JF ilipotaka kuchukuliwa msukule kisha igeuke zombie

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,632
697,845
Kwenye ulimwengu wa roho sio wote wafao hufa kikwelikweli .....hasa hawa wa vifo vya ajali na ghafla...hivi ni vifo vyenye mikono ya watu.

Ni katika kundi hilo ndio kuna wale wanaochukiwa utumwani kwa njia ya misukule ili wakageuke mazombie na kutumikishwa bila kubisha ama kukaidi.

Ndugu zako waking'amua na kukuwahi ama mustakabali wako ukiwa na nguvu unaweza kutoroka kabla hujageuzwa msukule zombie kamili kwa kukatwa ulimi.

Aina ya misukule hii ni mazombie yanayokuwa kama mazezeta...akili huwa nusu na robo yapo tu na hutumikishwa kama maroboti

Jamiiforums imekiepuka kikombe hiki...iliundiwa ajali ya ghafla usiku wa kuamkia tarehe 11.June. 2018....siku ya kukumbuka sana hii...kwenye gari JF alimokuwa amepanda hakuwa pekeyake bali na abiria wengine wengi tu.... Ambao hatutakaa tuwaone tena.

JF akapata ajali na kuandaliwa kuwa msukule.... Yalifanyika mengi ndani ya kipindi cha wiki tatu hivi. ....hatimaye JF akasalimika kukatwa ulimi ila akarudi akiwa kama zezeta kama zombie kabisa...lipolipo tu...no action... Una log in vizuri kabisa... Ukifika jukwaani huwezi kufanya lolote zaidi ya kuLIKE na kusoma tuu....nikajikuta naliona zombie JF...
Wajuzi na wajuvi wakaendelea kupambana mpaka JF ikafanikiwa kutoka kwenye NIRA na vifungo vya usukule na uzombie.

Pamoja na majeraha makubwa iloyoyapata pamoja na kosakosa yakuwa zombie msukule lakini hatimaye imeweza kupata uzima wake tena na sasa ni mchakato wa kuponya tu majeraha.

Niko kilingeni kwa wito maalum...kilichowekwa kaburini hakikuwa mwili wa marehemu bali pisi la mgomba tunafanya mila ,tambiko na kafara kulizimua kaburi ....mchawi mmoja keshadondoka..mwingine halali.
 
Tawire mganga.....tamba tambati ya sengo ya sese miungu kagone nhong'o.

Haikua kazi rahisi kuurudisha huu msukule, uliochukuliwa na mchawi mkuu wa anga. Angalau siku mbili hizi hali ya msukule imeimarika sio tia maji tia maji tena, anakunywa Uji kwa uzuri tu na anawatambua hadi ndugu zake kama mshana Jr, Da Vinci, baba swalehe Kiranga Demiss Bujibuji Ambiele Kiviele

Tawire baba! Mgonjwa hana zohari tena.
 
Tawire mganga.....tamba tambati ya sengo ya sese miungu kagone nhong'o.

Haikua kazi rahisi kuurudisha huu msukule, uliochukuliwa na mchawi mkuu wa anga. Angalau siku mbili hizi hali ya msukule imeimarika sio tia maji tia maji tena, anakunywa Uzi uzuri na anawatambua hadi ndugu zake kama mshana Jr, Da Vinci, baba swalehe Kiranga Demiss Bujibuji Ambiele Kiviele

Tawire baba!
Tawire baba
 
Vipi usalama wa kuwalinda watumiaji upo? Piga makombora ya nguvu huko kilingeni,we born town huwezi shindwa na wakuja waliokuja na mbio za Mwenge au gari za ng'ombe town Leo wanajiona wajanja baada ya kuonyeshwa mataa ya ubungo
Tumefundishwa kuwa werevu kama nyoka....ya juzi sio ya Jana.....muhimu kukagua uzio wako na kuimarisha nguzo zilizolegea na kuchoka
 
Tumefundishwa kuwa werevu kama nyoka....ya juzi sio ya Jana.....muhimu kukagua uzio wako na kuimarisha nguzo zilizolegea na kuchoka
True mawazo ya miaka ya 60 hayawezi shindana na mawazo ya milienium.Dotcom forever.Umekuja mjini Mkubwa utashindana na dotcom.
 
Hakuna post ya KT inayodumu humu...zote zinafutwa dakika kadhaa tu baada ya kupostiwa na pia Mods hawatoi hata sababu za kufuta.

Watuambie kama haturuhusiwi kupost lolote linalohusu KT ili tuwe aware.
Kwanini?nini mbaya?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom