KalamuTena
JF-Expert Member
- Jul 7, 2018
- 13,189
- 17,157
JokaKuu,
Tunaweza kuyajadili yote haya:
1. "kuonea wananchi katika kampeni dhidi ya 'walioitwa wahujumu uchumi"' Sijui hapa umewalenga 'wananchi' au 'walioitwa wahujumu uchumi'. Natambua 'wahujumu uchumi' nao ni wananchi; lakini wanatambulishwa na sifa yao hiyo ya nyongeza.
2. "Mwalimu Nyerere na Sokoine walishindwa kuendesha uchumi wa nchi."
3." Badala yake wakaanza kulaumu na kusingizia kuwa hali mbaya ya uchumi imesababishwa na wahujumu uchumi na walanguzi" Hapa nitapata fursa ya kujifunza kutoka kwako juu ya ushahidi wa hawa wawili kuzitumia sababu hizi kuwa ndio zilizosababisha anguko la uchumi.
4. Itakuwa ni fursa ya nadra pia kupata nafasi ya kujua heshima anayopata Sokoine imejikita zaidi katika "kutambua mchango wake alipokuwa waziri mkuu wakati wa vita vya Kagera." Bila ya vita hivyo "usingewaelewa wanaomkubali Sokoine".
Yote haya manne tunaweza kuyajadili vizuri tu.