Tuache siasa za mtandaoni tufanye utafiti wa kina,
na ninafikiri kwa hili ccm wamekwishalijua ndio matokeo ya hukumu.
wala msishangae na kuanza kushambulia (tafakarini kisha chukueni hatua na kushauri nini kifanyike kwa wapenda mageuzi)
SABABU NI HIZI HAPA:
Kwanza matukio ya baada ya uchaguzi mkuu ulioipa CDM ushindi yaliwachukiza watu wengi haswa vurugu.
Vitendo vya Lema kuongoza mapambano watu wengi walimtafsiri kama kijana na mpenda vurugu
hivyo wazee wengi walionyesha ingawa wanakipenda chama na walimchagua lema kwaajili tu ya chama na si lema kama lema.
leo hii uchaguzi ukirudi watu wengi haswa wazee na wakinamama wananafansi kubwa ya kukipigia Ccm kwao ikiwa na maana kuwa wanataka utulivu wakifikiri kuwa baada ya uchaguzi hakutakuwa na utuvuli na hakuta kuwa na mabomuu ya machozi, kitu amabacho walikichoka mara baada ya uchaguzi uliopita
Lema alijikiti zaidi kwenye operesheni ya kikijenga chama kitaifa kitu ambacho ni kizuri pia alikuwa muda mwingi akishughulika na kesi yake, na watu watapima kazi yake kwa kipindi alichokuwa madarakani hadi kutenguliwa kuwa kawafanyia nini watu wa Arusha. Na hapa ikumbukwe ndipo CCM watakapopashikilia kwelikweli kuwa walishindwa kufanya mambo ya maendeleo, ikumbukwe kuwa hata wakati fulani Meya ya rusha aliwahikusema kuwa Lema anapinga kila kitu hata mambo ya maendeleo wakati akiongelea kuhusu ujenzi wa eneo la kaloleni.
Kunahitajika jitihada za dhadhi na kuhakikisha kuwa CDM hawapotezi kura za wazee na akinamama hao
Sio tu kufikiria ushidni na ushabiki kutika kwa makundi ya vijana wa jiji la Arusha lakini CDM inapaswa kutizama kwa kina changamoto kama hizi ili kulizibiti jimbo
Ikizingatiwa pia kuwa wanasema Lema ni kijana mdogo kiasi serekali imekuwa ikimtharau kwa kutomsikiliza.
lakini pia ikumbukwe kuwa jiji la Arusha ni miongoni mwa miji mikubwa Tanzania nafikiri kibiashara na kimtazamo ni baada ya Dar es salaam. Ambapo shughuli nyingi kama za utalii, makao makuu ya EAC na mahakama ya kimataifa ya mauaju ya Rwanda wanaendesha shughuli zao.
Ikumbukwe Baada ya uchaguzi hata baadhi ya mikutano ilihamishiwa dar au kwa chuki au kwa nia ya kuja kujenga hoja sasa kuwa ilibidi kufanya hivyo kwakuwa jiji hili halikuwa salama tena kwani liko chini ya Upinzani.
Ikumbukwe kuwa iliwahi kusemwa hapa na pengine kuwa hata Kiongozi mkuu wa nchi alikuwa anajishauri juu ya kuja Arusha.
Mambo mengi yalifwanywa ili kujenga mazingira mazuri ya ushindi kwa ccm sasa
KAMA CHADEMA WANALITA HILI JIMBO TENA WAFANYAJE:
tunajua kama cha bado wanakubalika Arusha
Wajiulize swali Je mgombea wao bado anakubalika kwa kiasi gani (maana ccm walikwishamchafua vya kutosha)
Wasiangalie ushabiki wa kisiasa tu bali wafanye utafiti wa kina ni jinsi gani watu haswa wazee na akinamama wanamkubali mgombea atakayesimamiswa kunywe marudii ya uchaguzi,
hii ikizingatiwa wanaweza kubadili mgombea na kwakuwa chama kama cham kinakubali basi wanaweza kwa kuwashawishi wapigakura wazee na wakinamama wanaweza kumsimamisha mtu mwenye makamo kidogo ili walau kubalance mambo na kujizolea makura kutoka kada zote.
wawe makini sana wakati wa kampeni haswa kwenye kauli na sera.
LEMA AWE TAYARIU KWA LOLOTE KATIKA KUKIJENGA CHAMA
Mh. Lema anapaswa akubaliane na uamuzi wa chama hii ikiwa ni katika kuhakikisha kunakuwa na umoja na mshikamano kutokana na maamuzi ya chama yatakayokuwa yameongozwa na utafiti wenye utashi. maana mgawanyiko maanake ni maanguko na aibu.
Chama kisikurupuke katika kufanya maamuzi ya kumteua mgombea wa ubunge kwa kuangalia ushabiki na ufuasi wa Lema,
HAYA NI WAZAZO YANGU TU NMAWEZA KUCHUA LILILO JEMA NA KAAMA NIMEONGEA UPUU KWANZA MNISAMEHE NA KULIACHA LILILO LA KIPUUZI.
NIMETOA MAONI YANGU KAMA MWANACHAMA WA CHADEMA MWENYE KADI NAMBA CDM 0487097 NA MPIGA KURA WA ARUSHA