Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

halafu , hivi hizi simu kali kama galaxy s7 edge au s8 edge inayoukuja, hua zipo za dual line? maana me nakubali sana simu zenye dual line
zipo version za single sim, dual sim standby na dual sim active.
 
Huyu ni kuadi wa wamarekani. Ukisema simu za mkorea unamaana tuache SAMSUNG ?
Hauko sawa sawa naona
usisome kichwa cha habari na kucoment soma habari nzima, haihusu wakorea tu bali hata wamarekani

pia haihusu mahali kampuni ilipotoka bali mahala simu ilipomaanishiwa kuuzwa. hakuna mtu alokataza usinunue samsung wala simu yoyote humu, umekatazwa usikimbilie simu ambazo hazijatengenezwa kwa ajili ya soko lako.
 
Hivi mkuu Chief-Mkwawa Samsung grand prime inayouzwa hapa Africa, ni sawa na Samsung grand prime inayouzwa marekani, ulaya na kwingineko duniani? Naomba kujua mkuu.
 
Hivi mkuu Chief-Mkwawa Samsung grand prime inayouzwa hapa Africa, ni sawa na Samsung grand prime inayouzwa marekani, ulaya na kwingineko duniani? Naomba kujua mkuu.
grand prime ni ile ile sema kuna grand prime na grand prime plus

hii yenye plus ndio ya kwetu huku. ila hio prime ipo kote.
 
grand prime ni ile ile sema kuna grand prime na grand prime plus

hii yenye plus ndio ya kwetu huku. ila hio prime ipo kote.
Ahaa nimekupata mkuu; ila kwanin hii plus iwe ni kwa Africa tu? Tofauti na prime kiuwezo ni ipi mkuu? Na zote huwa zina 4g? Halafu kuna hii inaitwa Samsung grand core prime yenyewe ina 4g vip hapa bongo zipo?
34408b2d63ee96f6b3e2612eb7d33865.jpg

Halafu mkuu tofauti ya Version na Verizon ni ipi mkuu?
 
hio plus ni ya mediatek, na simu za mediatek nyingi zina matatizo ya kutumia technology ambazo hazijasajiliwa kwenye nchi kubwa mara nyingi wanashtakiwa, pia ni simu ya low quality wenzetu nchi kama marekani hata mtu masikini ana uwezo wa kununua simu highend sababu wananunua kwa mikataba.

karibia zinafanana prime zote ila mimi naona prime ya kawaida ni nzuri zaidi hasa kwa baadae sababu hakuna custom rom za maana za mediatek.

na ndio zote zina 4g.

core prime pia ipo yenyewe ni ndogo kidogo kwa grand prime, ni ya muda kidogo na bei zake za mkononi hata 100k unazipata.

version ni neno la kingereza linalomaanisha toleo kwa kiswahili wakati verizon ni jina la mtandao wa simu wa marekani.
 
naomba tofauti ya dual sim standby na dual sim active
-dual sim standby simu inakuwa na line mbili lakini ukitumia line moja line nyengine inakuwa haipatikani. mfano line 1 ni tigo na line 2 ni voda mtu akapiga tigo mkawa mnaongea, mwengine akipiga voda hakupati

-dual sim active Iine zote zinapatikana na mtu anaweza kukupigia line 1 na mwengine akapiga line 2 ukamueka hold line 1 na kupokea line 2.
 
kwa uimara ndio inaweza kuwa bora zaidi, na kuna wakati pia zinakuwa na processor bora zaidi, nakumbuka s4 ya korea ilikuwa ya kwanza kuwa na core 8 wakati ya kimataifa ikiwa na core 4.

lakini kimatumizi ya kawaida inaweza sumbua sana, mfano simu haina ussd au simu haina custom rom hata moja unaishi vipi hapo?
Kiukweli mpaka leo hii mtu akisema custom rom sielew kabisa msaada plz
 
Kiukweli mpaka leo hii mtu akisema custom rom sielew kabisa msaada plz
kila simu inakuwa na operating system, hizi operating system huekwa na mtengeneza simu mwenyewe, mfano simu ya samsung operating system yake ni android na android yao wameimodify muonekane wake na kuitwa touchwiz. sasa hii android kwenye simu ya samsung imeekwa na samsung wenyewe.

custom rom ni operating system ambayo imeekwa na mtu tofauti na mtengeneza simu, mfano mimi nikiamua kutengeneza operating system yangu inayotokana na android kwa ajili ya samsung then itaitwa custom rom.

hivyo kifupi custom rom ni os ambayo sio official kwa ajili ya simu.
 
yap msimamo upo vile vile, na sio Tecno tu hadi brand kubwa wanaodanganya watu na vimeo vya mediatek nitawaambia watu wasinunue.

japo mediatek ame improve sasa hivi, nitarecomend zile simu zinazotumia hizo improved processor tu.
Vipi mediatek ya hTc one e9+ dual sim?
 
Vipi mediatek ya hTc one e9+ dual sim?
helio x10 ni decent soc lakini kwa mimi siwezi acha snapdragon 800/801 nikanunua simu ya helio x10.

hivyo itategemea kama utaipata bei rahisi kuliko note 3, note 4, lg g3, galaxy s5, htc m8 etc then sio mbaya ila kama hizo zipo ni bora hizo.
 
Nmekuelewa mkuu,mimi pia sio mfuasi kabisa wa mtk,ila tangu nmeanza kuitumia kwenye hii hTc one e9+ nmependezwa nayo na inasuport pia ya custom roms kibao.
 
Nina simu Samsung galaxy mega model namba ni SGH-M819N niliba dilisha kioo nikaweka namba kwa muda kidogo sasa nimeitoa niitumie naona laini inaonesha majina ila network hakuna kitu kuna muda inaonesha muda mwingine hakuna kitu msaada wakuu
 
pengine ni issue ya duplicate imei, umejaribu mitandao yote?
 
Back
Top Bottom