Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Sio nzuri sana kuisoma maana madhara yake ni makubwa sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
Ni kweli mkuu si nzuri sana kuisoma,ila dhulma nayo ndio si nzuri zaidi. watu wengi hupanga na kufanya dhulma kisha kujificha katika koti la "watu wasiojulikana",nadhani albadir ndio dawa ya watu wasiojulikana,ni kama ulivyoainisha kwenye bandiko lako kwamba inaposomwa kwa haki huwa inatoa majibu fasta na ndio msingi wa msomaji wa haki kuhimiza aliyedhulumiwa kutangaza kwanza nia yake na kutoa muda ili mhusika asiyejulikana kujitokeza na kuomba msamaha. Hii kitu mimi binafsi naiheshimu na kama ningekuwa mimi ndiye niloshiriki kwa namna yoyote kwa kweli ningejitokeza kwa kuwa madhara yake nayajua tena kwa mfano hai,tatizo tu ni kwamba kwa miaka ya karibuni pamejitokeza masheikh uchwara ambao husoma hii kitu kiutapeli,lakini ukikutana na mtaalam wa kuisoma na kweli kukawa na haki iliyodhulumiwa huwa haikopeshi,na kwenye jambo hili la Lisu ni kweli kuna haki iliyodhulumiwa swali ni je wasomaji watatenda haki?
 
Samehe saba Mara sabini kwa aliyeomba msamaha. Wameambiwa wajitokeze na kutubu wamedharau. Hivyo bila kufanya hiyo dua kesho wayamchapa mwingine shaba na mwingine tena.
Lazima mambo hayo yakomeshwe. Sasa sijuikama mzee anahusika halafu wazimu ukampanda na kuvua nguo kwenye hadhara mbele ya kamera itakuwaje!
A wapi uyo sheh wako ndo wakwanza kudata,
 
Uislamu hauruhusu kufanya uchawi au ushirikina.Bahati nzuri wapo waganga waislamu ambao ni washirikina na waganga wachamungu.Chagua wewe unamtaka yupi
 
Unajua maana ya shirki???Abdul-Badr so shirki maana nikumlilia Mungu ndo atoe hukmu .sasa hapo shirki ikowapi??shirki nikumshirikisha mungu navitungine.
Kumshirikisha Mungu Kwa jambo lolote la kidunia ni shirki .yeye Allah anajua wakumpa haki na kumnyima hapangiwi .soma vitabu achana na maneno ya vijiwen.
 
Wadau naona watu wengi wamezungumza sana kuhusu kisomo cha Albadir ambacho baadhi ya waislamu wanatarajia kukisoma kesho kwa ajili ya kuwashtakia kwa Allah watu waliokusudia kumuua Mh, Tundu Lisu.

Kisomo hicho ambacho maana yake kwa Kiarabu kinaitwa Ahlul Badr, uwa kinasomwa kwa kuwataja maswaaba ambao walishiriki kupigana katika vita vya Badr,

Dua hiyo huwa ina majibu ya haraka sana kama inasomwa kwa ikhlas, na ni kwamba Allah uwa anaijibu punde tu kama jambo linalokusudiwa lipo kwenye haki, na kuna dhulma imefanyika,

Mtume Muhammad (Saw) anasema dua ya mwenye kudhulumiwa huwa haina pazia baina ya dua hiyo na Allah, tutarajie majibu ya haraka sana kama kweli dua hiyo itafanyika.

Madhara ya dua hiyo ni kwamba watu waliohusika, waliochangia mawazo, kifaa kilichotumika wote watapata madhara, na ndio maana dua hiyo waislam uwa tunashauriwa tutumie Busara kuisoma maana inaondokaga na wengi.

Assallaam Alleykum Warahmatullah Wabarakatuh.
Naomba isomwe na wote waliohusika wavae vyupi kichwani [emoji57] [emoji57]
 
Hivi hayo mambo yapo kweli nahisi kama stori za kudadikika, nakumbuka zamani tulikuwa tunaambiwa tukichana korahani tu karatasi tu unakuwa chizi.
Lakini kama hayo mambo yanawezekana kwa nini wasiwasomee albadrili vikundi vya kigaidi na mbaya zaidi hivyo vikundi vinavyosumbua vipo kwenye nchi za kiislamu??
 
Hapa kuna upotoshaji kidogo na nimeona ni vema tukawekana sawa.Ifahamike kwamba hiki kinachoitwa albadar ni uchawi na hata waislam wanaoelewa hili huita albadar ni shirki yaani ushirikina.
Albadir asili yake ni nini?

Jina albadili kwa kiswahili kwakiarabu ni badrii maana yake ni jini wa vita na hapa ndipo chanzo cha ushirikina wenyewe.Upo mkanganyiko mkubwa sana kwenye dua nyingi zinazoitwa zakumshitakia allah kwani msingi wake mkubwa ni majini ambayo ndio hutumika kudhuru watu na yeyote anayesoma albadili 100% ni mganga wakienyeji.
Nakaribisha maswali
 
Wadau naona watu wengi wamezungumza sana kuhusu kisomo cha Albadir ambacho baadhi ya waislamu wanatarajia kukisoma kesho kwa ajili ya kuwashtakia kwa Allah watu waliokusudia kumuua Mh, Tundu Lisu.

Kisomo hicho ambacho maana yake kwa Kiarabu kinaitwa Ahlul Badr, uwa kinasomwa kwa kuwataja maswaaba ambao walishiriki kupigana katika vita vya Badr,

Dua hiyo huwa ina majibu ya haraka sana kama inasomwa kwa ikhlas, na ni kwamba Allah uwa anaijibu punde tu kama jambo linalokusudiwa lipo kwenye haki, na kuna dhulma imefanyika,

Mtume Muhammad (Saw) anasema dua ya mwenye kudhulumiwa huwa haina pazia baina ya dua hiyo na Allah, tutarajie majibu ya haraka sana kama kweli dua hiyo itafanyika.

Madhara ya dua hiyo ni kwamba watu waliohusika, waliochangia mawazo, kifaa kilichotumika wote watapata madhara, na ndio maana dua hiyo waislam uwa tunashauriwa tutumie Busara kuisoma maana inaondokaga na wengi.

Assallaam Alleykum Warahmatullah Wabarakatuh.
Siku Mh.Lisuu amepata tukio la kupigwa risasi,sikula chochote na nilitoa machozi na kupata mfadhaiko wa akili. Niliwaza sana kwa kijana kama yule kumiminiwa risasi bila huruma. Nilijiuliza,na najiuliza hadi leo sijapata jibu! Ninaamini,hata hili jambo lisipofanyika,na kwa unyama ule, Mungu atawajibu kwa njia nyingine yoyote ile. Very,very sad. Fikiria ni wewe,umemzaa kijana,umemlea na kumsomesha kwa mahangaiko,amekua ,amepata elimu,sasa unamtegemea na anatokeza mtu tuu baki anamfanyia tukio kama lile,hii haingii akilini .
 
Utakoma hiyo swala hata wateteaji kama wewe haiwaachi salama mnaua kwa kukataa kupingwa tu. Au kupewa ushauri anza kujiandaa kuwa chizi.

[emoji23][emoji23][emoji23] Kweli kabisa aanze kujiandaa kisaikolojia kuwa Mkichaa! Mbona wale wanaokwapua Mali Za umma kiasi Kwamba kusababisha kukosekana Kwa madawa na vifaa Tiba Kwenye hospitali hali inayopelekea Watu wengi kupoteza maisha wanaachwa na kudunda mtaani? Mnataka kuumua Mtu ambaye anajaribu kuwatetea wanyonge[emoji87][emoji87][emoji87] kawakosea nini cha mno?! Eeeh Mwenyezi Mungu twakusihi kwaajili ya Rehema zako zidi kumponya Mwanao Tundu A.Lissu, twakusihi uzidi kumuondolea maumivu yote mwilini mwake Kwa haraka mfanyie wepesi wa uponyaji hadi madaktari na manesi washangae ktk Jina la Yesu Kristo Mpatanishi na Mwombezi wetu aliye Hai! Amin!
 
Itafika kipindi tuatkuwa htuna character za Kibinadmu, kwani jini ni nani asitutumikie?
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom