Shambulio la Lissu: Wajue wasiojulikana watakaojulikana na 'Wasiojulikana' ambao kamwe, hawatajulikana

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,553
Wanabodi,

Tangu kutokea kwa shambulizi kwa Mhe.Tundu Lissu, ambalo mpaka sasa linaelezwa kufanywa na watu wasiojulikana, kumeibuka shauku kubwa ya watu kutaka kuwabaini hawa watu wanaoitwa ni watu wasiojulikana, ni kina nani?, wanatumwa na nani? na lengo lao ni nini?, kunakopelekea kujengwa kwa dhana mbalimbali kuhusiana na wasiojulikana hawa, hadi kufikia kuwanyooshea vidole baadhi ya watu, wakiwemo wale 'jamaa zetu' kuwa ndio watu wasiojulilana!.

Ukimya wa Jeshi letu la polisi kuhusu matukio haya, japo ushahidi wa wazi upo lakini hakuna any update ya uchunguzi, na utulivu wa Comred Mwingulu Nchemba, kuonyeshea, he knows something kinyume cha dhamira yake, ila kujiuzulu kwa awamu hii ni suicide, hivyo Mwigulu yupo yupo tuu na kimya hiki kitampelekea ama kutumbuliwa ama kubadilishwa na kuwekwa mtu ambaye ana uwezo wa kusema uongo wa mchana kweupe na macho makavu ili kuitetea serikali kila inapo mess!. Kwa vile Mwigulu ni mtu wa haki, ameamua kuliko kutenda dhambi ya kusema uongo, na kumkosea Mungu wake, ameamua bora ajinyamazie tuu kimya kusubiria hatima yake, huku ameisha amua liwalo na liwe kwenye hatima yake!, of which time will tell!

Kufuatia taarifa nyingi za watu wasiojulikana kuhusika kwenye baadhi ya matukio na Jeshi letu la polisi ndio mamlaka rasmi ya uchunguzi nchini Tanzania (nchi za wenzetu wanazo private investigators, mamlaka rasmi ikishindwa, unaajiri private investigator, uchunguzi unafanywa), na mara zote jeshi letu la polisi hutoa taarifa kuhusu kuhusika kwa watu wasiojulikana ambao mwisho wa siku hubakia hivyo hivyo kuwa wahusika wa tukio fulani ni watu wasiojulikana, ambao hawajajulikana mpaka mwisho!.

Kumbe sometimes sii kweli kuwa wahusika wa kila tukio ni watu wasiojulikana, sometimes wahusika wa matukio hayo sio watu wasiojulikana bali ni watu 'wasiojulikana'!

Hivyo hili ni bandiko fikirishi tuu la dhana dhanifu ya kuwahusu watu wasiojulikana vs 'wasiojulikana' ambao mwisho wa siku baada ya uchunguzi wa kipolisi, wasiojulikana watakuja kujulikana, na 'wasiojulikana' kamwe hawatakuja kujulikana kwa njia za kawaida ila kitu kinacho itwa karma kitakuja kuwajulikanisha mmoja baada ya mwingine, tatizo ni wakati karma ikiwajulikanisha, hakuna watu wa ku connect the dots kuwa hiyo ni karma ya tukio gani.

Hivyo kuna mashambulio yanayofanywa na watu 'wasiojulikana', ambao hawa, kamwe hawakuja kujulikana!, haswa pale ambapo 'wasiojulikana' hawa ni wale 'jamaa zetu'!, ila karma itawashughulikia.

Hebu fuatilia jinsi hawa ,'jamaa zetu'!. 'wasiojulikana', wanavyotekeleza mashambulizi mbalimbali na sometimes hadi elimination in a very professional way by doing a clean job hivyo kamwe hawawezi kuja kujulikana, hivyo kubaki ni watu 'wasiojulikana', daima dumu!.

Hii hapa chini ni mifano tuu ya baadhi ya dhana hizo, na sio lazima iwe ni kweli, ila haya matukio ni matukio ya kweli yaliyotokea, sio lazima yawe yalitekelezwa na 'wasiojulikana', yanawezekana yalitokea tuu naturally ila kwa vile kulikuwa na dhana zilizosemwa, mimi nayataja tuu matukio haya na links ya dhana zake, ili ufikie conclusion wewe mwenyewe na sio kulishwa hitimisho.

1. Kuna kiongozi mmoja mkubwa serikalini anayesemekana alikufa kwa ajali ya gari, ila mwili wake ulikutwa na majeraha ya matundu ya kitu fulani!, inasemekana ni wale 'jamaa zetu'
Kifo cha Sokoine: Tujiondoe jela ya kifikra | JamiiForums | The ...

2. Aliyekuwa Waziri wa Fedha wa Mwinyi, Kighoma Malima alipo defect kutoka CCM na kujiunga na upinzani, chama cha NRA, aliugua ghafla na kupoteza maisha!. Inasemekana ni wale 'jamaa zetu'.
Ukweli wa kifo cha Kighoma Ally Malima ni upi? | JamiiForums | The ...

3. Aliyekuwa Katibu Mtendaji Mkuu wa CCM, Horace Kolimba akiwa CCM high ranking oficer, aliposema "CCM imepoteza Dira na Haina Mwelekeo", alipoteza maisha kwa kuanguka ghafla baada ya kuhutubia, ikasemekana niwale 'jamaa zetu'
Kabla ya kutoka ccm jiulize mara mbili;horace kolimba,gen kombe ...
Wananchi wakitaka kujua nani alimuua nani? | JamiiForums | The ...
Vifo vya viongozi vyenye utata | JamiiForums | The Home of Great ...


4. Kiongozi mwingine mkubwa wa serikali alifariki ghafla baada ya tuu ya kukamilisha ziara ya kutembelea maonyesho ya Saba Saba, mmoja wa hao 'jamaa zetu' aliyejiunga jf, alituhadithia kwa kutueleza baadhi ya madudu ya 'jamaa zetu'
Kikwete, huu mtandao ni hatari! Be careful, otherwise waweza kuwa ...

5. Tukio la kifo cha Imran Kombe aliyekuwa DG wa Tiss, aliuwawa nje nyumbani kwake nje kidogo ya mji wa Moshi baada ya kufuatiliwa na ma snipers wa polisi alipokuwa aki drive kutoka Dar. Baada ya kukamilisha kazi, ilatolewa taarifa kuwa ni kweli ameuwawa na polisi kwa bahati mbaya kwa kudhaniwa ni jambazi!.

6. Tukio la kutekwa kwa Dr. Ulimboka, Absolom Kibanda, Roma Mkatoliki, Mwandishi wa habari wa DW, Salma Said, Mwandishi wa habari wa gazeti la Mwananchi Azory Gwanda, na kupotea kwa mwana jf maarufu Ben Saanane, pia kukihusishwa na wale 'jamaa zetu' kwa jina la wasiojulikana kumbe ni 'wasiojulikana'.

7. Tukio la Uvamizi wa Kituo cha TV cha Clouds TV kilichofanywa na wale makirikiri wenye silaha wanasemekana ni wale 'jamaa zetu' na walitumia Nissan Patrol Nyeupe!.

8. Yule mpuuzi aliyemnyooshea Nape bastola, anajulikana kwa sura katika media zote, na alikuja kwa kutumia gari aina ya Nissan Patrol Nyeupe, naye licha ya picha yake na sura yake kuenea kote kuanzia kwenye mainstream media hadi kwenye social media, lakini na yeye a anaelezewa kuwa ni mtu 'asiyejulikana'!. Taarifa za chini chini zinaeleza huyu jamaa ni miongoni mwa wale jamaa 'jamaa zetu'.

9. Kuna huyu Blogger wa Kenya amesema haya kwenye mitandao ya kijamii, Blogger Robert Alai(Kenya) atoa siri ya waliompiga Lissu risasi. Amtaja RC Makonda...

hadi akataja majina ya wahusika na magari yaliyohusika ikiwemo hiyo Nissan Patrol Nyeupe na sijasikia yoyote akikanusha taarifa ya blogger huyu!, hata serikali yetu kukanusha. Hivyo sometimes silence ni admission of guilt, kwa vile ni 'wasiojulikana', hawana sababu ya kujibu lolote wasije wakajulikana!.
Hii inapelekea mimi kujiuliza maswali haya.
  1. Kama wahusika wa Tukio la shambulio la Mhe. Tundu Lissu, ni wale 'jamaa zetu', kwa vile wale ni ma pro, they have one million ways to do things, in a good clean job in a professional way na not leave and traces behind, and they have never missed a target!, sasa kama kweli ni wao, ndio waliomshambulia Lissu, how could they do such a bad dirty messy job?!, how could they missed a target in such close range?, hadi watumie risasi 38!, wakati kwa trained snipers, only one is enough?!.
  2. Tuambiane ukweli jamani, hawa waliofanya haya watakuwa sio wale 'jamaa zetu!' na kama ni kweli walikuwa wale, saa hizi si tungekuwa tunazungumza mengine?!.
  3. Unless kama ni kweli ni wao, ila wamejifanya to miss the target makusudically ili ku dupe the public kwa kupotezea maboya ili kupoteza lengo ionekane waliofanya tukio lile sio ma pro ili tukio lionekane limefanywa na amateurs!.
  4. Kama 'jamaa zetu' have 100 ways to do elimination in a good clean professional way by doing it right in a clean job, on natural death look aike, kama natural accidents, or any clean job that nobody would've suspected anything, why did they do such a mess, such a bad dirty job?!.
  5. Hawa "jamaa zetu" hufanya elimination kwenye some serious security threats to our national security, or threats to the status quo of the ruling elites waliopo, swali la kujiuliza ni kwa the ruling class ya sasa when was Mhe.Tundu Lissu, has ever been such a threat to warrant such elimination?!. Kama kuna defectors very high rankings wame cross na wamejizolea kura nyingi kuliko zilizomuingiza rais Kikwete madarakani ile 2010, hawa ndio the real threats!, hivyo kama issue ingekuwa ni eliminations for status quo threats, kwa nini hawa ambao ndio the real threats wasiwe targeted aje kuwa targeted Lissu?, Why Lissu?!.
  6. What if kilichomtokea Lissu ni kutokana na issue nyingine yoyote na sio siasa?. Hili niliwahi kuuliza humu JamiiForums.
  7. Kama kuna chama viongozi wake waliwahi kutuhumiwa kupanga vitendo vya ugaidi na utekaji na video zikaletwa humu, hawawezi kuwa ndio wao wao waliopanga mpango huo?, kwa kufanya timing ya Dodoma ili wadhaniwe ni 'wale jamaa zetu'?.
  8. Kama Wangwe alipotaka kugombea uenyekiti alikufa kwa ajali yenye utata mpaka kesho, na huu ni mwaka wa uchaguzi wa ndani, haiwezekani ikawa ni an inside job ya friendly fires?.
  9. Kama Zitto alipotaka kugombea Uenyekiti alifanyiwa a life atempt kwa sumu, lakini kwa vile ameaga kwao, akasalimika, haiwezekani na Lissu pia ameaga kwao na ndio maana amesalimika?.
  10. Kama Mlinzi wa Dr. Slaa, alieaminika sana, lakini alipostukiwa, alishughulikiwa ipasavyo!. Haiwekani dereva wa Lissu has a hand ila hajastukiwa?!.
  11. Maadam Chadema wanao utaratibu wao wa ndani wa kuwashughulikia watu ambao threats kwao. Jee haiwezekani tukio la Lissu linaweza kuwa ni an inside job? na alihudumiwa hivyo na watu wao? ndio maana dereva hakuguswa?!. Kama watu wanaoweza kushughulikia hivi binadamu wenzao, they are capable of doing anything, then haiwezekani hii sasa ndio the advanced methods za kudeal na the internal threats zao?.
Conclusion Kuwahusu hawa Watu Wasiojulikana na 'wasiojulikana', according to the motive behind the shooting.
1. Threats to National Security.
If the motive behind the shooting ya Lissu ni kwa sababu he is very vocal hivyo kuonekana ni mwiba, then hawa wanaoitwa ni wasiojulikana, kiukweli sio wasiojulikana, hawa watakuwa ni 'wasiojulikana' ambao ni wale 'jamaa zetu', kama ni wale 'jamaa zetu', then hawa sio watu wasiojulikana, hawa ni watu 'wasiojulikana', kama yule mpuuzi aliyemshikia Nape bastola ni mtu 'asiyejulikana' na mpaka leo hajulikani na kamwe hatajulikana, and if this being the case, then watu hawa hawatajulikana kabisa, hata yule aliyetajwa na blogger wa Kenya, pia ni mtu 'asiyejulikana'. Ila hukumu ya karma itawahusu wahusika wote.

2. Party Politics hivyo this is an inside job.
Kama the motive behind the shooting ya wasiojulikana hawa ni partly politics ya siasa za ndani za run of kuelekea 2020, then polisi wetu waendelee na uchunguzi, soon watasalitiana na tutawabaini wasiojulikana hawa na watu humu watabaki midomo wazi kwa kutoamini.

3. Divide and Rule za Mabeberu
Lakini kama the motive behind wasiojulikana hawa ni hawa mabeberu wezi wa rasilimali zetu na lengo lao ni kutufarakanisha sisi na serikali yetu kwa devide and rule, wagawanye uwatawale, ili kutuhamisha kwenye hoja za rasilimali zetu, ili tusahau makinikia, Tanzanite, Dhahabu, Almasi na Gesi, then, sisi as sisi, hatuna uwezo huo wa kuwabaini bila msaada wa Scotland Yard, ila, kwa vile tayari, tumeisha wastukia nia yao ovu, hatuta farakana, tutasimama firm as one, and under th e united front. Kama lengo ni ili tufarakane, tuichukie serikali yetu kuwa ni ya kidikiteta, na kuanza kufanya vurugu, tukifarakana, tutakuwa tumewapa walichokitaka, tusikubali kufarakana, kwa kufakaranishwa na wafakaranishaji hawa, lets stand together as one, tupendane, tuheshimiane, tuvumiliane, tustahimiliane, tubishane bila kupigana, tukubaliane kwenye maslahi ya taifa na ikishindikana tukashindwa kukubaliana, then tukubaliane kutokubaliana lakini mwisho wa siku, wasiojulikana wajulikane lakini 'wasiojulikana', sijui.

I'm not very certain kuhusu majaaliwa ya position ya Mwigulu, but lets keep on, wishing TL, To Get Well Soon!.

Paskali
 
Tatizo lako unapenda sana vitendawili, inawezekana ndiyo ilikuwa nguzo yako kubwa katika kufaulu hilo jisomo darasa la pil enz zako. Ss yakija kutokea ambayo hatuyajui baadae, utakuja kutubananisha kwenye thread yako hii hapa uliyoiandika Leo, huu nao ni umaarufu wako, wengi wetu tumeshakujua. Be critical, kwa sababu tulipofikia hakuna haja ya kumun'gunya mun'gunya maneno. Ulipata bahat ya kuuliza swal la msing ikulu, ukaitendea vema taaluma yako, tukapata tafsiri ya jina lako katika kabila flan kuwa maana yake ni NJAA!!! Sikuwa najua, na hainihusu hili.
 
Ukweli lazima tuseme CHADEMA they are behind this well planned na mwenyekiti na mwenye chama THUS WHY kila siku tunasema humu FAMILIA ya LISSU they are should be more close na ndugu yao kuliko hao kina mbowe...WASIWAAMINI KABSA
Watu vwa EAGLE kamwe hawezi kupiga risasi kizembe hivyo na kama kweli wangekuwa ni wao lazima wangeakikisha LISSU kapotea kabsa kwenye USO WA DUNIA hiyo ndio one of the principles za watu wa EAGLE.....

Afu suspect mwingne ambaye naweza amini kabsa anaweza kuwa BEHIND this ni hawa CUF MAALIM...tuna wasahau sana hawa jamaa......na wao the only option ya kupambana na SERIKALI YA CCM ni kutengeneza matukio ya namna hii
 
Utawaamini vipi Scotland Yard kufanya huo uchunguzi wa wanao tufarakanisha kama mmoja wa member wao walioko kwenye mazungumzo na Tanzania juu ya swala la makinikia ni High ranking officer wa kikosi cha anga cha Uingereza?


Mimi namsubiria tu karma alete mrejesho wengine wote sina imani nao kuanzia serikali nk
 
Back
Top Bottom