za makohozi hupangwa kwa mfwatano halafu Panya buku huachwa na kuanza kunusa kila Sampuli na kama Panya Buku akigundua Sampuli yenye Bakteria basi hugandisha pua yake hapo na kubakia hapo. Tayari nchi ya Thailand imeshaanza kuagiza Panya Buku ktk Tanzania kwa kazi hiyo ya kugungua Kifua Kikuu!

Matumizi mengine makubwa ya Panya Buku wa ktk TZ na labda ya muhimu kuliko yote ni kugundua Mabomu yaliyozikwa chini ya ardhi (land mines) na hili hufanyika kama ifuatavyo; Panya Buku hufungwa kwa kamba ndefu shingoni na hupelekwa sehemu iliyoathirika kwa mabomu na hapo kwa kutumia uwezo mkubwa wa kunusa panya Buku huanza kukwangua chini pindi anusapo bomu na kulingana uwepesi wake huzuia Bomu kulipuka!

Panya buku hawa sasa hivi wanatumia sehemu mbali mbali Duniani kama Msumbiji na kuokoa Maisha ya watu!



View attachment 232195View attachment 232196View attachment 232197View attachment 232198View attachment 232199View attachment 232200View attachment 232201
 
Kazi nzuri sana, waanze kujitangaza na kuwatangaza hao panya buku kwenye mashirika makubwa ya vifaa vya Tiba na Kivita....!!

Ni mwanzo mzuri na biashara nzuri sana itafanyika hapo wawe serious.....!!!!!

BACK TANGANYIKA
 
Have they published their findings in any peer reviewed journal? Can you share the link? limetumbuka

Hii mbona ni ya muda sana, na kuna documentary BBC inayoonyesha hao panya na walishapelekwa Mozambique kufanya zoezi hilo la kutafuta landmines?

Just google Apopo project au nenda Website ya BBC na search for Rats : scratch and sniff landmines detections
 
Last edited by a moderator:
Pole sana kama ndo umeisikia leo hii makitu! APOPO wako siku nyingi sana pale SUA na utafiti huo. Panya hao pia wantumika kugundua mabomu yaliyofukiwa ardhini
 
Miaka zaidi ya 15 iliyopita nilipita pale Sua walikuwa wameanza kazi hiyo siyo jambo jipya sana, ila ni kazi nzuri naunga mkono sana juhudi hizi na Sua kwa utafiti wapi vizuri kuliko chuo kikuu kingine Tanzania
 
Back
Top Bottom