Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Leo inasomwa Albadir takribani mikoa kama 7 hivi inavyosemekana kwa watu wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu huko Dodoma.

Sasa nakuomba Mahaba Jr utufafanulie kuhusu Albadir na matokeo yako.

Hongera kwa wote wanaoisoma matokeo yanasubiriwa.
Mahaba Jr tena. Na isomwe tu, dhulma inataka kugeuka mtindo wa maisha.
 
Wadau naona watu wengi wamezungumza sana kuhusu kisomo cha Albadir ambacho baadhi ya waislamu wanatarajia kukisoma kesho kwa ajili ya kuwashtakia kwa Allah watu waliokusudia kumuua Mh, Tundu Lisu.

Kisomo hicho ambacho maana yake kwa Kiarabu kinaitwa Ahlul Badr, uwa kinasomwa kwa kuwataja maswaaba ambao walishiriki kupigana katika vita vya Badr,

Dua hiyo huwa ina majibu ya haraka sana kama inasomwa kwa ikhlas, na ni kwamba Allah uwa anaijibu punde tu kama jambo linalokusudiwa lipo kwenye haki, na kuna dhulma imefanyika,

Mtume Muhammad (Saw) anasema dua ya mwenye kudhulumiwa huwa haina pazia baina ya dua hiyo na Allah, tutarajie majibu ya haraka sana kama kweli dua hiyo itafanyika.

Madhara ya dua hiyo ni kwamba watu waliohusika, waliochangia mawazo, kifaa kilichotumika wote watapata madhara, na ndio maana dua hiyo waislam uwa tunashauriwa tutumie Busara kuisoma maana inaondokaga na wengi.

Assallaam Alleykum Warahmatullah Wabarakatuh.
Mkuu, salama na amani yaAllah iwe juu yako na wengine wote humu jamvini, mkuu kisomo cha ahlul badri ni kitu ambacho hakijathibiti kamwe katika dini ya uislam, ni moja ya mambo ambayo hufanywa na wachawi na washirikina wakijificha katika mwamvuli wa uislam, ni upotovu wa dhahiri na ni shirk kubwa katika uislam kuwaomba au kumwomba yeyote asiyekuwa Allah.
Mkuu nakusihi kwa jina la Allah kama jambo hulijui katika uislam wako basi kwanza litafutie elimu, ni kosa kubwa kuongea jambo usilo na elimu nalo.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kusoma Halal Badiri au Albadiri (Ahlul-Badr) Kwa Ajili Ya Kinga Na Kuapiza Ni Shirki Na Dhambi Kuu!


Albadir imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili. Wapo wanaosema Alibadirilakini makusudio ni Ahlul-Badr, yenye maana watu wa Badr (wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyo karibu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili. Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi yao ndogo hiyo waliweza kuwashinda washirikina waliokuwa na idadi kubwa ipatayo mara sita yao.



Kisomo cha Ahlul Badri inakuwa ni kutaja majina ya Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) mmoja baada ya mwingine. Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine. Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya. Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameikema na kuipiga vita sana. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (4: 48). Shirki ni dhuluma kubwa sana.
Jazaakillahu khayra, ningekupa like lakini mwisho ni 5 tu, na tayari ushazipata.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Yaaan sijui niseme nn . Mbona Waislam wa Burma wanaonewa hamuwaombei dua. Nyinyi mnaosoma Albadir Mungu anakuoneni.

Kuna waislam kibao wanauliwa ovyo wanakufa kwa njaa mbona hamukai mkaanza kuwaombea dua.

Acheni Unafiki na Dini yenu.

Neno langu la mwisho Sadaka Huwanza nyumbani. Sio kwa jirani
 
Aliyekuwa mkuu wa mkoa wa DSM Yusuf Makamba alisomewa albadir katika msikiti wa Mwembechai mwaka 2000, mpaka leo anadunda. Labda Makamba hakuwa na kosa. Ngoja tuone kuhusu hawa watu wasiojulikana, au pengine yatakayowapata hatutayajua kwa sababu watuhumiwa wenyewe hawajulikani!
 
Kama utahitajika mchango tafadhali piteni kwangu ntawapa maana hakuna namna sasa tumechoka warogwe tu wao si hawajulikani ngoja watafutwe kwa njia za kitaalam
 
sio ifike kesho waanze kusema wanamuachia mungu aamua, au wanaepusha madhara kwa watu wasiojulikana ... Hiyo itakuwa sababu tosha ya kusema wasomaji walisema tu iki kutafuta kick au kutoa vitisho..
Hiyo kesho dude liamshwe tu, wasome hiyo kitu, kama ni mtu kudhurika na adhurike tu hatutaki visingizio.
Hiyo Albadir Mwenyezimungu aipe Makbul na waliohusika watatarishwe kama vile vitu vinavyotatarika wakati dua hiyo ikisomwa inshaallah!!!!!
 
Sijui nn sasa we ndo ujui Mungu wetu ni mmoja na alisema Samehe saba mara sabini,.. Nyie na matakbir yenu mnaleta shida dunia nzima sio kila jambo unatakiwa ulipize kwa damu, vingine vya kukaa mezani yanaisha,mnajiita chinja chinja
Kumjua adui yako ni hatua mojawapo ya ushindi, nakushauri yatafiti usemayo je kweli uislam unayafundisha na kuyakubali unayowatuhumu nayo waislam.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom