Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Jifunze hapa kuhusu ALBADIR

Ukweli kwamba watu wanawalalamikia kila siku halafu kumbe kuna solution dogo tu unawasomea wanapatwa na daflao, unaonyesha kwamba hata watu hawaiamini hii Al-Badr,inatumika kama njia ya kuunganisha watu tu,lakini kuiamini kama dua inayoweza kufanya kazi hakupo.

Kama ipo na inafanya kazi, mimi hapa mkana Mungu, dhambi yangu kukana kwamba Mungu yupo na kueneza habari hizo hapa JF.

Naomba mtu anisomee hiyo Al-Badr nife weekend hii, ili wiki ijayo nikikosekana hapa JF,uwe ushahidi mzuri kabisa kwamba Mungu yupo na anajibu Al-Badr.

Unaweza kuthibitisha hii Al-Badr inafanya kazi kwa mimikusomewa nife ili ukweli ujulikane na uongo ujitenge?

Na nikiweza kuja hapa Jumatatu kuendelea kuandika, ijulikane hiyo Al-Badr ni a social psychology myth tu,haina ukweli.

Hapo vipi?
ikitokea juma 3 ukaonekana umepost humu watasema Mungu anajibu kwa wakati wake, tumpe muda...siku utakayopotea kabisa humu watasema ule muda ndio umefikia Mungu amejibu..
 
Ni aina fulani ya kujifariji pia.

Al Badr ingekuwa inafanya kazi, waliosaini mikataba mibovu wote wangekuwa washakufa vifo vibaya sana.

Badala yake wanadunda na kututukana malofa kila mwaka.
Labda wana kinga ya kuzuia kuwadhuru na albadili
 
Tofautisha Kati ya shirki na dini hata km huamini
Dini zote ni shirki.

Ndiyomaana Wakristo wanayaita makanisa yao "usharika wa wapi na wapi".

Kuamini uchawi na kuamini Mungu kote ni kuamini supernaturalpowers ambazo hazithibitishiki.

Sasa utaniambiaje kuamini uchawi ni tofauti na kuamini Mungu ni vitu tofauti wakati vyote ni kuamini vitu visivyothibitishika?
“Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na Shaytwaan na kwa msaada wake (Shaytwaan)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.”

Ama Swahaba Ibni 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:

"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki."

Hayo ni katika kamusi za lugha.

Amma katika kamusi ya dini, maana ya neno Uchawi (As Sihr), kama alivyofasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhruddin Al Razi kuwa;

"Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa (khidaa)."

Amma Shaykh Wahiyd Abdulsalaam Bali, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho 'Al Saarim Al Batar fiy muhaarabat Al Saharatul ashraar', na kitabu kiitwacho "Al wiqaya mina l jinni wa shaytan", ambaye pia ni mtaalamu maarufu katika elimu ya majini na Mashaytwaan na uchawi na ambaye pia ni katika maulamaa maarufu wanaotoa majini kwa njia ya kusoma Qur-aan, yeye anasema:

"Uchawi ni makubaliano baina ya mchawi na Jinni akishurutishwa mchawi kufanya mambo ya haramu au ya shirki, na baada ya kufanya hayo, Jinni anashurutishwa kumsaidia na kumtii mchawi huyo kwa kila anachotaka."

Baadhi ya yale ambayo mchawi anatakiwa na Shaytwaan ayatende ili ajikurubishe naye ni:

 Mchawi anatakiwa auvae msahafu miguuni na aingie nao chooni

 Aandike baadhi ya aya za Qur-aan kwa damu ya hedhi.

 Miongoni mwao wanashurutishwa kuandika aya za Qur-aan penye nyayo za miguu.

 Au aiandike suratulFatiha kinyume nyume.

 Asali bila ya Udhuu.

 Wengine hutakiwa kuchinja mnyama bila ya kulitaja jina la Allaah kisha amtupe mnyama huyo mahali maalum anapoamrishwa na Shaytwaan.

 Wamo miongoni mwao wanaozungumza na nyota au kuzisujudia.

 Au hutakiwa kuandika herizi kwa maneno yenye kufru ndani yake
 
Kusoma Halal Badiri au Albadiri (Ahlul-Badr) Kwa Ajili Ya Kinga Na Kuapiza Ni Shirki Na Dhambi Kuu!

Albadir imetoka katika lugha ya Kiarabu lakini kupotolewa au kuandikwa na kusomwa makosa katika Kiswahili. Wapo wanaosema Alibadirilakini makusudio ni Ahlul-Badr, yenye maana watu wa Badr (wale waliopigana vita vya Badr). Badr ni sehemu iliyo karibu na Madiynah na ndio iliyokuwa sehemu ambayo Waislamu wakiongozwa na Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) walipambana na mushirikina wa Makkah katika vita vya kwanza baina ya pande hizo mbili. Waislamu waliohudhuria walikuwa baina ya 313 – 317, lakini pamoja na idadi yao ndogo hiyo waliweza kuwashinda washirikina waliokuwa na idadi kubwa ipatayo mara sita yao.

Kisomo cha Ahlul Badri inakuwa ni kutaja majina ya Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) mmoja baada ya mwingine. Katika kutaja huko ni Imani ya mwenye kusoma hao Maswahaba (Radhiya Allaahu ‘anhum) wanamsaidia kwa njia moja au nyingine. Ima kupata kitu alichopoteza au kilichoibiwa au kulaaniwa aliyefanya. Na hii katika Uislamu ni njia moja ya shirki ambayo Allaah Aliyetukuka na Mtume Wake (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) wameikema na kuipiga vita sana. Allaah Aliyetukuka Anasema:

“Hakika Allaah Hasamehe kushirikishwa, na husamehe yaliyo duni ya hilo kwa Amtakaye. Na anayemshirikisha Allaah basi hakika amezua dhambi kubwa” (4: 48). Shirki ni dhuluma kubwa sana.
Subirini kesho akiri iwaruke na wengine wajifunze .....utapangaje kumuuwa mtu kisa tu anakupinga????
 
Ilisomwa na mzee fulani Kilwa baada ya kuibiwa nazi zake.
Weeeeeeeeeehhhh.
Mpaka punda aliyetumika kubeba mzigo, shoka lililotumika kufua nazi, walaji na walioiba wote walikwenda.
Au asiyeijua vizuri aende Pale Afrikana Dar aulize nini maana ya Ahlul badr , vijana wa bodaboda wote waliochoma moto daladala ya Mpemba walikufa kama kuku wamepigwa na sotoka.
Huu ni wakati wa Bashite kujisalimisha ili atetee uhai wake na wa mjomba wake.
 
Sijui nn sasa we ndo ujui Mungu wetu ni mmoja na alisema Samehe saba mara sabini,.. Nyie na matakbir yenu mnaleta shida dunia nzima sio kila jambo unatakiwa ulipize kwa damu, vingine vya kukaa mezani yanaisha,mnajiita chinja chinja
Na mtakoma ...,lazima akili ziwarudi safari hii!!!
 
Subirini kesho akiri iwaruke na wengine wajifunze .....utapangaje kumuuwa mtu kisa tu anakupinga????
Acha kuchanganya chai na mabungo,sijamkataza mtu nyie fanyeni kisomo chenu cha kichaw Ila msiseme uislam. Mimi Chadema pure.
 
Ukweli kwamba watu wanawalalamikia kila siku halafu kumbe kuna solution dogo tu unawasomea wanapatwa na daflao, unaonyesha kwamba hata watu hawaiamini hii Al-Badr,inatumika kama njia ya kuunganisha watu tu,lakini kuiamini kama dua inayoweza kufanya kazi hakupo.

Kama ipo na inafanya kazi, mimi hapa mkana Mungu, dhambi yangu kukana kwamba Mungu yupo na kueneza habari hizo hapa JF.

Naomba mtu anisomee hiyo Al-Badr nife weekend hii, ili wiki ijayo nikikosekana hapa JF,uwe ushahidi mzuri kabisa kwamba Mungu yupo na anajibu Al-Badr.

Unaweza kuthibitisha hii Al-Badr inafanya kazi kwa mimikusomewa nife ili ukweli ujulikane na uongo ujitenge?

Na nikiweza kuja hapa Jumatatu kuendelea kuandika, ijulikane hiyo Al-Badr ni a social psychology myth tu,haina ukweli.

Hapo vipi?
Mungu akusamehe
 
Kistor kiduchu.
Kuna kijana mmoja anafanya kazi ya utengezeji Wa chokostiki(chostik) ninavoita cjui wew?

Sasa huyu anaetengeza anawafanyakazi ambao ni wauzaji(wasambazaji) kuna siku alieka hela sehem ili akuchukulie sukar mmoja Wa hawa wauzaji Wa chokostik zile pesa aliziona akachukua 1500MT ni kama 50000sh.

Sasa wauzaji ni wengi Huyu mtengenezaji hakumjua nani alichukua hela ile jion aliwakusanya kuwauliza wote walikataa alilolifanya ni kuwapisha akawatilisha udhu akachkua msahafu akaufunua akasoma aya mbili tu za mwanzo Wa suratul mulk.

Badae wakaondoka kila mmoja kwenda kwao sasa yule aliochukua zile pesa siku ya pili asubuhi mapema alikuja na hakuwahipokuja mapema lkn sikuhii alikuja mapema sasa mkono ulivimba kidgo ukawa unamuuma akasema kuwa pesa nilichukua mimi Ila 50 nimetumia imebakia 1450 kwahiyo akafuatanishwa na muuzaji mwenzke mpaka anakoishi kufuata hela.

Madhara alianza kuyapata ndo akakiri asubuh mapema bada ya kufika kazini. Mpaks hii leo hatujamuonapo hats Sikh moja.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Tofautisha Kati ya shirki na dini hata km huamini

“Neno “Uchawi”, kwa kiarabu “As Sihr”, maana yake ni kitendo cha kujikurubisha na Shaytwaan na kwa msaada wake (Shaytwaan)”, na akasema pia kuwa; “Uchawi ni kulibadilisha jambo mbali na uhakika wake, nako ni kuwadhihirishia watu jambo lisilo la kweli wakaliona kuwa ni la kweli.”

Ama Swahaba Ibni 'Abbaas (Radhiya Allaahu ‘anhu) amesema:

"Uchawi ni kuidhirisha batili katika sura ya haki."

Hayo ni katika kamusi za lugha.

Amma katika kamusi ya dini, maana ya neno Uchawi (As Sihr), kama alivyofasiri Mwanachuoni mkubwa Fakhruddin Al Razi kuwa;

"Ni kila jambo lililofichika sababu zake, linalotokeza kwa sababu zisizo za kawaida na ndani yake mna hadaa (khidaa)."

Amma Shaykh Wahiyd Abdulsalaam Bali, mwandishi wa kitabu maarufu kiitwacho 'Al Saarim Al Batar fiy muhaarabat Al Saharatul ashraar', na kitabu kiitwacho "Al wiqaya mina l jinni wa shaytan", ambaye pia ni mtaalamu maarufu katika elimu ya majini na Mashaytwaan na uchawi na ambaye pia ni katika maulamaa maarufu wanaotoa majini kwa njia ya kusoma Qur-aan, yeye anasema:

"Uchawi ni makubaliano baina ya mchawi na Jinni akishurutishwa mchawi kufanya mambo ya haramu au ya shirki, na baada ya kufanya hayo, Jinni anashurutishwa kumsaidia na kumtii mchawi huyo kwa kila anachotaka."

Baadhi ya yale ambayo mchawi anatakiwa na Shaytwaan ayatende ili ajikurubishe naye ni:

 Mchawi anatakiwa auvae msahafu miguuni na aingie nao chooni

 Aandike baadhi ya aya za Qur-aan kwa damu ya hedhi.

 Miongoni mwao wanashurutishwa kuandika aya za Qur-aan penye nyayo za miguu.

 Au aiandike suratulFatiha kinyume nyume.

 Asali bila ya Udhuu.

 Wengine hutakiwa kuchinja mnyama bila ya kulitaja jina la Allaah kisha amtupe mnyama huyo mahali maalum anapoamrishwa na Shaytwaan.

 Wamo miongoni mwao wanaozungumza na nyota au kuzisujudia.

 Au hutakiwa kuandika herizi kwa maneno yenye kufru ndani yake
Kamauchawi ni kufanya jambo lisilo kweli kuwa kweli, kusemaMungu yupo wakati hayupo ni uchawi.

Ndiyo maana naona huo uchawi na dini vyote uchawi tu.

Kwa sababu vyote vinasema mambo ambayo hayapo kama yapo.
 
Mtoa mada umepotosha vkali juu ya shirk akbar ya ahlul badr na kuipa hadh ya dua ebu jitaid kabla ujapost fanya bahth au ulza kwa wenye kujua knyume na apo utakua unajichmia madhamb buuuureee.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom