Jinsi panya wanavyofundishwa kugundua mabomu SUA Morogoro kitengo cha APOPO

Ngalikihinja

JF-Expert Member
Sep 1, 2009
30,875
30,595
Hivi wale panya waliotangazwa kuwa wana uwezo wa kutegua mabomu ni kweli walikuwepo/wapo au au yalikuwa mambo ya wanasia tuuu? Kama wapo kwa nini wasipelekwe Mbagala wakafanye kazi yao? Saidia mimi jamani.

---------

SHIRIKA moja lisilo la kiserikali la Ubelgiji APOPO limeanza kuwafundisha panya namna ya kutambua mabomu yaliyofukiwa ardhini.

Panya hao ambao ni wakubwa kuliko panya wa kawaida wanafanyiwa majaribio Morogoro Tanzania.

Panya.jpg
Inaaminika wanauwezo mkubwa wa kunusa kuliko mbwa na hii inatokana na kuwa pua zao zipo karibu na ardhi, hali ambayo inawasaidia katika kazi yao ya utambuzi wa mabomu.

Uwezo kutokana na maumbile ya pua

Panya wanafundishwa jinsi ya kunusa wakiwa wadogo, kwa kuwekewa vitu vyenye madini ya milipuko. Tangu mwaka 2000, APOPO imekuwa ikiwafunza panya kwenye chuo cha Sokoine, Morogoro. Mwaka 2006 panya wa hao walianza zoezi la kutafuta mabomu ya ardhini huko Msumbiji.

Panga 2.jpg
Kabla ya panya kuanza kazi ya kunusa wapi mabomu yalipo, lazima wafuzu mtihani kutimiza viwango vya kimataifa vya kutambua mabomu ardhini.

Zawadi kwa ufanisi

Wakati wa mafunzo panya hupewa zawadi kwa kufuzu vizuri kwa sauti maalumu ambayo inaashiria kufuzu kwake na kupewa kipande cha ndizi kama zawadi.

Panya aliyefuzu vizuri huwa ana uwezo wa kuzunguka mita 400 za mraba kwa siku, wakati eneo kama hili litamchukua binadamu wiki mbili ili kuweza kugundua wapi kumefukiwa bomu.

Pua za kunyumbulika

Kulinganishwa na mbwa, panya wanaweza kutumiwa na mtu yeyote kwani hawana tabia ya kutokuwa na mahusiano ya karibu na mtu aliyemfundisha kama walivyo mbwa.

Panya 3.jpg
Panya anaweza kufanya kazi ya kufichua mabomu, hata kama aliyemfundisha hayupo na huwa wanafanya kazi vizuri kwa ufanisi na mtu yeyote hakuna shida kwa panya aliyefundishwa Tanzania, kwenda kufanya kazi Msumbiji, Angola, Thailand na Kambodia.

Kazi nchini Msumbiji

Hadi kufukia sasa nchini Msumbiji, zaidi ya mita za mraba milioni 6,5 za ardhi zimeshachunguzwa na mabomu 2,000 yaliyotegwa ardhini yamepatikana na kuharibiwa, pia bado mabomu 1,000 kuteguliwa na bunduki na silaha nyingine ndogo 12,000 zilipatikana.

Na mpaka sasa kuna makundi saba yenye watu 54 ambayo yanashughulika na kazi ya kutegua mabomu kwa kuwatumia panya.
 
Labda walipelekwa Lindi na Mtwara wakajeruhiwa kule. Maana kule kwetu ile mboga ya kumalizia ugali mkubwa tu
 
Wale nadhani wamespecialise katika maeneo ambayo hakuna makazi ya watu kama mbagala...mbagalakuna kambi ya jeshi, mabomu, na watu.....sad indeed.
 
Au mie sielewi au nyie mmechanganya mambo na kuingilia kesi ya wale Panya buku wa SUA kichwakichwa.

Kutokana na kumbukumbu zangu ambazo huwa naziamini kwa asilimia 95, zinasema kuwa "Wale panya buku wanategua mabomu yaitwayo kwa Kiingereza -LANDMINES".

Yale ya Mbagala kuna ya aina nyingi sana hadi ya ndege (ni kama risasi kubwa sana), mizinga, vifaru nk na si landmines peke yake. Na ndiyo maana wanapelekewa nchi kama Msumbiji na Angola ambako kuna haya mabomu chini ya ardhi mengi sana yakikata miguu ya watu kama unavyomuona huyu jamaa kutoka Angola.

[ame]
 
Naona humu ndani kuna watu mabomu kabisa hivyo wakija kunusanusa wanaweza kutegua mijibomu iliyotegwa hapa JF.
 
Jibu hili hapa

"Licha ya juhudi nzito za serikali ya JK ya kutafuta mijibomu ya mbagala inayoendelea kurindima kila kukicha na kusababisha maafa,imeelezwa kama hata kama wale panya waliohitimu 'digrii' ya kutegua mabomu ktk Chuo Kikuu cha Kilimo Sokoine (SUA) watapelekwa eneo la tukio kusaidia kazi ya kutegua mabomu hayo...hawataweza kufanya lolote kwa maana watadata (watachanganyikiwa).

Akielezea kuhusu hilo mwishoni mwa wiki, Mratibu wa Mradi huo upande Jeshi la Wananchi wa Tanzania, Brig. Jenerali Charles Mzanila, alisema panya hao hawataweza kazi hiyo c'se wamefundishwa kubaini mabomu yaliyotegwa kwa mpangilio maalumu na ambayo yanakuwa hayajalipuka.

"Wanafanya kazi katika eneo ambalo halina alama ya mlipuko, kama kuna mlipuko watachanganyikiwa," alisema Brigedia Mzanila."
 
Panya hawana uwezo wa kutegua mabomu ya mizinga au vifaru.Mabomu yanayopigwa na mizinga na vifaru ni aina za projectiles and shells,na kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari kuwa mabomu yale mengi yalikuwa ni ya mortar,Grad p complex hii yote ni mizinga.

Hivyo basi sina budi kusema ajali ya mbagala ilitokana na mabomu ya mizinga na ndio sababau yalikuwa na kishindo kikubwa na kelele kali kama radi,kishindo kikubwa ni tabia ya mlipuko wa mabomu aina ya mortar na kelele kali kama radi ni tabia ya mabomu ya grad p complex ambayo ni rockets kwani rockets hutoa backthrust ambayo huleta kelele kama za radi kwani backthrust hii huwa ni mseto wa ni heat,light and sound.

kwa mabomu kutapakaa eneo kubwa la mbagala hiyo ni conclusion kuwa yalikuwa ni mabomu ya mizinga kwani yalitengenezwa kwa ajili ya kusafiri na kwenda kulipukia mbali na mahali yalipopigwa.

kwa data hizo ninajiridhisha kusema yalikuwa ni ya mizinga ambayo huitwa shells and projectiles.

Shells and projectiles zina inner detornation mechanism ambapo panya wetu hawezi kufika humo ndani ya bomu ili kulitegua kwani yako sealed.wakati land mines zina extrior mechanism ambazo panya wetu anaweza kucheza na mechanism na kuliharibu bomu.nawasilisha
 
jibu hili hapa

"licha ya juhudi nzito za serikali ya jk ya kutafuta mijibomu ya mbagala inayoendelea kurindima kila kukicha na
kusababisha maafa,imeelezwa kama hata kama wale panya waliohitimu 'digrii' ya kutegua mabomu ktk chuo kikuu cha kilimo sokoine (sua) watapelekwa eneo la tukio kusaidia kazi ya kutegua mabomu hayo...hawataweza kufanya lolote kwa maana watadata (watachanganyikiwa).

Akielezea kuhusu hilo mwishoni mwa wiki, mratibu wa mradi huo upande jeshi la wananchi wa tanzania, brig. Jenerali charles mzanila, alisema panya hao hawataweza kazi hiyo c'se wamefundishwa kubaini mabomu yaliyotegwa kwa mpangilio maalumu na ambayo yanakuwa hayajalipuka.
"wanafanya kazi katika eneo ambalo halina alama ya mlipuko, kama kuna mlipuko watachanganyikiwa," alisema brigedia mzanila."

aaaah mapanya wenye degree ???
 
Au mie sielewi au nyie mmechanganya mambo na kuingilia kesi ya wale Panya buku wa SUA kichwakichwa.
Kutokana na kumbukumbu zangu ambazo huwa naziamini kwa asilimia 95, zinasema kuwa "Wale panya buku wanategua mabomu yaitwayo kwa Kiingereza -LANDMINES".
Yale ya Mbagala kuna ya aina nyingi sana hadi ya ndege (ni kama risasi kubwa sana), mizinga, vifaru nk na si landmines peke yake. Na ndiyo maana wanapelekewa nchi kama Msumbiji na Angola ambako kuna haya mabomu chini ya ardhi mengi sana yakikata miguu ya watu kama unavyomuona huyu jamaa kutoka Angola.

http://www.youtube.com/watch?v=dfA7N2SISCM

huyo jamaa mbona simwoni vizuri,.....naona tu wakina yoyo wanakata viuno......
 
huyo jamaa mbona simwoni vizuri,.....naona tu wakina yoyo wanakata viuno......

Jamaa anaonekana vizuri tu ila sema Video yenyewe imekaa Ki-Angola Angola. Basi labda angalia hii ambayo anaonekana vizuri kabisa kama John Silver (aka John Fedha).

[ame]http://www.youtube.com/watch?v=n3rBUktOIjM[/ame]
 
Jamani mkae mkijua kuwa yaliyo au yanayolipuka Mbagalairaq si mabomu bali ni misiles au marocketi kwa lugha nyingine ni katyusha na marisasi ya mizinga ,na kidogo maguruneti mawili matatu ,hivyo msikae mkidanganywa kuwa na mabomu ,ipo tofauti kubwa kati ya mabomu na vitu vinavyolipuka hapo Mbagalairaq.
 
Panya hawana uwezo wa kutegua mabomu ya mizinga au vifaru.Mabomu yanayopigwa na mizinga na vifaru ni aina za projectiles and shells,na kama ilivyoripotiwa na vyombo vya habari kuwa mabomu yale mengi yalikuwa ni ya mortar,Grad p complex hii yote ni mizinga.Hivyo basi sina budi kusema ajali ya mbagala ilitokana na mabomu ya mizinga na ndio sababau yalikuwa na kishindo kikubwa na kelele kali kama radi,kishindo kikubwa ni tabia ya mlipuko wa mabomu aina ya mortar na kelele kali kama radi ni tabia ya mabomu ya grad p complex ambayo ni rockets kwani rockets hutoa backthrust ambayo huleta kelele kama za radi kwani backthrust hii huwa ni mseto wa ni heat,light and sound.
kwa mabomu kutapakaa eneo kubwa la mbagala hiyo ni conclusion kuwa yalikuwa ni mabomu ya mizinga kwani yalitengenezwa kwa ajili ya kusafiri na kwenda kulipukia mbali na mahali yalipopigwa.
kwa data hizo ninajiridhisha kusema yalikuwa ni ya mizinga ambayo huitwa shells and projectiles.
Shells and projectiles zina inner detornation mechanism ambapo panya wetu hawezi kufika humo ndani ya bomu ili kulitegua kwani yako sealed.wakati land mines zina extrior mechanism ambazo panya wetu anaweza kucheza na mechanism na kuliharibu bomu.nawasilisha

......NDIO Mzee wa ARTILLERY,NIAMBIE PANYA WANATEGUA MABOMU AU WANAO UWEZO WA KUONESHA LILIPO BOMU ILI LIWEZEKULIPULIWA KWA KUTUMIA MIKONO AU VIFAA MAALUMU(MECHANICAL METHOD)
 
Mkuu mwiba heshima mbele,
Ninapenda kutoa ufafanuzi wa kutoka katika hoja zako kuwa kufauata mstari kwa mstari kwa manufaa ya wanaJF

1.Kwa hapa kwetu Missiles zinatumika na Jeshi la anga tu (Air defence artillery) katika stock ya mbagala hazikuwepo,

2. Mabomu jamii ya Rocket ni kweli yalikuwepo na ni yale yanayorushwa na mzinga aina ya Grad p complex na BM 21

3. Katyusha si aina ya mabomu bali ni aina ya mzinga uliotengenezwa na USSR katika world war 2.(Katyusha hutumika kupigia au kurusha maroketi.kwa lugha nyepesi Katyusha hufanya kazi kama bunduki (means of launching) na Rocket ni kama ilivyo risasi (Projectile).

4.Hakuna Mizinga unaotumia risasi bali inatumia mabomu.
naomba kuboresha mada kwa ufafanuzi huo nilioutoa na kusisitiza kuwa mabomu ndio yaliyolipuka mbagala.
 
"NDIO Mzee wa ARTILLERY,NIAMBIE PANYA WANATEGUA MABOMU AU WANAO UWEZO WA KUONESHA LILIPO BOMU ILI LIWEZEKULIPULIWA KWA KUTUMIA MIKONO AU VIFAA MAALUMU(MECHANICAL METHOD)"
__________________
Mkuu Shycas
Panya anaonyesha na Engineer anategua baba.
 
Mkuu mwiba heshima mbele,
Ninapenda kutoa ufafanuzi wa kutoka katika hoja zako kuwa kufauata mstari kwa mstari kwa manufaa ya wanaJF
1.Kwa hapa kwetu Missiles zinatumika na Jeshi la anga tu (Air defence artillery) katika stock ya mbagala hazikuwepo,
2. Mabomu jamii ya Rocket ni kweli yalikuwepo na ni yale yanayorushwa na mzinga aina ya Grad p complex na BM 21
3. Katyusha si aina ya mabomu bali ni aina ya mzinga uliotengenezwa na USSR katika world war 2.(Katyusha hutumika kupigia au kurusha maroketi.kwa lugha nyepesi Katyusha hufanya kazi kama bunduki (means of launching) na Rocket ni kama ilivyo risasi (Projectile).
4.Hakuna Mizinga unaotumia risasi bali inatumia mabomu.
naomba kuboresha mada kwa ufafanuzi huo nilioutoa na kusisitiza kuwa mabomu ndio yaliyolipuka mbagala.

Mkuu wanikumbusha JKT miaka ilee.....
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom