Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Kusoma Halal Badiri au Albadiri (Ahlul-Badr) Kwa Ajili Ya Kinga Na Kuapiza Ni Shirki Na Dhambi Kuu!
Maswali: Bid'ah - Uzushi

SWALI:
Assalama alikum warahmatullah taala wabarakatu.
Napenda kuanza kwa kumshukuru Mola mlezi wa ulimwengu kwa kuwapa nguvu, afya na uwezo ndugu zetu wa alhidaaya kwa kutuelimisha sisi ndugu zenu Waislam katika musuala mengi yanayohusu dini yetu ya haki. Mola awape kheir, baraka na pepo inshaalah. Ameen.

Na suali langu ni kutaka kujua kama kusoma halal badr ni sawa au si sawa katika uislam? Kuwa kama kinga na kuomba Mungu akuhukumie kwa anetaka kukudhuru au kukufania ubaya.

Asanteni....assalam aleykum.

JIBU:
Sifa zote njema Anastahiki Allaah Aliyetukuka Mola wa walimwengu wote, Swalah na salamu zimshukie kipenzi chetu Mtume Muhammad (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) na Swahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.

Shukran zetu za dhati kwa swali lako kuhusuHalali Badiri. Awali twataka kurekebisha ibara hiyo kwani sivyo inavyokusudiwa au inavyotamkwa au kuandikwa. Ibara hiyo imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili.

Wapo wanaosema Alibadirilakini makusudio ni Ahlul-Badr, yenye maanawatu wa Badr (wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyo karibu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili.

Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi yao ndogo hiyo waliweza kuwashinda washirikina waliokuwa na idadi kubwa ipatayo mara sita yao.

Kisomo cha Ahlul Badri inakuwa ni kutaja majina ya Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) mmoja baada ya mwingine. Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine.

Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya. Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameikema na kuipiga vita sana. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (4: 48). Shirki ni dhuluma kubwa sana.

Ingia Katika Kiungo Kifuatacho pia upate maelezo yam as-ala haya:

Wazazi Wangu Wako Kwenye Maasi,Ushirikina Wa Waganga Na Albadiri (Ahlul-Badr)

Ikiwa unataka kinga basi kinga ni nyingi sana tulizopatiwa na Uislamu ni nyingi. Qur-aan yenyewe ni ponyo na kinga ya mambo mengi na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) naye hakutuacha hivi hivi ila ametupatia kinga nyingi katika Surah na Aayah za Qur-aan na du’aa alizotuachia.

Miongoni mwa kinga ni Muislamu kusoma Surah 112, 113 na 114 mara tatu tatu asubuhi, jioni na wakati wa kulala.Hiswnul Muslim ni kijitabu kizuri cha du’aa na adhkaar katika mas-ala haya.

Utakipata kitabu hicho ndani ya Alhidaaya kwenye kiungo hiki:
 
Ni aina fulani ya kujifariji pia.

Al Badr ingekuwa inafanya kazi, waliosaini mikataba mibovu wote wangekuwa washakufa vifo vibaya sana.

Badala yake wanadunda na kututukana malofa kila mwaka.
Mkuu samahani kwani wale jamaa waliokuwa wanasaini mmikataba ya hovyo na wenyewe walishawahi kusomewa Ahlul-badr ikagoma
 
Ni aina fulani ya kujifariji pia.

Al Badr ingekuwa inafanya kazi, waliosaini mikataba mibovu wote wangekuwa washakufa vifo vibaya sana.

Badala yake wanadunda na kututukana malofa kila mwaka.
Mi kiukweli naona huu ni mchezo wa kumwaga sukari baharini..bora kuna muislam kacomment albadiri ni shirki na sio uislam....hili ni dua la kuku tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
i hope it works ili tuwajue wasiojulikana
 
Sasa mbona inaaminika kwamba wanamlilia Mungu hebu tupe historia yake kidogo
Wachawi wanaposoma talasimu zao huwadanganya watu kwa kuanza kusoma baadhi ya aya au sura ndogo ndogo za Qur-aan na kulitajataja jina la Nabii SULAYMAAN na utawasikia daima wanamnasibisha Mtume huyu ('Alayhis Salaam) na kufru zao hizo ili wajinga wanaowafuata wadhani kwamba hayo yamo katika dini.

Uchawi haujaanza zama za Nabii Sulaymaan kama wachawi wanavyozuwa na kumsingizia Nabii Huyu wa Allaah, bali ulikuwepo kabla yake kwa miaka elfu nyingi.


Uchawi ulikuwepo tokea zama za Nabii Saleh ('Alayhis Salaam) aliyekuja kabla ya Nabii Sulaymaan kwa miaka elfu nyingi.


Allaah Anasema:

"Wakasema: (kumuambia Nabii Swaalih); "Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa."

Ash-Shu'araa - 153

 
Mbona bibi faiza kasema albadil ni uchawi hata kweny quran hakuna kitu kama hicho
 
Wasiongee sana isije ikachachukaa...kesho tunapiga kisomo mpaka minyoo kama ilishiriki walahii inakaukaa..
 
Mkuu samahani kwani wale jamaa waliokuwa wanasaini mmikataba ya hovyo na wenyewe walishawahi kusomewa Ahlul-badr ikagoma
Ukweli kwamba watu wanawalalamikia kila siku halafu kumbe kuna solution dogo tu unawasomea wanapatwa na daflao, unaonyesha kwamba hata watu hawaiamini hii Al-Badr,inatumika kama njia ya kuunganisha watu tu,lakini kuiamini kama dua inayoweza kufanya kazi hakupo.

Kama ipo na inafanya kazi, mimi hapa mkana Mungu, dhambi yangu kukana kwamba Mungu yupo na kueneza habari hizo hapa JF.

Naomba mtu anisomee hiyo Al-Badr nife weekend hii, ili wiki ijayo nikikosekana hapa JF,uwe ushahidi mzuri kabisa kwamba Mungu yupo na anajibu Al-Badr.

Unaweza kuthibitisha hii Al-Badr inafanya kazi kwa mimikusomewa nife ili ukweli ujulikane na uongo ujitenge?

Na nikiweza kuja hapa Jumatatu kuendelea kuandika, ijulikane hiyo Al-Badr ni a social psychology myth tu,haina ukweli.

Hapo vipi?
 
Wachawi wanaposoma talasimu zao huwadanganya watu kwa kuanza kusoma baadhi ya aya au sura ndogo ndogo za Qur-aan na kulitajataja jina la Nabii SULAYMAAN na utawasikia daima wanamnasibisha Mtume huyu ('Alayhis Salaam) na kufru zao hizo ili wajinga wanaowafuata wadhani kwamba hayo yamo katika dini.

Uchawi haujaanza zama za Nabii Sulaymaan kama wachawi wanavyozuwa na kumsingizia Nabii Huyu wa Allaah, bali ulikuwepo kabla yake kwa miaka elfu nyingi.


Uchawi ulikuwepo tokea zama za Nabii Saleh ('Alayhis Salaam) aliyekuja kabla ya Nabii Sulaymaan kwa miaka elfu nyingi.


Allaah Anasema:

"Wakasema: (kumuambia Nabii Swaalih); "Hakika wewe ni miongoni mwa waliorogwa."

Ash-Shu'araa - 153

Na wakafuata yale waliyoyasoma mashaytwaan juu ya ufalme wa Sulaymaan; na Sulaymaan hakukufuru lakini mashaytwaan ndio waliokufuru; wanafundisha watu sihiri na yaliyoteremshwa kwa Malaika wawili katika (mji wa) Baabil; Haaruwt na Maaruwt. Nao wawili hawamfundishi yeyote mpaka waseme: “Hakika sisi ni mtihani, basi usikufuru.” Kisha wakajifunza kutoka kwa hao wawili yenye kupelekea kufarikisha kwayo baina ya mtu na mkewe. Na wao hawawezi kamwe kumdhuru yeyote kwayo isipokuwa kwa idhini ya Allaah; na wanajifunza yanayowadhuru na wala hayawanufaishi; na kwa yakini walijua kwamba atakayechuma haya hatopata katika Aakhirah fungu lolote, na ni ubaya ulioje walichojiuzia nafsi zao, lau wangelikuwa wanajua. [Al-Baqarah: 102]
 
Hakuna kitu hapo ni ujinga tu unawasumbua' tunataka tumjue huyo atakaedhurika sio watuambie aliemtwanga lisu kafa bila kumshuhudia
 
Wanaouchafua uislam au wanatekeleza stahiki ya dini, ni
nani kama sio masheh wanasoma izo albadil au kusema takbir, ...nyie wenyew ndo mnafanya halafu mnasema vitu gani,
Sio kila anayetaja Jina la bwana atauona ufalme wa mbinguni..........................
 
Mi kiukweli naona huu ni mchezo wa kumwaga sukari baharini..bora kuna muislam kacomment albadiri ni shirki na sio uislam....hili ni dua la kuku tu

Sent using Jamii Forums mobile app
Dini zote ni shirki.

Ndiyomaana Wakristo wanayaita makanisa yao "usharika wa wapi na wapi".

Kuamini uchawi na kuamini Mungu kote ni kuamini supernaturalpowers ambazo hazithibitishiki.

Sasa utaniambiaje kuamini uchawi ni tofauti na kuamini Mungu ni vitu tofauti wakati vyote ni kuamini vitu visivyothibitishika?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom