Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Captain A

Member
Joined
Dec 25, 2016
Posts
67
Reaction score
164
Wadau naona watu wengi wamezungumza sana kuhusu kisomo cha Albadir ambacho baadhi ya waislamu wanatarajia kukisoma kesho kwa ajili ya kuwashtakia kwa Allah watu waliokusudia kumuua Mh, Tundu Lisu.

Kisomo hicho ambacho maana yake kwa Kiarabu kinaitwa Ahlul Badr, uwa kinasomwa kwa kuwataja maswaaba ambao walishiriki kupigana katika vita vya Badr,

Dua hiyo huwa ina majibu ya haraka sana kama inasomwa kwa ikhlas, na ni kwamba Allah uwa anaijibu punde tu kama jambo linalokusudiwa lipo kwenye haki, na kuna dhulma imefanyika,

Mtume Muhammad (Saw) anasema dua ya mwenye kudhulumiwa huwa haina pazia baina ya dua hiyo na Allah, tutarajie majibu ya haraka sana kama kweli dua hiyo itafanyika.

Madhara ya dua hiyo ni kwamba watu waliohusika, waliochangia mawazo, kifaa kilichotumika wote watapata madhara, na ndio maana dua hiyo waislam uwa tunashauriwa tutumie Busara kuisoma maana inaondokaga na wengi.

Assallaam Alleykum Warahmatullah Wabarakatuh.
 
Kusoma Halal Badiri au Albadiri (Ahlul-Badr) Kwa Ajili Ya Kinga Na Kuapiza Ni Shirki Na Dhambi Kuu!

Albadir imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili. Wapo wanaosema Alibadirilakini makusudio ni Ahlul-Badr, yenye maana watu wa Badr (wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyo karibu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili. Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi yao ndogo hiyo waliweza kuwashinda washirikina waliokuwa na idadi kubwa ipatayo mara sita yao.

Kisomo cha Ahlul Badri inakuwa ni kutaja majina ya Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) mmoja baada ya mwingine. Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine. Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya. Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameikema na kuipiga vita sana. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (4: 48). Shirki ni dhuluma kubwa sana.
 
Safi sana natugemea kuona majibu ya haraka kutokana na dua Al badri
 
sio ifike kesho waanze kusema wanamuachia mungu aamua, au wanaepusha madhara kwa watu wasiojulikana ... Hiyo itakuwa sababu tosha ya kusema wasomaji walisema tu iki kutafuta kick au kutoa vitisho..
Hiyo kesho dude liamshwe tu, wasome hiyo kitu, kama ni mtu kudhurika na adhurike tu hatutaki visingizio.
 
Kusoma Halal Badiri au Albadiri (Ahlul-Badr) Kwa Ajili Ya Kinga Na Kuapiza Ni Shirki Na Dhambi Kuu!

Albadir imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili. Wapo wanaosema Alibadirilakini makusudio ni Ahlul-Badr, yenye maana watu wa Badr (wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyo karibu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili. Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi yao ndogo hiyo waliweza kuwashinda washirikina waliokuwa na idadi kubwa ipatayo mara sita yao.

Kisomo cha Ahlul Badri inakuwa ni kutaja majina ya Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) mmoja baada ya mwingine. Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine. Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya. Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameikema na kuipiga vita sana. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (4: 48). Shirki ni dhuluma kubwa sana.

Mkuu kwa maelezo yako ni dhambi kuisoma hiyo Ahlul-badr
 
Embu na waisome....

Maana tunaiskiaga...

Ila sidhani kama mipoliccm itawaacha...!!??
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom