JF Exclusive: Video/Audio ya Waziri Mkuu Edward Moringe Sokoine (1978)

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Mar 10, 2006
33,040
2,000
Tukiendelea na mijadala mingine nimeonelea niwashirikishe video hii. Nimeulizwa mara kwa mara kuhusu video/ audio ya Edward Sokoine. Katikati upekuzipekuzi wangu nimekutana na hii. (Kuna mtu aliniuliza chemba kuwa angependa kumuona na kumsikia Sokoine) badala ya kusoma tu habari zake. Hii ni miongoni mwa video nzuri nilizopata kuziona au kuzisikia.

 

mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
51,760
2,000
Screenshot_20191115-210223.jpeg
 

Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
2,130
2,000
Tanzania hatujaweza kupata Waziri Mkuu mchapakazi kama huyu. Sokoine ndiye aliyeanzisha daladala yaani alipita pale Posta (Opps Posta ya Zamani si hii mpya) na msafara wake akaona watu wengi wanasubiri usafiri, akauliza pana nini hapa? Akaambiwa wananchi wanasubiri UDA kwa usafiri wa kwenda nyumbani.

Basi kesho yake akaagiza mabasi yote ya mashirika ya umma wakati ule yakimaliza kuwaleta/ kuwarudisha wafanyakazi yaendelee kuwachukua wananchi kuwaleta kazini na wenye mabasi binafsi waanze kufanya hivyo kama wanaweza. Ndipo ikazaliwa daladala. Alikuwa anajali Maisha ya wananchi wa Tanzania.

Hata kabla ya kifo chake, ndege iliyotakiwa kumrudisha Dar es Salaam kutoka Dodoma ilichelewa, basi akasema hakuna shida nitakwenda Dar kwa gari, hapo ndipo alipokutana na mauti kule Morogoro (Dumila).

Watu wengi walikuwa wanasema kwamba JK Nyerere alikuwa anamwandaa kuwa Rais akiondoka kwa sababu hiyo ilikuwa ni mara yake ya pili kuchukua cheo hicho baada ya kujiuzulu, ikumbukwe Mawaziri wengi wanyakuaji walikuwa wanamuhara.

Mwenyezi Mungu ailaze roho yake peponi salama.
 

Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
2,130
2,000
BTW msingi wa kuitwa daladala ulikuwa hivi: Shillingi tano za Kitanzania zilikuwa sawa na dola moja ya marekani na pound sterling 1 wakati huo tulikuwa tunabadili kwa shillingi 7 (saba). Hivyo mabasi hayo kuitwa daladala.
 

JokaKuu

Platinum Member
Jul 31, 2006
21,129
2,000
Ni ajabu sana; lakini katika hili naungana nawe moja kwa moja.
"Uzalendo usiotiliwa shaka yoyote."

'Uzalendo' usiohitaji kuwahimiza wengine wautambue, bali wanauona wenyewe bila ya shurti.

Ni kweli alikuwa mzalendo, lakini alionea wananchi katika kampeni dhidi ya walioitwa wahujumu uchumi.

Mwalimu Nyerere na Sokoine walishindwa kuendesha uchumi wa nchi, badala yake wakaanza kulaumu na kusingizia kuwa hali mbaya ya uchumi imesababishwa na wahujumu uchumi na walanguzi.

Nawaelewa zaidi wanaomkubali Sokoine kwa kutambua mchango wake alipokuwa waziri mkuu wakati wa Vita vya Kagera, na siyo wakati wa vita dhidi ya wahujumu uchumi.
 

Ole

JF-Expert Member
Dec 16, 2006
2,130
2,000
JokaKuu,
Vita ya uhujumu uchumi haikuweza kutekelezwa wacha uongo, sababu kubwa ni pale wahindi wengi walipokwenda kutupa TV sets baharini pamoja na mafridge nk. lile zoezi lilisitishwa ile pekua pekua ya kila nyumba haikufanyika. BTw Sokoine will be credited for so many things, hata bidhaa ambazo zilikuwa hazipatikani Tanzania yeye ndiye aliyesema zianze kuuzwa Tanzania baada ya ziara yake ya mikoa ya Tabora na Kigoma. (Kwa sababu wakati ule hata masufuria tu tulikuwa hatuna)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom