Jiji liondoe zile palm trees pale Mlimani City

M-bongotz

JF-Expert Member
Joined
Jan 7, 2010
Posts
1,736
Reaction score
411
Ni wiki 2 zilizopita tu tulishuhudia hekaheka za maandalizi ya mkutano wa World Economic Forum pale Mlimani City, katika maandalizi yale kuna ile miti ilipandwa katikati ya barabara ile ya Sam Nujoma, nadhani lengo lilikuwa ni kuwahadaa wageni kuwa Bongo ni ever green, sasa mkutano umeisha ile miti inakauka pale na badala ya kuwa mapambo sasa inakuwa ni uchafu, nadhani kwa kuwa mkutano umekwisha jiji lingefanya mpango wa kutuondolea magogo yale tuendelee na hali yetu tuliyoizoea.
 
Itaota vizuri kabisa, baada ya muda mfupi itachipua.
Si mnakumbuka millenium tower walipanda palmz kubwa kabisa?
 
hakuna haja ya kung'oa, ile miti inashika kwenye ardhi, itachipuka tena, itapendeza sana, italifanya lile eneo liwe na mvuto....kaangalie pale Kempisink Hotel the old Kilimanjaro Hotel, walipanda yakiwa makubwa hivyo hivyo .
 
Tusubiri wageni wengine wakija wataoa hii ya zamani na kuweka mipya!
 
Kwa nini waing'oe, itashika tuu na kuhalalisha gharama za kila mti ni zaidi ya milioni, kila mti umenunuliwa kwa 700,000/= hii ni gharama ya mti, usafiri, na winchi la kupandikiza/kusimika. Labor charge ya kuchimba mashimo, kuipandikiza, mbolea na maintainance kwa kila mti, itazidi 300, 000/= ila gharama hizi za ziada zitajumlishwa kwenye gharama za ziada za mradi.

Mgeni aje mwenyeji apone, jamani huko ndio kupona kwenyewe, hiyo milioni ingenunua vitanda 10 vya wodi ya wazazi pale Mwananyamala hospitali ili Mama zetu wajawazito angalau walale wawili wawili, kuliko sasa watatu watatu hivyo kupelekea wengine walale chini.

Haya October ndiyo hiyo, tutawachagua tena kwa ushindi wa kishindo!
 
hapo hawajafanya kosa bwana, hata kama nchi imeoza bora kunawa uso utongotongo usionekane kwa watu, haujui kuwa utanashati huficha umasiikini? waiache tu hapohapo,
 
Nimepita jana nikajiuliza swali hilo hilo kwamba hii miti itapona? ni kweli miti imeanza kupona kwa hiyo hakuna haja ya kuiondoa cha kufanya sasa ni kupanda mingine hadi mwisho ili kuweka madhari barabara hii nzuri kupendeza zaidi.
 
Hii policy ya mgeni njoo mwenyeji apone haifai kabisa. Kama hakuna wageni basi ndo tumekufa?
 
Swali langu ni kuwa je miti hii huwa inaota yenyewe bila kumwagiwa maji? what if masika ikaisha Dra na tukaona UVIVU wa kuimwagia maji?
 
Ni wiki 2 zilizopita tu tulishuhudia hekaheka za maandalizi ya mkutano wa World Economic Forum pale Mlimani City, katika maandalizi yale kuna ile miti ilipandwa katikati ya barabara ile ya Sam Nujoma, nadhani lengo lilikuwa ni kuwahadaa wageni kuwa Bongo ni ever green, sasa mkutano umeisha ile miti inakauka pale na badala ya kuwa mapambo sasa inakuwa ni uchafu, nadhani kwa kuwa mkutano umekwisha jiji lingefanya mpango wa kutuondolea magogo yale tuendelee na hali yetu tuliyoizoea.

Nimekubali watanzania tu wasanii mbayaaa, yaani wageni wameingia mkenge wakijua tuko safi kwenye kutunza mazingira kumbe ni famba kabisa, tunatisha.Hii inahamia kwenye mambo mengine kama mikataba ya madini na hata mambo muhimu ya kuendesha shughuli za serikali kisha baadae tunakwama kama hio miti inavyotuumbua kwa kukauka, mfanya jamaa wa WEF wakarudi ghafla leo si aibu hii.Jamani viongozi tuwe serious na kila tunachofanya sio kuleta usanii kwa kila jambo.Toene uchafu wenu hapo eboooo...
 
si uliona walivyopiga deki barabara arusha kipindi clinton alipokuja, hadi akasifia ati Arusha ni Geneva ya africa, ukienda sasahivi arusha utafikiri Temeke na mbagala.
 
Subirini mvua ziishe uone yatakavyo nyauka
Wasiingie hizo gharama yatakufa kama kawaida yetu
Twajua kutunza vitu sembuse kutengeneza
 
kuota itaota akuna shida, tatizo ni kwamba wageni wameshaondoka je kuna atakayekumbuka tena kuiendeleza kweli
 
acheni ushamba ile miti ndio ishaoteshwa
nani amewaambia kuwa ilikua kwa ni kwa
ajili ya mkutano?
 
mwenye picha apige aweke hapa basi, sisi wengine hatujui mazingira yamekuwaje hapo kwa sasa
 
Back
Top Bottom