Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

Samahani mkuu...
Hivi njia ya ku-root simu zenye android version ya 6. 0 bila kutumia PC ishapatikana?
Maana nataka nikaroot haka ka simu...

inategemea na model na model ukigoogle model yako inakuaje?
 
kuna samsung z2 ina os ya tizen lakini unaweka pia apps za android hivyo vi opera mini, whatsapp, fb vyote vipo.

sijajua bongo wanaiuza sh ngap maana wakati naenda dukani walisema hazijafika bado ila mabango yao wameshaanza kuyaeka.

kenya wanaiuza 6,000 (130,000 ya Tanzania),

ina 4g, quadcore, 1gb ram etc ni simu nzuri kuliko y3.

pia kuna j1 mini ukiitafuta vizuri unaipata bei hio
z2 ina battery capacity 1500mAh. Unazungumziaje hapo? Ni ndogo ukicompare kwa zile za Tecno
 
z2 ina battery capacity 1500mAh. Unazungumziaje hapo? Ni ndogo ukicompare kwa zile za Tecno
hio ni tizen sio android usitegemee battery life zifanane na tecno battery life ni mbovu sana, sababu inatumia mediatek.

halafu tu assume tecno batterylife ni kubwa

-z2 ina 4g wakati y3 haina
-z2 ina ram 1gb wakati y3 ni 512mb
-z2 camera ni 5mp wakati y3 ni 2mp
-z2 processor ni quadcore 1.5ghz wakati y3 ni dual core 1.0 ghz
-mwaka 2017 bado tecno wanauza simu zenye 3g 7.2mbps wakati z2 3g yake ni 21/42mbps

yani kila idara Y3 kapitwa, tena na samsung kampuni yenye low end mbaya, bado tu huoni mnaliwa na Tecno?
 
Chief umesema samsung ni kampuni zinazotengeneza simu za low end za kiwango cha chini.

Unaweza kunisaidia kampuni zipi zinazotengeneza low end za kiwango kidogo kilingana na kipato chetu wabongo?
 
aysee...sasa inakuaje ndo wanaongoza kwa brand ya simu inayotumiwa sana bongo, nigeria
 
hio ni tizen sio android usitegemee battery life zifanane na tecno battery life ni mbovu sana, sababu inatumia mediatek.

halafu tu assume tecno batterylife ni kubwa

-z2 ina 4g wakati y3 haina
-z2 ina ram 1gb wakati y3 ni 512mb
-z2 camera ni 5mp wakati y3 ni 2mp
-z2 processor ni quadcore 1.5ghz wakati y3 ni dual core 1.0 ghz
-mwaka 2017 bado tecno wanauza simu zenye 3g 7.2mbps wakati z2 3g yake ni 21/42mbps

yani kila idara Y3 kapitwa, tena na samsung kampuni yenye low end mbaya, bado tu huoni mnaliwa na Tecno?
af me naona pia tatizo ni urahisi wa upatikanaji..ndo maana Tecno kasikilia soko sana, sababu anapatikana kwa urahisi. I wish simu kama hiyo z2 ingekua inapatikana kiurahisi kama Tecno zilivyojaa kkoo

sasa tatizo simu kama hiyo kupatikana shida...sio kamaTecno zilivyojaa kkoo
 
Chief-Mkwawa hiyo meizu m3 note ina support 4g kwa huku Tanzania
 
Chief umesema samsung ni kampuni zinazotengeneza simu za low end za kiwango cha chini.

Unaweza kunisaidia kampuni zipi zinazotengeneza low end za kiwango kidogo kilingana na kipato chetu wabongo?
motorola wapo vizuri kwenye premium low end, xiaomi wana simu nzuri pia za low end, series zao za redmi zipo level nyengine. lenovo pia naona anajitahidi na huawei kwenye honor pia wapo vizuri
 
flex 2 ni nzuri zaidi tena tofauti ni miaka 2,

sema inatumia snapdragon 810 ambayo ilikuwa inaheat sana,

hio z2 umeiona wapi 110k? maana hio bei inakaribiana na modem za 4g za tigo,
kkoo mtaa wa Uhuru pale RoundAbout kwenye lile jengo la Blue lenye maandishi ya tecno na samsung
 
af me naona pia tatizo ni urahisi wa upatikanaji..ndo maana Tecno kasikilia soko sana, sababu anapatikana kwa urahisi. I wish simu kama hiyo z2 ingekua inapatikana kiurahisi kama Tecno zilivyojaa kkoo

sasa tatizo simu kama hiyo kupatikana shida...sio kamaTecno zilivyojaa kkoo
samsung hawana shida ya supply zipo za kutosha maduka mengi ila oem wengine wakubwa kama LG, HTC, Sony, etc ni kama hawapo na wala hawana time na hili soko letu la Africa labda kwa nchi chache kama south Africa
 
kkoo mtaa wa Uhuru pale RoundAbout kwenye lile jengo la Blue lenye maandishi ya tecno na samsung
Samahan mkuu, unaweza kuniwekea picha ya hiyo sim ili nione inafananaje maana sifa zake zinaanza kunishawishi niende dukani
 
samsung hawana shida ya supply zipo za kutosha maduka mengi ila oem wengine wakubwa kama LG, HTC, Sony, etc ni kama hawapo na wala hawana time na hili soko letu la Africa labda kwa nchi chache kama south Africa
halafu , hivi hizi simu kali kama galaxy s7 edge au s8 edge inayoukuja, hua zipo za dual line? maana me nakubali sana simu zenye dual line
 
Asante kwa uelewesho wako murua kaka, nimekuuliza hivyo sababu hii iphone yangu nilinunua kwa mtu inafanya kazi fresh kabisa ila kuna baadhi ya vitu ipo tofaut kabisa na iphone zote nilizo wahi kutumia, kwanza hii simu nikiwa imezimwa nikichomeka chaja inaleta kibox cha chaja na inaendelea kuonesha inachaji kitu ambacho sijawahi kukiona kwenye iphone huwa najua iphone ukiichomeka kwenye chaja inawaka yenyewe automatic! Pili hii simu upande wa mwanga brightness hakuna sehem ya kufunga usijiongeze automatic! Tatu hii simu tangia niwe nayo namba za simu hazionekani sababu namba zangu zote naziwekaga kwenye icloud
801467fe34c313c17f8ec4ce932283af.jpg
6b325e0f6a20085fbd4dc076d3f2eef5.jpg
Ina apple store ama inakudirect store nyingine kudownload apps?
 
Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa na ndugu yangu mmoja mitaa ya Aggrey tukitafuta simu aina ya galaxy Note 4 mpya, huwezi kuamini tulizunguka maduka yanaweza kufika hata 100 lakini hatukupata hata note 4 moja ambayo ni ya kimataifa (Africa pia) zote zilikuwa ni simu ambazo wamezitoa kwenye mitandao ya simu ya Kimarekani, Korea na China pamoja na nchi nyengine kubwa kubwa. Simu hizi nyingi zilikuwa zimelokiwa na jamaa wamezi unlock na pia ni mbaya kwa matumizi yetu ya kitanzania, leo hii nimeona niandike thread hii kuelezea madhara ya hizi simu na pia tuelezane njia za kupunguza hayo madhara kwa wenye nazo.

Hupati updates, warranty wala support yoyote
Unaponunua simu hizi usitegemee kupata updates badala yake ukitaka update inabidi udownload manual, vile vile hata kama simu ni mpya ikiharibika inabidi urudishe ilipotoka. mfano una galaxy s7 ya kikorea ukiwapelekea samsung Tanzania hawatakutengenezea sababu haiwahusu. Hata mwenye duka akikwambia anakupa warranty ni muongo tu labda airudishe alipoitoa kama atakua tayari.

Zinasumbua ussd
Umeshanunua simu ukaona ukiuliza salio *102# inakubali lakini mpesa, tigopesa na vyengine vinakataa? ukiona hivyo ujue tayari upo mkumbo huu umeuziwa simu za kikorea na wenzie
connection-problem-invalid-mmi-code.png

Muda wote zinaandika 4g au kutoshika kabisa 3g
Watu wengi hufikiri simu zao zina 4g kumbe hazina, mitandao mingi ya kimarekani na baadhi ya nchi wanaitwa hspa+ kama 4g kitu ambacho sio sahihi, hivyo simu hizo zikija hapa kwetu huandika 4g hata kama mtandao ni wa 3g, ukiona simu yako ipo hivi ujue umeshauziwa hizi simu, pia kuna mitandao kama T-mobile band yao ni 1700mhz hivyo simu zao zinaweza zisishike kabisa 3g huku kwetu

Simu za CDMA na band tofauti
Pia simu hizi zipo za CDMA zinaweza kuja Tanzania zisishike kabisa network ukapata pengine 4g tu, na hio 4g inaweza iwe ni band ambazo hazikubali kwetu, mtandao pekee wa Tanzania wenye band za kichina china ni smart band 2300mhz hivyo ukiwa na simu ya namna hii angalia mtandao wa smart.

Zinakuja bila google play store
Nchi kama China playstore kwao sio maarufu, hivyo simu zao zikija huku kwetu zinasumbua unakuta haina playstore wala app yoyote ya google hivyo kuanza kukuhangaisha kuweka hizo app sometime inabidi hadi uflash simu

SMA charachter sio 160
Kikawaida sms moja huwa na herufi 160 (pamoja na space na namba) lakini simu hizi huwa na herufi chini ya 160 hivyo utakatwa hela nyingi zaidi pamoja na kuharibu mfumo mzima wa kutumiwa mfano mtu akituma msg ya 160 kwako itakuwa kama msg 2. kwa wale wanaotuma msg ni muhimu hii.
jw-ucEQB3dwV42Bl8OMBJR51HbdW-0rLyJoJvOsrr2IP_b2-LlhJd0Cx-qaW0JqM_54=h900

mfano hii ina charachter 70 tu hivyo msg ya 160 itahesabika kama sms 3

Dialer ya kikorea au kichina
Pia inaweza tokea dialer (ya kupigia simu) ikawa mfumo wa kikorea
main-qimg-6a4e834ec4324839357802e8b65ec023

Support ndogo ya developers
Pia simu hizi huwa na custom rom chache au usipate kabisa, njia za kuroot wakati mwengine zinakuwa ngumu, nyengine zinalokiwa bootloader etc kama wewe ni power user simu hizi zinakuwa pasua kichwa.

Hayo ni baadhi ya madhara ya simu za kikorea, kama kuna mengine nimeyasahau mutaniambia.

Namna ya kujua kama simu ni ya kikorea au international
Kusema simu inaitwa lg g2 au galaxy s5 haitoshi kila simu inakuwa na model zake, simu moja kama galaxy s5 inaweza kuwa na model tofauti tofauti hata 10, hivyo kujua simu yako fanya hivi

-Nenda setting halafu about utaona model number ya simu
Tap-on-device-name-under-settings.jpg

Ukiipata hio model number angalia online ni ya wapi, site kama gsmarena kwenye specs za simu hueka model na maeneo zinapotoka unatakiwa uwe na model international, au just google simu yako na neno international version kwa mbele, mfano galaxy s5 international version utapata model ya international kama huna hio ujue kuna uwezekano kupata madhara ya hapo juu

-Njia nyengine ni kuregister na warranty ya samsung sema njia hii ni kwa simu mpya zilizotoka chini ya miaka miwili iliopita.. utaandika neno REG*imei# halafu tuma kwenda 15685 utajibiwa, badili neno imei na imei halisi ya simu

jinsi ya kupunguza madhara ya simu za kichina

1.Badili app husika
Mfano dialer ina maneno ya kikorea nenda playstore install dialer nyengine tumia

2. Badili rom
Unaweza ukaeka custom rom kama cyanogen hii itasolve matatizo mengi tu

3. Mods mbali mbali
Kuna simu zinakubali kubadili bands zake na kueka bands za nchi yako, kuna mods za bootloader kwa wale ambao rom za international zinakataa etc

Una tatizo la simu za Kikorea? Usisite kulitaja hapo chini.
Useful, umedadavua vema. Nilitaka niiweke ila nisingefikia utaalamu wako. Niliwahi kuwa mhanga pia
 
Huyu ni kuadi wa wamarekani. Ukisema simu za mkorea unamaana tuache SAMSUNG ?
Hauko sawa sawa naona
 
Back
Top Bottom