Mwafrika wa Kike
JF-Expert Member
- Jul 5, 2007
- 5,185
- 59
Kulingana na taarifa ya KLHNEWS, serikali na Mukandala wameamua kuwafutia kesi vijana 38 wa chuo kikuu waliokuwa wameshitakiwa eti kwa kusababisha fujo chuoni.
Hii ni baada ya wana JF kusimama kidete na kupinga kitendo cha uongozi wa chuo kuingilia uhuru wa wanafunzi wa kuchagua viongozi wao. Ingawa Afrika inajulikana kwa udikiteta na ukiukwaji wa haki za binadamu. Ninaamini kuwa Mukandala na Maghembe hawatarudi kwenye zama za mawe na kuwakandamiza hawa vijana wasio kuwa na hatia yoyote isipokuwa kudai uhuru wao wa kidemokrasia.
Habari yenyewe hii hapa kwa hisani ya KLHNEWS na mtiifu wetu Mwanakijiji ambaye alipiga simu zaidi ya mia moja kufuatilia hii habari behind the scene na kutoa sikio kuwasikiliza "wavuta bangi hawa" :
Source KLHNEWS:
http://www.klhnews.com/index.php/headlines/mashtaka-dhidi-ya-wanachuo-38-yafutwa.php
Hii ni baada ya wana JF kusimama kidete na kupinga kitendo cha uongozi wa chuo kuingilia uhuru wa wanafunzi wa kuchagua viongozi wao. Ingawa Afrika inajulikana kwa udikiteta na ukiukwaji wa haki za binadamu. Ninaamini kuwa Mukandala na Maghembe hawatarudi kwenye zama za mawe na kuwakandamiza hawa vijana wasio kuwa na hatia yoyote isipokuwa kudai uhuru wao wa kidemokrasia.
Habari yenyewe hii hapa kwa hisani ya KLHNEWS na mtiifu wetu Mwanakijiji ambaye alipiga simu zaidi ya mia moja kufuatilia hii habari behind the scene na kutoa sikio kuwasikiliza "wavuta bangi hawa" :
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Jumanne Maghembe, ameridhia wanafunzi 38 wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam waliofunguliwa mashitaka katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam wakikabiliwa na mashitaka mbalimbali kuondoloewa mashitaka hayo.
Waziri Maghmbe ameridhia uamuzi huo kutokana na maombi yaliyowasilishwa na uongozi wa chuo hicho kuwa masuala hayo yatamalizwa na uongozi huo, wadau mbalimbali na Serikali ya Wanafunzi (DARUSO).
Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa leo jioni (saa za Tanzania) na Makamu Mkuu wa chuo hicho, Profesa Rwekaza Mukandala, ilieleza kuwa masuala yote yaliyotokana na vurugu chuoni hapo yatashughulikiwa chini ya sheria za chuo hicho.
"Tunafurahi kuwafahamisha kwamba Waziri wa Elimu amekubali ombi letu, hivyo tunaliomba Jeshi la Polisi kufuta kesi dhidi ya wanafunzi 38 zilizofunguliwa Aprili 23 mwaka huu, kwani kesi hizo zitashughulikiwa kwa mujibu wa sheria za chuo, nao pia wamekubali," ilieleza sehemu ya taarifa hiyo.
Profesa Mukandala alisema uongozi wa chuo na DARUSO pia inafuatilia kwa karibu kesi ya wanafunzi 14 iliyofunguliwa polisi kutokana na matukio ya Februari 17 na 22, ili kubaini wasio na hatia waweze kurejea madarasani
Aidha, alisema uongozi wa chuo hicho umeliomba Jeshi la Polisi kuharakisha kesi ya kukutwa na dawa za kulevya inayowakabili wanafunzi watano, ili wasiopatikana na hatia nao waweze kurejea darasani mara moja.
"Tutaendelea kufuatilia kwa karibu hali ya usalama chuoni hapa ili kuhakikisha hali ya usalama inarejea kama kawaida," alisema.
Makamu Mkuu huyo wa chuo, aliupongeza uongozi wa DARUSO kwa kusisitiza kuwa mazungumzo ndio mwafaka ya kumaliza mgogoro chuoni hapo. Katika hatua nyingine, Serikali ya wanafunzi chuoni hapo imepinga hatua iliyochuliwa na Waziri wa Elimu na Ufundi kuwafutia udahili wanafunzi 339.
Akizungumza na wandishi wa habari chuoni hapo, Rais wa Serikali ya wanafunzi (DARUSO), Deo Daud, alisema hatua hiyo imetolewa kisiasa, kwani haikufanyiwa utafiti.
Baadala yake wanataka mazungumzo ambayo wanaamini ndio njia muafaka yanafanyika kati ya utawala na Daruso ili wanafunzi wote waliofukuzwa wanarejeshwa chuoni na hatua zozote dhidi yao zinazingatia taratibu na kanuni chuo kuliko kumbilia kuwapeleka Polisi.
Katika Tamko lao Daruso wamesema kwamba hatua iliyochukuliwa na Serikali kuwafutia wanafunzi mikopo na usajili ni ya kibabe isiyozingatia utawala bora kwani miongoni mwao waliofukuzwa chuo bado kesi mahakamani hawajatiwa hatiani hivyo kutoa tamko hilo ni kuingilia uhuru wa Mahakama.
"Lazima Waziri aeleze Umma kuwa ametumia sheria zipi kuweza kufikia maamzi hayo,tatizo tunalolishughulikia hapa ni uvunjivu wa taratibu uliofanywa na wanafunzi lakini DARUSO inaona hatua iliyochukuliwa dhidi ya wanafunzi ndizo zinavunja taratibu na sheria zilipo"alisema Daud
Alitoa mfano kuwa kati ya wanafunzi waliofutiwa udahili wapo wanne wanaodhaniwa kuvuruga madarasa adhabu yake kama wakidhibitika kufanya hivyo ni kusimamishwa masoma si zaidi ya miezi tisa. Alisema kama uchunguzi wa kina ungefanyika bila serikali kukurupuka, ungeweza kubaini kuwa wakati vurugu za juzi zinafanyika hawakuwepo kutokana na kusimamishwa masomo.
Adha, rais huyo wa Daruso alionya serikali kutotumia umasikini wa wanafunzi 415 walioshindwa kujilipia ada kuwakandamiza kuwa ndio waliongoza mgomo huo na kuwaacha walengwa. Kutoka na tamko hilo tamko hilo, wanafunzi hao wametaka hatua zozote kuhusiana na tamko la serikali ziachwe na baadala yake wanafunzi hao kurejeshwa chuoni, ili washitakiwe kulingana na sheria za chuo.
Pia wameomba serikali iruhusu majadiliano kati yake na Daruso, ili kuona namna ya haki za wanafunzi wasio na hatia kati ya wenye hatia zitapatikana. Pia Daruso imelaani kitendo cha askari wa Kutuliza ghasia (FFU) kuwafungia ndani ya mgahawa wa chuo wanafunzi waliokuwa wanakula na kuanza kuwapiga mabomu ya machozi, hivyo kupata nafasi ya kuwashika hata wale wasiohusika.
Juzi, Waziri wa Elimu alitangaza kuwafutia udahili wanafunzi 339 kwa tuhuma za kuhusika kwenye mgomo wa kushinikiza wanafunzi wenzao warejeshwe chuoni akiwemo Waziri Mkuu wa Daruso, Julias Mtatiro.
Tangia kufunguliwa kwa kesi hiyo kampeni ya dhati imekuwa ikifanyika ikiwahusisha Watanzania walio ndani na nje ili kutaka uongozi wa Chuo Hicho Kikubwa kabisa nchini kubadili maamuzi yake na kurejea kwenye meza ya mazungumzo badala ya kutumia vyombo vya dola kujibu hoja za wanafunzi.
KLHN inatarajia kufanya mahojiano na mmoja wa viongozi wa serikali ya wanafunzi wa Chuo hicho mwishoni mwa juma hili.
Source KLHNEWS:
http://www.klhnews.com/index.php/headlines/mashtaka-dhidi-ya-wanachuo-38-yafutwa.php