JF Focus: Interview with Maxence Melo

nawaombea msamaha malaria sugu na faiza foxy(Jf contrevesial iconic figures).Je max yupo tayari kuwafungulia?
Swali la mwisho;Jf iko kwa maslahi ya nani?

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA

Asante sana. Suala la ban ya members linahusu Moderators zaidi hivo nadhani linaweza kupelekwa tu jukwaa la complains congrats and advices na likajibiwa. Kwa vile sio kila siku tunapata nafasi ya kumuuliza Maxence strategic questions of management and leadership within JF, bora uulize masuali ambayo hatuwezi kupata majibu toka kwa moderators. Kumbuka tuna masuali 10 tu.
Hilo la maslahi ya JF nalifikisha kama lilivo na nadhani litachaguliwa katika masuali kumi ya kumuuliza mkuu Maxence.
 
safi sana ila kiingereza cha nini sasa???aargh

Poleee... Hapa JF tunaruhusiwa kutumia Kingereza, kiswahili na ikiwa ni jukwaa la lugha hata kifaransa kimeruhusiwa lately. Nadhani hakuna kilicho haribika kwa vile message imefika mkuu.
 
Asante sana mkuu, maoni yako yamefika na nadhani mkuu Maxence anaweza kujibu haya pale atakapo kua nasi on Friday the 17th.
 
Naona Russian umegonga kingleza cha kum impress boss. Zamani tulikuwa tunaita mabomba...

Muda huo utakosa baadhi ya nguvukazi za taifa zitakazokuwa zinajenga taifa. Najua umeangalia data zenu huko na kujua Prime time humu JF ni ipi!
 
Nami nipende kutoa shukrani zangu za dhati kwa Max, Mike na timu nzima ya JF.

Japo nipo JF kwa takribani miaka minne sasa ni mara ya kwanza nashuhudia tukipata nafasi ya kumuuliza Max maswali ya hapo kwa papo.
Swali langu ni moja tu: Japokua JF inakua siku hata siku, na tunaona wanachama wapya wakijiunga kila leo, Je ni nini basi kilichofanya Jamiiforums ya leo kutokutoa habari motomoto kama ilivyokua wakati wa Jamboforums( Tukikumbua zile Ijumaa za Mwanakijiji na Vi inzi vyake) kwa maana ya nyaraka na habari za ndani sana zilizopelekea JF kutikisa kila kuta za nchi?


Je kuna mkono uliozuia hili? ama kwa kuwa ile risk ya habari kama zile inabebwa na watu wachache lakini wanaofaidika ni wengi hivyo kupelekea wale wachache kukata tamaa? .Ni hayo tu kwa sasa ila siku nikibahatika kukutana na Max nitamuuliza mengi zaidi
 
Pongezi nyingi kwa Max and the entire JF crew.

We are missing the old good days of JamboForums where JF used to be more of 'WIKILEAKS' kind of, and over the years, I have observed JF undergoing complete 'metamophorsis' into some form of a SOCIAL MEDIA.

My question is; waht was the original vision of JF founders Vs the current direction having taken into account to address socio-political dynamics in the region. I presume there have been major deviations.
 
big boss, I'm here now.
Worry out, Roulette yuko makini, nikishindwa kuwepo atafanya utaratibu.

 
Roulette, nashukuru kwa uteuzi huu ambao ni rare. Na haswa kwa kuniamini (inabidi nisilipulize sasa, aaghh!)

all, nawashukuru kwa maswali yenu ya utangulizi. Please keep them coming. Binafsi I'm so proud of jf na Maxence personally kwa sababu ya umakini na ni mtu anaeshaurika na kufanyia kazi maoni na maono pia. Can't wait for this day, Mungu atupe uzima
 
Last edited by a moderator:
Max, Mike and the all crew..natanguliza hongera maanake kazi kubwa mlofanya haina kipimo na Mungu awazidishie kila la kheri mfikie mafanikio makubwa zaidi ya haya yaliyopo..

Binafsi sioni tatizo, guyz you have done it!..endeleeni kuweka utaratibu mzuri wa kupokea watu kule baraza la wazee wa busara!..viwanja vingine kama vinavyojieleza, SIASA zitakuwa siasa za migogoro kila siku zote na hamuwezi kuzuia kila kitu kila mtu..
- Kazi njema
 
Swali langu kubwa kabla ya kutoa pongezi kwa Maxence Melo ni nini matarajio na malengo ya uwepo wa JF kwa sasa na baadae haswa ikichanganywa na kukuwa kwa teknolojia ya mawasiliano ambapo JF inavuma hadi vijijini
Tutarajie kipi kwa hali ya sasa na ya baadae kutoka Jf ambacho kitawafanya watumiaji wake waendelee kuipenda na kuisupport JF
Je malengo ambayo wakati anaianzisha JF yametimia, yatatimia,au yamefikiwa na nini matarajio au maboresho ambayo anategemea kuyafanya kuiweka JF juu zaidi ya hapa ilipo
Baada ya hayo nampa pongezi sana Maxence Melo kwa kuwa na wazo hili la kuanzisha JF ambapo kimekuwa kisima cha kuchota na kupata habari mbalimbali na utaalam ambao kwa namna moja au nyingine unamsaidia mtu mmoja mmoja au watu wengi kwa pamoja
 
Last edited by a moderator:
Dah ninamaswali mengi sana ila na wewe Madame ya kupasa uwe kwa pembeni kwani nauhakika watu watataka kujua zaidi juu yako japo naona maswali yatakuwa kwenye chekecho hivyo itakuwa nikazi kubwa kumaliza kihu ya wachangiaji!!Kwa yote mimi naanzia hapa kumpa shukurani za dhati kwakuweza kuanzisha chombo hiki!!mbali na hiyo kuweza kusimamia mawazo yake!niwengi wanaanzisha lakini kwakosa kusimamia mawazo yao wameshindwa kufika mbali!!
 
Roulette, hongera kwa kuja na mada nzuri na ya tofauti. yale niliyokuwa nayo kichwani kuhusu JF yameshaulizwa na wenzangu hapo juu, mimi swali langu ni moja tu HIVI KUNAKUA NA UTARATIBU GANI WA KUWAPATA MODERATORS? Na kuhusu jinsi hawa MODS wanavyofanya kazi ningeomba kujuzwa maana nina uhakika hawajaajiliwa na JF wanafanya kwa moyo wa kujitolea sasa inapokuja suala la vitendea kazi kama Computer na Internet uongozi wa JF huwa unawa support? Ningeomba mkuu Max aliweke sawa hili swali maana huku mtaani JF inahusishwa na CHADEMA na mzee Mwanakijiji
 




Asante sana kwa pongezi ndugu, bila shaka zimemfikia Maxence na team nzima. Suali lako ni nzuri sana maana wengi wanasema Jamii Forums ya leo sio sawa na ile ya zamani. Labda Maxence ataweza kuthibitisha hili na kutupa mtazamo wake. Asante sana, na karibu siku hiyo.
 
Naona Russian umegonga kingleza cha kum impress boss. Zamani tulikuwa tunaita mabomba...

Muda huo utakosa baadhi ya nguvukazi za taifa zitakazokuwa zinajenga taifa. Najua umeangalia data zenu huko na kujua Prime time humu JF ni ipi!

Mkuu, hapa nipo kikazi zaidi, na boss ndie anaalikwa interview, lazima niwe makini. Lugha zote mbili na-struggle ila niliona bora hata kingereza kuliko kiswahili kibovu maana kiswahili nitakua sina excuse ila kingereza naweza kusema ni lugha ya kuazima. hahaha

Kuhusu timing, kuna baadhi ya watu wanapata access internet siku za wiki tena saa za kazi peke yake. Last time tuliendesha mjadala weekend na wengi waliomba safari hii tuweke office time. In any case, we will gather all questions during the week na majibu yatatolewa Ijumaa ila hata weekend yatakua accessible.
 
Asante sana mkuu kwa pongezi, nadhani limewafikia Maxence, Mike na team nzima la Jamii Forum. Pia ushahuri wako umefika, tutajaribu kuzingatia hilo. tunashukuru sana kwa mchango.
 

Mkuu, we ni mjanja, sikuwezi. umeuliza two in one: unataka kujua kama malengo yametimia na pia unataka kujua kuna strategy gani in store ya kuwafikia watanzania wa vijjini. Noted mkuu.
 
Nashukuru kwa maoni, kuhusu masuali yanayo nihusu kwani nani kakataza kuniuliza? tumieni njia ya PM, na kama nitaweza kujibu nitajibu, kama siwezi nitatoa sababu. Hapa tunauliza strategic and managerial questions zaidi, ambazo mimi kama Mod naweza kua sina jibu kwa baadhi ya suali hizo. Ni fursa ya kipekee kwa wengi wetu ambao labda hatuwajui Mike wala Max in person.
 

Asante sana kwa pongezi, na kwa busara yako ya kutorudia masuali ambayo yamesha ulizwa na great thinkers wenzetu. Hili suala la vigezo vya kuwachagua moderators, pamoja na namna yao ya kutenda kazi limesha ulizwa huko nyuma, nadhani ni wakati muafaka wa kupata jibu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…