Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Wewe ndio kajifunze.
Dua ni ibada. Tena kubwa sana.

Ibada yeyote ni lazima iwe ina asili kwenye Qur-aan au Sunnah. Hiyo yenu mmeipata wapi?

Nadhani hujui hata inavyosoma na nini kinatumika kwenye kisomo hicho. Usingeandika haya.

Ule ni uchawi. Na uchawi kwenye uislamu ni shirki.

Wanaweza kuwa wanamlilia mungu. Lakini si Mungu muumba
Duh wewe utanifanya nimkufuru mola wangu wewe, nadhan nikuache tu na upoyoyo wako
 
Waangalie isije ikaondoka na Lissu...... Kila la Kheri yakhee.....
nataka yule jamaa imkamate fasta ninavyomchukia yelewii hehe nitafanya sherehe na nitakunywa bia wiki nzima mfululizo na kukaa uchi wa mnyama kibarazani kwetu uswazi
 
kama bwai bwai tu, kama walizani risani ni biscuit ngoja na wao waonje madhara, sjui watachangiwa na nani na watahifadhiwa hospital gani! mshahara wa dhambi ni mauti, wasiojulikana watajulikana..
 
Hapa kuna upotoshaji kidogo na nimeona ni vema tukawekana sawa.Ifahamike kwamba hiki kinachoitwa albadar ni uchawi na hata waislam wanaoelewa hili huita albadar ni shirki yaani ushirikina.
Albadir asili yake ni nini?

Jina albadili kwa kiswahili kwakiarabu ni badrii maana yake ni jini wa vita na hapa ndipo chanzo cha ushirikina wenyewe.Upo mkanganyiko mkubwa sana kwenye dua nyingi zinazoitwa zakumshitakia allah kwani msingi wake mkubwa ni majini ambayo ndio hutumika kudhuru watu na yeyote anayesoma albadili 100% ni mganga wakienyeji.
Nakaribisha maswali
Hakuna maswali juu yako mkuu, atakaye ayajibu tu haya matatu, ni nani anayeombwa dua baya dhidi ya wanadamu hata wawe ni wahalifu? Je ni Mungu, Maswahiba wanaotajwa ama kuna viumbe vingine vilivyoumbwa kwa madhumuni hayo ya kupokea na kutimiza dua baya dhidi ya viumbe vingine?

Hapa tuwe makini kidogo, vipi kama hakutakuwa na baya litakalo tukia, upande huo hauta prove wrong kwamba imani hiyo siyo sahihi na kuushusha? Huu ni mtego kwa anayejitegea, nakumbuka alishasomea na Mzee Yule wa Msoga pia, ikamuongezea baraka za kupendwa zaidi.

Siwaungi mkono wauaji na watesaji, ila hii njia ilaleta ukakasi ktk dunia ya leo.
 
UISLAMU HAUNA KITU KINACHOITWA ALBADIRI

Ninapenda kutoa elimu kiasi ninachoelewa kwa wale wote waliopanga kusoma wanachoita Albadir kwamba hakuna kitu kama hicho katika mafundisho ya Uislamu hata kama ni jambo linalotajwa na wengi na limekuwepo kwa muda mrefu na watu kuliamini.

Kwanza kimsingi ilipaswa itamkwe AHLUL BADR yaani maswahaba walioshiriki vita vya badir.

Kwa mujibu wa masheikh waongofu wa 'Ahlul sunna waljamaa' kisomo kinachoitwa Albadir au Alalbadiri kama wengine wanavyotamka hakina asili katika dini tukufu ya Kislamu hivyo ni ibada au kisomo cha kuzua.

Tukisema cha kuzua tunamaanisha hakufundisha kitu hicho Mtume wa Allah.Kila ibada au kisomo katika Uislamu lazima ifanywe/kifanywe kwa masharti mawili:Mosi kwa ajili ya kutaka radhi za Allah na pili kifanywe kama alivyofundisha Mtume (SAW).Hayo mawili yakikosekana hicho kitu ni takataka (uzushi/bidaa)

Ibada zote sahihi zina dalili (ushahidi) ktk sunna (mienendo ya Mtume) na/au Quran.

Inasemekana katika kisomo hicho wanataja majina ya maswahaba walioshiriki vita vya Badr huku wakifanya ushirikina wa madude ya ajabu ajabu kama malimao na sindano.

Hakuna kitu kama hicho katika Uislamu SAHIHI. Hakuna dua ya kuomba kupitia kwa watu. ANAYEOMBWA NI ALLAH MOJA KWA MOJA.

Kama ndivyo, kisomo cha aina hiyo bila shaka wanaotajwa ni mashetani na si vinginevyo na hivyo kinachofanyika ni ushirikina ambao kwa bahati mbaya sana unanasibishwa na Uislamu kimakosa sana.

Kama kuna watu wanataka kumshitakia Mungu ziko dua za kawaida za kisheria na haziitwi albadir na hazina masula ya kuapizana.

Ni vyema niungane na wengine waliojitokeza katika mitandao kuufahamisha umma ujue kwamba hakuna kisomo wala ibada katika uislamu SAHIHI inayoitwa Albadir.

Ni mambo ya hovyo kabisa yanayonasibishwa na Uislamu wakati hayana asili na dini hiyo tukufu.

_Mwandishi wa waraka huu ni Msomi wa Elimu dunia kwa ngazi ya Shahada ya Chuo Kikuu na ni Mbobezi kwenye Elimu Ahera._

_Pia ni Mwandishi wa Habari Mkongwe na amewahi kuwa Mhariri wa magazeti mbalimbali yakiwemo Sunset,The Guardian, Nipashe,Alasiri,Habari Leo n.k._

Nime-copy toka kwa khamis kibari
 
Sijui nn sasa we ndo ujui Mungu wetu ni mmoja na alisema Samehe saba mara sabini,.. Nyie na matakbir yenu mnaleta shida dunia nzima sio kila jambo unatakiwa ulipize kwa damu, vingine vya kukaa mezani yanaisha,mnajiita chinja chinja
Acha upumbavu wewe!!Mpaka angefumuliwa baba au mama yako ndio ungehisi ni sawa!!Tena kama Mashehe kuna namba za kuchngia mziweke officially NITACHANGIA!
 
nataka yule jamaa imkamate fasta ninavyomchukia yelewii hehe nitafanya sherehe na nitakunywa bia wiki nzima mfululizo na kukaa uchi wa mnyama kibarazani kwetu uswazi
Hapo kwenye uchi wa mnyama hapo ndo umekera wengi, unataka kumuonyesha nani ako kabamia kako wewe poyoyo??
 
Leo inasomwa Albadir takribani mikoa kama 7 hivi inavyosemekana kwa watu wasiojulikana waliomshambulia Tundu Lissu huko Dodoma.

Sasa nakuomba Mahaba Jr utufafanulie kuhusu Albadir na matokeo yako.

Hongera kwa wote wanaoisoma matokeo yanasubiriwa.
 
UISLAMU HAUNA KITU KINACHOITWA ALBADIRI

Ninapenda kutoa elimu kiasi ninachoelewa kwa wale wote waliopanga kusoma wanachoita Albadir kwamba hakuna kitu kama hicho katika mafundisho ya Uislamu hata kama ni jambo linalotajwa na wengi na limekuwepo kwa muda mrefu na watu kuliamini.

Kwanza kimsingi ilipaswa itamkwe AHLUL BADR yaani maswahaba walioshiriki vita vya badir.

Kwa mujibu wa masheikh waongofu wa 'Ahlul sunna waljamaa' kisomo kinachoitwa Albadir au Alalbadiri kama wengine wanavyotamka hakina asili katika dini tukufu ya Kislamu hivyo ni ibada au kisomo cha kuzua.

Tukisema cha kuzua tunamaanisha hakufundisha kitu hicho Mtume wa Allah.Kila ibada au kisomo katika Uislamu lazima ifanywe/kifanywe kwa masharti mawili:Mosi kwa ajili ya kutaka radhi za Allah na pili kifanywe kama alivyofundisha Mtume (SAW).Hayo mawili yakikosekana hicho kitu ni takataka (uzushi/bidaa)

Ibada zote sahihi zina dalili (ushahidi) ktk sunna (mienendo ya Mtume) na/au Quran.

Inasemekana katika kisomo hicho wanataja majina ya maswahaba walioshiriki vita vya Badr huku wakifanya ushirikina wa madude ya ajabu ajabu kama malimao na sindano.

Hakuna kitu kama hicho katika Uislamu SAHIHI. Hakuna dua ya kuomba kupitia kwa watu. ANAYEOMBWA NI ALLAH MOJA KWA MOJA.

Kama ndivyo, kisomo cha aina hiyo bila shaka wanaotajwa ni mashetani na si vinginevyo na hivyo kinachofanyika ni ushirikina ambao kwa bahati mbaya sana unanasibishwa na Uislamu kimakosa sana.

Kama kuna watu wanataka kumshitakia Mungu ziko dua za kawaida za kisheria na haziitwi albadir na hazina masula ya kuapizana.

Ni vyema niungane na wengine waliojitokeza katika mitandao kuufahamisha umma ujue kwamba hakuna kisomo wala ibada katika uislamu SAHIHI inayoitwa Albadir.

Ni mambo ya hovyo kabisa yanayonasibishwa na Uislamu wakati hayana asili na dini hiyo tukufu.

_Mwandishi wa waraka huu ni Msomi wa Elimu dunia kwa ngazi ya Shahada ya Chuo Kikuu na ni Mbobezi kwenye Elimu Ahera._

_Pia ni Mwandishi wa Habari Mkongwe na amewahi kuwa Mhariri wa magazeti mbalimbali yakiwemo Sunset,The Guardian, Nipashe,Alasiri,Habari Leo n.k._
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom