Ahsate sana
Roulette kwa thread hii muhimu sana,
Kwanza kabisa, nakupongeza wewe na wakuu wote katika timu ya uendeshaji wa JF (chini ya kamanda Max) kwa kazi ngumu ila muhimu sana mnayofanya ya kuiendesha, tena kwa mafanikio makubwa. Huwa mara nyingi nasema kwamba, hata kama mambo mengi yanatushinda na tunaonekana vilaza/viazi (wajinga wa kutupa), JF imeonesha pasipo shaka kwamba Watanzania tunaweza kubuni na kutekeleza mambo yetu kwa kiwango cha juu kabisa cha mafanikio!!
Pili, naomba nikiri kuwa mimi binafsi nimekuwa nikiguswa sana na JF kama network na manufaa ambayo sisi members na wadau wengine wanayapata. Hata hivyo, ningependa kujua mpango mkakati wa kibiashara wa JF (JF business strategic plan) kwa muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu (short term, medium and long term business strategies) ambazo zitaonesha jinsi management ilivyojipanga kuhakikisha hili jukwaa halifi kama policies zetu including ujamaa zilivyokufa kifo cha ajabu ajabu.
Pia, naomba Max atueleze ni kwa jinsi gani management ya JF imejipanga kuwashirikisha members katika kuipa uhai JF (financing and running) ili kuwapunguzia mzigo wadau wachache ambao wamekuwa wanatumia muda wao na resource zao nyingi kuhakikisha JF inaendelea kuwepo hewani!
Naomba niishie hapa ili wadau wengine waongezee!