Nakuunga mkono kamanda.Kuna member alisema kuwa atakuja RA nae atapewa maandishi ya kijani.Sidhani kama kuna umuhimu wa member kuchangia JF na kuonekana au kujulikana.Jamani naomba tusibaguwane kwa pesa humu ndani, ranking ziende kama zilivyo na isiwepo hata hiyo premium. kwani SI KILA atowaye ataka ajulikane kama katowa. Mtu kama katowa, katowa tuu, si kwa kujulikana, na ambae hana asidhalilishwe kwa kupewa karangi au kacheo cha kumfanya ajione inferior. Ranking ziwe za uchangiaji wa posts tuu.
Itafikia kipindi wale watakaotoa kiwango fulani hapa watakuwa na room yao ya kukata ishu.
Kwwa hiyo wachache "nyie" mkishakubaliana ndio inakuwa mtakavyo?Hatuwezi kukubaliana wote...........
SteveD
Mawazo mazuri natumai Invisible and co-moderators watayashughulikia. Labda pia wakati mchakato huu unaendelea ni vyema moderators wakatoa utaratibu wa kuchangia fedha forum hii pamoja na accounting ya michango ya wadau itakuwa inakuwa handled vipi.
kuna thread inajibu hilo swali lako. lakini vyeo vinategemea na count ya posts, mfano ukifikisha 250 kama sijakosea basi unakua JF Senior and Expert Member. U-Premium ni kama una/umechangia ki fezwa..........nadhani inatosha kwa ufupi!!.
Naomba tafwadhali unipatie address ya hiyo thread please
Naomba kupatiwa maelezo japo kidogo, hivi vyeo humu ndani vinapatikana namna gani, maana nimeona kuna title kadhaa kama vile:
Member
Junior Member
Senior Member
JF-Senior Expert Member
Senior & JF Premium Member
Je upatikanaji wake huu ni wa kupigiwa kura za siri, kuchaguliwa au just upendeleo. Maana nilishtuka kuona eti hata X-Paster naye ni JF-Senior Expert...! Mhh nikahisi sasa huku si kuvishana viremba vya kuchorwa? I mean ukoka, maana baada ya muda ukipigwa na jua tu vimenyauka... Wajameni wale wanao itwa monamodireta!!au sijui majinireta, hapana nimekumbuka ni Forum Moderators, wanifahamishe yanakuwaje mambo haya...?!
Naomba kujiwakilisha
Mawazo mazuri Steve D lakini hivi ni kwa nini tunaidharau rangi nyeusi kiasi hiki? kwanini rangi nyeusi, rangi ya ngozi zetu ndio iwe chini? Arent we proud of our colour?
Ndugu wadau na mods katika siku za hivi karibuni na kipindi kilichopita wadau mbalimbali humu,wamekuwa wakiuliza sana juu ya vigezo vinavyotumika kurank jf members,majibu yamekuwa yakitolewa,wapo wanaoridhika labda wapo pia wasioridhika.Sio mbaya sisi sote ni wa moja,mie mwenzenu katika kufikiria sana,nimeonelea nipendekeza hivi: Pamoja na mfumo tulionao sasa wa rank za member.junior member,senior member na senior jf expert member nk.tureform mfumo huu au kuuongezea nyama kidogo,kwa vigezo vilivyopo sasa.Ndio kuna wale ambao labda kwa namna moja au nyingine wanaiwezesha jf kifedha na hivyo kuendelea kuwa hewani,hilo halibishiki kwa kuwa kila mtu anafahamu kuhost tovuti hii lazima tulipia tena vijipesa vingi tu.Hawa wenzetu tuwape status maalumu ya heshima labda "kama senior honorary member" au meritocrat member nk,ili mradi tu tuoneshe tunavyoappreciate michango yao na kwamba mtu yeyote akitaka kuingia katika kundi hilo la heshima,basi afuate vigezo hivyo nasi tutampa tuzo hiyo ya kuitwa hivyo.
Pili,kuna wadau wenzetu humu ni wachangiaji wazuri sana,hoja zao huwa zinaconvince sana na kwa kweli huleta maendeleo chanya.Watu hawa pia uanzishwe mfumo wa kuwatambua na kuwapongeza au kuwatunza,na hii ni kwa admins kutafuta utaratibu ambao sisi wanachama kila baada ya kipindi fulani tutapiga kura au kupendekeza mwanachama wau wanachama tunaofikiri wapewe hiyo eshima kwa mchango wao wa kifikra humu ndani,hii yaweza kuwa wakapatikana kwa thread (yaani kutokana na kuchangia sana katika thread fulani au general) kwa wale watakaotokeza mara nyingi basi tunawachangua walau watu 25 wanapewa hadhi fulani, labda "prior member au senior associate member au hata huo usinia expert member" watu kweli waoneshe expertism fulani katika mada husika au mada fulani fulani.
Na kwa wanaobakia mfano junior member,member,senior member hapa uendelee kutumika utaratibu wa kawaida aidha ni wa credit au number of posts mtu alizoziweka ama kuchangia.wadau mtanisaidia zaidi kuboresha hili wazo.
Angalisho.Hata hivyo wale wanaopewa honorarium kwa kwa kuthamini michango yao kifedha hiyo hadhi yao iwe "ceremonial tu" yaani sijui wataalamu wa kiswahili ceremonial kwa kiswahili ni nini?yaani wasiwe na nguvu ya maamuzi kuwazidi wengine,maamuzi mengo yashiriishe wadau na hawa bwana wasidominate mawazo ya wengine.Labda kwa namna moja ama nyingine watu wengi tunaweza kuwaridhisha kwa mtindo huu.Nadhani kuna mtu aliuliza ina maana mimi nikilipa hela let say 10,000 nitatoka kwenye ujunior member hadi senior au expert member? ili kuondoa mkanganyiko kama huu tuweke merit.
Mnaonaje wakuu,hebu tuchangiane mawazo,hili nimelifikiria haraka haraka tu ili kuboresha mfumo,nikalipost hapa kabla halijanitoka.Mnakaribishwa kukosoa,kuboresha au kutoa mwelekeo chanya mwingine.
Augustoons,
Wazo zuri sana, ila mimi naona tayari liko incorporated kwenye vikorombwezo vingine vilivyomo, sema labda watu hatuvitumii tu. Check thread hii:
https://www.jamiiforums.com/showthread.php?t=7889
Nafikiri inamaelezo yanayohusiana na hilo, au basi yanayokaribiana na yako.
Kingine hapa cha kukumbukana ni kuwa, karibia kila kitu kinawezekana, kile ambacho tunaweza kukifikiria kuhusiana na software. Tatizo lililopo ni kuwa, software tunayotumia vBulletin, imejengwa na watu, na vitu vingine ni vigumu kuviongezea na kuacha kila kitu intact bila ku cause security risks au stability ya software. Pia uwezo wakufanya hivyo bila ku breach terms of use ya software na copyrights. Otherwise, kuna additional utilities ambazo zinaweza kununuliwa za kuongezea madoido hapa, ila ndiyo hivyo tena... mifuko ni mifupi... lol!!
SteveD.
SteveD kumbe na wewe ni Mod au adimin wa jf? sikuwa najua!