Jicho la tatu Arusha na Lema linavyoona

Jicho la tatu Arusha na Lema linavyoona

Kayoka

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2011
Posts
2,366
Reaction score
2,151
Napenda kuwaeleza kwamba, haya yote yanayomkuta Lema ni kutokana na nyie kutumiwa na mafisadi kuweza kukandamiza haki ya mnyonge.
Tazameni sasa damu yetu wana Arusha inaenda kumwagika wakati wote wa kampeni mpaka uchaguzi ujao hapo Arusha.
Mmekubali kutumika ili kuweza kumkomoa lema lakini kumbukeni kwamba nguvu ya umma kamwe haiwezi kuzimwa na nyie. Kitu gani kiliwawasha mpaka mkafanya hivyo?
Anyway MUNGU yupo one day atakuja kudhihirisha ukweli juu ya jambo hili.
 
Habari wana jf.
Ndg zangu kutokana na hali halisi iliyotokea pale Arusha leo juu ya kumvua ubunge mh Lema hiyo inamaanisha kwamba jimbo liko wazi,sasa nami nimeamua kuingia kwenye kinyan'ganyiro hicho kupitia chama changu.Maana maisha ya udaktari yamenishinda,kila kukicha migomo tuuuuuuuuuuu!!!
Sasa jee nikipata nafasi ya kugombea akina mama hapo mbele mtanipa?na akina baba hapo nyuma mtanipa?
 
WALIOMUUA LEMA HAWA HAPA!

wakazi watatu wa Jimbo la Arusha Mjini na wanachama wa CCM Kulia ni Mussa Mkanga,Agnes Mollel na Happy Kivuyo waliofungua kesi ya kupinga matokeo ya uchaguzi katika jimbo hilo kwa Mbunge wa Chadema Godbles Lema,wakiwa katika chumba cha Mkahakama Kuu Kanda ya Arusha leo wakati kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa.




waliomuua Lema.jpg
 
Biashara biashara imewadia katika mji wetu wana wa arusha! tukashone mashati ya magamba na suluwali nyeusi tumeze mihela halafu siku ya majumuisho tunakomaa kwenye Kombati.
This time ndiyo huwe mkakati! si unajua ****** aliondoa mikutano ya kimataifa hapa baada ya kuchagua cdm pesa ikapotea town sasa this time tukae kibiashara zaidi tujiunge na sisiemu kwa wingi tubonse mihela halafu mwisho teh teh teh! Pipoooooooooooooooooooooooooooooooo!
 
lema anatosha kwa maoni yangu, hebu tusaidie kutibu ndg zetu. Kama una ona migomo mibaya we usigome tu naamini utasaidie wengi. Asante kwa kunielewa
 
Niko Arusha, hivi huu ulinzi mkali namna hii ni dalili kwamba walikuwa wamejua matokeo ya hukumu?. Mahakama zetu haziaminiki? Je si kwamba polisi walikuwa wanajua matokeo. Nimhesabu polisi wanafika 200! Ni hatari tupu.
 
CCM ilishasambaratika yenyewe ndani baada tu ya kichapo pale Arumeru Mashariki, na sasa Arusha mjini itakuwa ndiyo mwisho wao. Arumeru walienda na sera ya matusi, sijui Arusha watakuja na kipi tena; maana udini walijaribu Igunga ukafeli, matusi Arumeru yamefeli!!!!!! Arusha ........!! yetu masikio.
 
Namsubiri atakefungua mkutano wa kampeni wa ccm anipe kadi ya uwanachama ha ha ha ha!
 
Nimeongea na mwana CCM mmoja hapa DAR ni mtu mwenye nafasi kubwa kidogo lakini kwasababu ni mtani wangu nimemuuliza je mnategemea kushinda Arusha akanijibu wao Wanaamini hawatashinda ila wanataka CHADEMA watumie mda mrefu kuhangaika na chaguzi ndogo na fedha kidogo walizo nazo zitumike kughalamia kesi na hizo chaguzi ili ifikapo 2015 wawe hoi kifedha waburuzwe tu kama Mizoga.
 
Habari wana jf.
Ndg zangu kutokana na hali halisi iliyotokea pale Arusha leo juu ya kumvua ubunge mh Lema hiyo inamaanisha kwamba jimbo liko wazi,sasa nami nimeamua kuingia kwenye kinyan'ganyiro hicho kupitia chama changu.Maana maisha ya udaktali yamenishinda,kila kukicha migomo tuuuuuuuuuuu!!!
Sasa jee nikipata nafasi ya kugombea akina mama hapo mbele mtanipa?na akina baba hapo nyuma mtanipa?

Ukiondoa herufi e kwenye jina lako unaonekana wewe ni Magamba.

Ili uweze kugombea jifunze kuandika kiswahili fasaha. Sii udaktali ni udaktari.
 
Back
Top Bottom