Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

Jihadhari na simu za mitandao ya Kikorea, China na Marekani

Nimenunua Table iPad ya Apple zile first generation sasa kufanya updating kutoka kwenye old version to new version ambayo ios8. 0 imekataaaa, na wataalam husema haikubali tena ile##HIVI NI KWELI MKUU#
 
swali nje ya mada kidogo chief, hivi mtu akinunua modem vodacom inayokubali kuingiza line za vodacom tu, je akija kwangu nimflashie iingize line zote itakuwa kosa??
Kwani moderm (router) za vodacom zinaweza kufunguka na kutumia line za mitandao mingine?
 
Nimenunua Table iPad ya Apple zile first generation sasa kufanya updating kutoka kwenye old version to new version ambayo ios8. 0 imekataaaa, na wataalam husema haikubali tena ile##HIVI NI KWELI MKUU#
hio ni ios 5 mwisho huna ujanja.
 
Wiki kadhaa zilizopita nilikuwa na ndugu yangu mmoja mitaa ya Aggrey tukitafuta simu aina ya galaxy Note 4 mpya, huwezi kuamini tulizunguka maduka yanaweza kufika hata 100 lakini hatukupata hata note 4 moja ambayo ni ya kimataifa (Africa pia) zote zilikuwa ni simu ambazo wamezitoa kwenye mitandao ya simu ya Kimarekani, Korea na China pamoja na nchi nyengine kubwa kubwa. Simu hizi nyingi zilikuwa zimelokiwa na jamaa wamezi unlock na pia ni mbaya kwa matumizi yetu ya kitanzania, leo hii nimeona niandike thread hii kuelezea madhara ya hizi simu na pia tuelezane njia za kupunguza hayo madhara kwa wenye nazo.

Hupati updates, warranty wala support yoyote
Unaponunua simu hizi usitegemee kupata updates badala yake ukitaka update inabidi udownload manual, vile vile hata kama simu ni mpya ikiharibika inabidi urudishe ilipotoka. mfano una galaxy s7 ya kikorea ukiwapelekea samsung Tanzania hawatakutengenezea sababu haiwahusu. Hata mwenye duka akikwambia anakupa warranty ni muongo tu labda airudishe alipoitoa kama atakua tayari.

Zinasumbua ussd
Umeshanunua simu ukaona ukiuliza salio *102# inakubali lakini mpesa, tigopesa na vyengine vinakataa? ukiona hivyo ujue tayari upo mkumbo huu umeuziwa simu za kikorea na wenzie
connection-problem-invalid-mmi-code.png


Muda wote zinaandika 4g au kutoshika kabisa 3g
Watu wengi hufikiri simu zao zina 4g kumbe hazina, mitandao mingi ya kimarekani na baadhi ya nchi wanaitwa hspa+ kama 4g kitu ambacho sio sahihi, hivyo simu hizo zikija hapa kwetu huandika 4g hata kama mtandao ni wa 3g, ukiona simu yako ipo hivi ujue umeshauziwa hizi simu, pia kuna mitandao kama T-mobile band yao ni 1700mhz hivyo simu zao zinaweza zisishike kabisa 3g huku kwetu

Simu za CDMA na band tofauti
Pia simu hizi zipo za CDMA zinaweza kuja Tanzania zisishike kabisa network ukapata pengine 4g tu, na hio 4g inaweza iwe ni band ambazo hazikubali kwetu, mtandao pekee wa Tanzania wenye band za kichina china ni smart band 2300mhz hivyo ukiwa na simu ya namna hii angalia mtandao wa smart.

Zinakuja bila google play store
Nchi kama China playstore kwao sio maarufu, hivyo simu zao zikija huku kwetu zinasumbua unakuta haina playstore wala app yoyote ya google hivyo kuanza kukuhangaisha kuweka hizo app sometime inabidi hadi uflash simu

SMA charachter sio 160
Kikawaida sms moja huwa na herufi 160 (pamoja na space na namba) lakini simu hizi huwa na herufi chini ya 160 hivyo utakatwa hela nyingi zaidi pamoja na kuharibu mfumo mzima wa kutumiwa mfano mtu akituma msg ya 160 kwako itakuwa kama msg 2. kwa wale wanaotuma msg ni muhimu hii.
jw-ucEQB3dwV42Bl8OMBJR51HbdW-0rLyJoJvOsrr2IP_b2-LlhJd0Cx-qaW0JqM_54=h900

mfano hii ina charachter 70 tu hivyo msg ya 160 itahesabika kama sms 3

Dialer ya kikorea au kichina
Pia inaweza tokea dialer (ya kupigia simu) ikawa mfumo wa kikorea
main-qimg-6a4e834ec4324839357802e8b65ec023


Support ndogo ya developers
Pia simu hizi huwa na custom rom chache au usipate kabisa, njia za kuroot wakati mwengine zinakuwa ngumu, nyengine zinalokiwa bootloader etc kama wewe ni power user simu hizi zinakuwa pasua kichwa.

Hayo ni baadhi ya madhara ya simu za kikorea, kama kuna mengine nimeyasahau mutaniambia.

Namna ya kujua kama simu ni ya kikorea au international
Kusema simu inaitwa lg g2 au galaxy s5 haitoshi kila simu inakuwa na model zake, simu moja kama galaxy s5 inaweza kuwa na model tofauti tofauti hata 10, hivyo kujua simu yako fanya hivi

-Nenda setting halafu about utaona model number ya simu
Tap-on-device-name-under-settings.jpg

Ukiipata hio model number angalia online ni ya wapi, site kama gsmarena kwenye specs za simu hueka model na maeneo zinapotoka unatakiwa uwe na model international, au just google simu yako na neno international version kwa mbele, mfano galaxy s5 international version utapata model ya international kama huna hio ujue kuna uwezekano kupata madhara ya hapo juu

-Njia nyengine ni kuregister na warranty ya samsung sema njia hii ni kwa simu mpya zilizotoka chini ya miaka miwili iliopita.. utaandika neno REG*imei# halafu tuma kwenda 15685 utajibiwa, badili neno imei na imei halisi ya simu

jinsi ya kupunguza madhara ya simu za kichina

1.Badili app husika
Mfano dialer ina maneno ya kikorea nenda playstore install dialer nyengine tumia

2. Badili rom
Unaweza ukaeka custom rom kama cyanogen hii itasolve matatizo mengi tu

3. Mods mbali mbali
Kuna simu zinakubali kubadili bands zake na kueka bands za nchi yako, kuna mods za bootloader kwa wale ambao rom za international zinakataa etc

Una tatizo la simu za Kikorea? Usisite kulitaja hapo chini.

Ndyo maana nikahamia iPhone tu maana hao wengine wababaishaji. Na pia hizo simu huwa hazishiki 4G lte hapa bongo kutokana na defference ya bands na frequency. Mf inaweza kuwa 4G band 3 ila frequency ni 2100 wakati bongo ni band 3 frequencyo 850. NI HOMA TU, usidanganyike na nembo ya 4G lte kwa nyuma, UTAUMIA


USISEME MTANZANIAJEURI HAKUKWAMBIA
 
itakuwa imefungiwa na TCRA mkuu
Leo muda uliopita nimeweka Windows 8.1 tatizo haipo activated nimecheki baadhi ya mitandao naona link zao sio salama samahani kwa usumbufu unaweza kunipa link ambayo ni salama nika activate windows yangu natanguliza shukrani zangu kwako maana umenisaidia sana
 
Mdogo wangu amekuja na ASUS A68 Padfone toka japan.

Cha ajabu hata haiwaki, Nimemuona anahangaika nayo week nzima.

Unaweza msaidiaje?
 
Mdogo wangu amekuja na ASUS A68 Padfone toka japan.

Cha ajabu hata haiwaki, Nimemuona anahangaika nayo week nzima.

Unaweza msaidiaje?
ni simu au lile jumba lake tu la juu? akieka charger ina chaji?
 
Haichaji na haifanyi chochote.

Inawaka inaonesha maneno halafu inazima.

Shida inaweza kuwa nini?
kama inawaka na kuonyesha maneno na kuzima means ni nzima,

unajua kufanya factory reset ya kutumia button za sauti na volume key?

jaribu ku wipe data na cache inaweza kurudi hali ya kawaida.

ikikataa itabidi tu uflash.
 
Top 5 camera 2017
1.Pixel 2
2.LG V30
3.iPhone 8
4.Note 8/S8
5.OnePlus 5 Bwana mtaalamu unasemaje?? Chief-Mkwawa mk(unaweza nitajia zako )
 
Top 5 camera 2017
1.Pixel 2
2.LG V30
3.iPhone 8
4.Note 8/S8
5.OnePlus 5 Bwana mtaalamu unasemaje?? Chief-Mkwawa mk(unaweza nitajia zako )
mkuu ni ngumu kutaja, ila kwangu mimi Nokia za zamani kama 808, lumia 1020 na 950xl still zina camera nzuri kuliko simu za sasa.

steve wa AAWP anafanya comparison kila simu mpya na hizo za zamani na matokeo kila siku ni yale yale.

mfano hii ya pixel 2 na 950xl kuna situation pixel inakuwa nzuri na situation 950xl ni nzuri angalia hapa

Low light camera head to head: Lumia 950 vs Google Pixel 2

ila tukienda mbele tukirudi nyuma, google anajitahidi sana hasa kwenye software HDR+ yao ni nzuri, hata ukieka kwenye simu nyengine ambazo sio pixel picha zinatoka vizuri sana.
 
IMG-20171110-WA0014[1].jpg
Wakati mwingine simu kutoka Marekani haswa za mitandao ya Verizon, T-Mobile, Sprint na AT&T huwa zinalimit baadhi ya features kama Wifi Hotspot na kwa bahati mbaya zaidi baadhi ya simu kutoka kwenye mitandao hii hazina support ya community ya custom ROM's na wakati mwingine ukipata ROM inakua na shida ya Bluetooth na Wifi mfano HTC One M7 ya Sprint(m7sprt).
Kwa wale watakaopenda simu kutoka kwenye kampuni za kichina au Korea wawe wanajaribu kupitia forums mbalimbali kama XDA kuangalia upatikanaji wa ROM, radio, custom kernel, RUU, na hizo mods nyinginezo.

Hivi simu ikiandikwa hivi UNLOCKED AT&T inakua hivo hivo haziangalii mpesa wala tigo pesa?

nisije nikaingizwa chaka mapema




IMG-20171110-WA0014[1].jpg
Cc: [HASHTAG]#chief mkwawa[/HASHTAG]
 
Hivi simu ikiandikwa hivi UNLOCKED AT&T inakua hivo hivo haziangalii mpesa wala tigo pesa?

nisije nikaingizwa chaka mapema

Cc: [HASHTAG]#chief mkwawa[/HASHTAG]
most of time za AT&T zinakubali hio miamala sababu mtandao huo unafanana na wakwetu, mitandao ya china na korea na kwa marekani mitandao kama verizon na sprint inaweza ikazingua.

kama unanunua online muulize muuzaji kama inakubali ussd, kama ni mtaani itest kwanza.
 
View attachment 636245

Hivi simu ikiandikwa hivi UNLOCKED AT&T inakua hivo hivo haziangalii mpesa wala tigo pesa?

nisije nikaingizwa chaka mapema




View attachment 636245
Cc: [HASHTAG]#chief mkwawa[/HASHTAG]

Nimefanikiwa kununua hii simu ni nzuri ila changamoto zake

1. inakupa options zote za tigo pesa kasoro za sim banking(kutuma pesa kwenda bank haiwezi)
2. inaandika 4g mda woote japo iko speed sana kwa kweli


[HASHTAG]#chief[/HASHTAG] mkwawa
 
most of time za AT&T zinakubali hio miamala sababu mtandao huo unafanana na wakwetu, mitandao ya china na korea na kwa marekani mitandao kama verizon na sprint inaweza ikazingua.

kama unanunua online muulize muuzaji kama inakubali ussd, kama ni mtaani itest kwanza.

Nimefanikiwa kununua hii simu ni nzuri ila changamoto zake

1. inakupa options zote za tigo pesa kasoro za sim banking(kutuma pesa kwenda bank haiwezi)
2. inaandika 4g mda woote japo iko speed sana kwa kweli
 
Back
Top Bottom