Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Mbona una hofu mkuu? Uko miongoni mwa watu wasiojulikana nini? Albadir haina mchezo, inatembea haswa na inatafuta, kila aliyehusika inamchukua.

Iliwahi kusomwa Tanga miaka ya nyuma na sharifu ilikuwa balaa, watu walitafutana.

Ni baada ya mwenye shamba la minazi kuingia shambani kwake na kukuta makumbi tu ya nazi, wezi walisafisha shamba zima.

Akatangaza kwa siku tatu, aliyehusika ajitokeze mwenyewe, watu wakakaa kimya, baada ya siku tatu kupita, sharifu akaenda kuisoma, ilikuwa ni kutafutana haswa kupita kiasi.

Punda aliyebeba nazi alikufa, chuma kilichofulia nazi kilimong'onyeka, wezi wote walikufa, kila aliyekula zile nazi alikufa, iliacha gumzo kubwa Tanga miaka na miaka, yoyote aliyeshiriki katika hizo nazi alikufa.
Huoni huu niujinga mkuu? Yaani umemtuma mtoto nazi ameleta umekula ufe kwani wewe ndo mwizi
 
Huoni huu niujinga mkuu? Yaani umemtuma mtoto nazi ameleta umekula ufe kwani wewe ndo mwizi
Ni sasa hivi tu kwa kuwa madhambi yamezidi... lakini albadir huwa haina masihara.... Mpaka kesho Tanga wapo mbuzi wa albadir.... Hawana mwenyewe hao mbuzi... Wanazunguka tu mitaani... Mkamate umle ndio utaiona shughuli yake.
 
I hope it could be true. Let the wrong doers perish and suffer 10 times the suffering of TL
 
Kusoma Halal Badiri au Albadiri (Ahlul-Badr) Kwa Ajili Ya Kinga Na Kuapiza Ni Shirki Na Dhambi Kuu!


Albadir imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili. Wapo wanaosema Alibadirilakini makusudio ni Ahlul-Badr, yenye maana watu wa Badr (wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyo karibu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili. Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi yao ndogo hiyo waliweza kuwashinda washirikina waliokuwa na idadi kubwa ipatayo mara sita yao.



Kisomo cha Ahlul Badri inakuwa ni kutaja majina ya Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) mmoja baada ya mwingine. Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine. Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya. Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameikema na kuipiga vita sana. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (4: 48). Shirki ni dhuluma kubwa sana.
Ufafanuzi mzuri kabisa, Allah akubariki sana
 
bfec2b12b16aadeb03ae16e94a897a00.jpg
d2237a16b981f54ea0d3468b47e54001.jpg
 
Kwa hio vile mlovyofanya amerika ni halali enzi zile za utumwa ❔ je LRA inavuofanya Uganda hadi Afrique ya kati ni haki ❔
Tukirudi kwenye hio Halbadir / Alalbadir ; Huo ni ushirikina ambao haufai kufanywa kwa maana anaeshiri anakuwa ni mshirikina nae
 
Kwa jinsi watanzania wanavyo lia miyoyoni mwao juu ya uonevu,,hakika kuweka NIA tu ya kuisoma hii ahul badri inatosha kumsambaratisha mtu.
 
Ni nini Alalbadri??

Ni dua ya kutaka msaada wa majini kwa kufanya ushirikina wa kumuomba mungu kupitia maswahaba waliopigana vita ya badri.

Katika dua hii:-
1- hutajwa majina ya waliopigana vita vya badri.
2-Wengine huongezea nafaka mbalimbali zenye kupendwa na majini watakao fanyia kazi maombi hayo.

3-Wengine huchinja.ili kumshawishi shetani zaidi.

4-baada ya hapo vitu hivyo:-
Nyama hutolewa sadaka.
Chungu,nafaka,ndimu na sindano na kichwa cha mnyama vilivyotumika kwa ushirikina huo wengine huvitupa njia panda,makaburini na kuvifukia ardhini kuendana na malengo.

*EWE MUISLAMU JIEPUSHE NA USHIRIKINA HUU.KWA HAKIKA KUMSHIRIKISHA ALLAH NI UKAFIRI NA UKIFA KATIKA HALI HIYO UTAINGIA MOTONI MILELE NA HUTOPATA WALAU MWANYA WAKUTOKA HUMO.*
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom