Wakuu, hatua lilipofikia hili jiji la Dar es Salaam, hakuna tena hamasa watu kwenda Ulaya au US kupiga picha

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,142
2,000
Tulizoea zamani mtu akienda Ulaya atalazimisha atafute angle ili apige Picha background imtambulishe hayuko Tanzania.

Jana baada ya miezi kama tisa hivi kukaa upande mmoja wa jiji LA DSM bila kuzunguka niliachwa mdomo wazi.

1: Kuna Majengo Mapya makubwa mazuri hatari. Mfano mitaa ya Makumbusho Victoria yaani hadi unatabasamu tu kwa jinsi miundombinu na design zilivyosambazwa pale. Lililoniacha hoi ni jengo moja hivi maeneo ya palm beach. Ile kitu ni matata sana. What a design!

2: Kale kadaraja ka masaki baharini mwanzoni nilidhani ni vile kama vya Miti chini kwa chini Jana nimeshangaa kunastructure za hatari wanazimount pale kumbe ni kitu hatari Sana.

3: Nikapita Ubungo Simu2000 na stand ya mabasi napo kuna road zimesukwa pale ndani ya muda mfupi utapenda. Naona wanajiandaa kuweka taa za barabarani ukiongezea Interchange. Alafu ukichungulia kuelekea Mlimani city aisee pako Bomba sana.

4: Nikachungulia CCBRT, hadi nikadhani nimekosea njia. Kuna zinga la hospitali. Yaani Majengo mengi Mapya mageti mengi ya kuingilia hawajaifungua. Hadi nikajiuliza kwa nini hata Mloganzila ilijengwa. Maana kile nilichokiona Wenda hata Muhimbili inaweza isifue dafu licha ya Eneo kuwa dogo.

Nikapita Mbagala, kuna structure flani barabarani zinainuliwa pale nadhani ni kwa ajili ya mwendokasi au sijui ni daraja basi napo patakuwa poa sana.

Kimsingi nina mpango wa kwenda nchi kadhaa Ulaya lakini nikifika nitapiga Picha kwenye mabarafu tu ila Majengo kama background sidhani maana hicho nilichokiona Jana hata Ulaya hakuna.

Msema Kweli ni mapenzi wa Mungu. Natamani kupata Picha ya aerial views current ya maeneo mengi ya jiji.
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,293
2,000
Hii nchi hela nyingi Sana Inaenda kwenye miundo mbinu hasa barabara Kwa Gharama za ufukara wa wananchi...... Kuna jamaa angu engineer huwa namwambia msipopiga hela utawala huu, utawala mwingine ukija mtalia na kusaga meno
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,142
2,000
Hii nchi hela nyingi Sana Inaenda kwenye miundo mbinu hasa barabara Kwa Gharama za ufukara wa wananchi...... Kuna jamaa angu engineer huwa namwambia msipopiga hela utawala huu , utawala mwingine ukija mtalia na kusaga meno
Wanapigaje Mkuu. Maana naona kila mfanyakazi anahofu ya kukamatwa. Kila mtu anamuona mwenzake kama shushushu na informer wa Mkuu. Inabidi uwe na akili nyingi katika kupiga huko usimshike Mkono kipofu ukashtukiwa.

Ila Barabarani zimesukwa aisee. Tungejengewa kamoja kwetu kaseme na sisi tungepiga business saana msimu huu. Maana nimegundua barabara na umeme ndio kila kitu aisee
 

Slowly

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
4,293
2,000
Wqnapigaje Mkuu. Maana naona kila mfanyakazi anahofu ya kukamatwa. Kila mtu anamuona mwenzake kama shushushu na informer wa Mkuu. Inabidi uwe na akili nyingi katika kupiga huko usimshike Mkono kipofu ukashtukiwa...
Mkuu hii nchi watu wanapiga hela Sana Acha Tu , mwamba wangu yupo Tanroad kulaza million 100, au 50 kwenye miradi ni kitu cha kawaida sana , na miradi ni mingi hatari.
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,142
2,000
Ulaya sehemu gani umefika ili tuone ufananisho wako lama una mantiki.
Nalinganisha Picha zawadau wangu walio Ulaya wanazopiga kwa kutumika nguvu nyingi kutafuta background zenye mvuto wa kimiundombinu naona hata huku ni zaidi.

Sio lazima ufike. Hata Googlesatellite unaweza kutembezwa manispaa nzima za Mimi mingi ya Ulaya. Tena ukapewa na 3D view.

Kuna mlaya mmoja tulikuwa tuazunguka akinitembeza kwa google satellite mitaa ya Ireland yote hadi chumba alichopanga tunavuta hadi Dirisha. Kawaida sana
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,142
2,000
Msukuma toka ikungulyabashashi
Mkuu nilikuwa nauza ng'ombe Pugu narudia huko huko. Kwa kweli nilifarijika sina haja ya kuingia Ulaya na Kamera tena. Hizo KAZI nilizoziona nikipiga Picha zinatosha kabisa kuwa background sawasawa na tour zangu nikizianza Ulaya
 

ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,731
2,000
Tulizoea zamani mtu akienda ulaya atalazimisha atafute angle ili apige Picha background imtambulishe hayuko Tanzania.

Jana baada ya miezi kama tisw hivi kukaa upande mmoja wa jiji LA DSM bila kuzunguka niliachwa mdomo wazi....
Uko vizuri kwa kuandika story aiseee jinsi ulivokusanya habari na kuzielezea kongole zako mkuu
 

matunduizi

JF-Expert Member
Aug 20, 2018
3,142
2,000
Wakuu walahi kabisa siku natua Ulaya nitakuwa bize na mishe zangu kuuza sura nikiamua hiki nilichokiona kimenistosha kabisa.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom