JF Exclusive: The Buzwagi Contract

JF Exclusive: The Buzwagi Contract

Samahani sikuona kuwa kulikuwa na thread hii. Nilianzisha thread ambayo ninategemea kuanza kuichangia kuhusu mkataba huu kuannzia jumatatu ijayo nikisharudi nyumbani. kwa vile mmeshaanza, basi nitakuja kutoa mchangu hapa hapa.
 
Nilipotoka kijijini kwa mara ya kwanza kwenda Dar kwenda kuuza mahindi na kununua mitumba ya kurudi nayo kijijini nilipewa onyo moja. Ogopa matapeli. Sikuelewa matapeli ni nini hadi nilipokuwa mitaa ya congo najaribu kujikusanyia mitumba na viatu vya puma, pamoja na suruali za kodirai. Kwa macho yangu niliona wakiifunga kwenye magazeti na kuniwekea kwenye mabegi yangu. Ilikuwa baada ya kuondoka na kufikia kwenye hoteli niliyofikia pale Manzese Msufini (lilipo daraja la kuvusha watu) ndipo nilipoelewa tapeli ni nini. Nilipofungua begi langu kuangalia vile nilivyonunua kwa ajili ya babu, bibi, mkaza mjomba, shangazi yake babu, na binadamu mdogo wa baba yake shemeji nilijikuta nimepigwa na butwaa! Ndani ya misokoto ya magazeti kulikuwa na matambara ya rangi rangi na hakukuwa na suruali ya kodirai wala shemeji yake kodirai.. hakukuwa na viatu wala nini... Nilikuwa nimeingizwa mjini!! Niliporudi kesho yake pale mtaa wa Congo.. yule jamaa aliapa kwa wazazi wake na kuwalala wazazi wake kuwa hajawahi kuniona maishani mwake!!!

Ndugu zangu, tumetapeliwa kwenye hoteli ya London.... it is as simple as that..
 
Karibu tena mkuu na pole sana kwa mihangaiko ya kimaisha.....tulikuwa tumekumithi!!! tumegee na nyinginezo za darisalama.....kama vile hali ya maisha kwa ujumla!.
 
Samahani sikuona kuwa kulikuwa na thread hii. Nilianzisha thread ambayo ninategemea kuanza kuichangia kuhusu mkataba huu kuannzia jumatatu ijayo nikisharudi nyumbani. kwa vile mmeshaanza, basi nitakuja kutoa mchangu hapa hapa.

Asante Kichuguu...

mchango wako utasaidia pia kuelewa baadhi ya maneno yalotumika hapa! pole na mihangaiko.... na karibu tena kijiweni
 
4.7 The company shall be allowed to deduct 80% of capital expenditure in the year incurred, thereafter at 50% per annum on declining balance method, provided that the Government shall have made legislative changes to ensure that this provision is applicable under the laws of Tanzania


Kwa wale mliosoma very simple accouting kama AC 100 au the like, jamaa wanaamua wao ni njia gani ya depreciation watumie.... hii ina maana kwamba kila mwaka wakipata faida.... wanaweza kuifuta faida yote kwa kusingizia kuwa wamefanya capital expenditure na hivyo wanahitaji 80% itolewe kwenye faida kabla ya kulipa kodi



This is wasup man!
 
Wanachama wenzangu wa JF,
Naanza kwa kuwapa hongera kemkem kutokana na jinsi mnavyomwaga ukweli wenye kuuma pande zote. Baada ya hapo nawaombeni samahani sana kwa kutoweka bila kuaga; wakati mwingine mihangaiko ya maisha haitabiriki. Nimefurahi kukuta mijadala kemkem kibao inaendelea hapa kijiweni. Bado nipo hapa Dar nilipokuja kwa muda mfupi kwa mambo ya kifamilia, jana nilipata bahati ya kukata kinywaji na rafiki zangu wachache ambao wana nyadhifa kubwa serikalini. Nilishangaa sana kugundua kuwa wanaiogopa sana Jambo Forum to death. Wanasema inatoa vijembe vikali ambavyo wakati mwingine huwa vinahusu mambo waliyoshiriki katika kufanyia maamuzi. Nilichojifunza ni kuwa vijembe vya hapa kumbe kweli vinawafundisha adabu baadhi ya vigogo wetu.

Kwa hapa mtaani nimefanikiwa kupata nakala ya mkataba wa Buzwagi, na kweli kile ni kichekesho kabisa wala siyo mkataba unaweza kuwa umeingiwa na serikali ya watu wenye akili zao. Inawezekana mmekisha ujadili mkataba huo hapa , lakini nitarudi na uchambuzi wangu kipengele kwa kipengele kupitia articles zote 18 ambazo nyingi zinaweka masharti ya kuinufaisha kampuni tu wala wala hakuna masharti ya kuinufaisha serikali. La muhimu ni kutambua kuwa mkataba ule siyo binding kabisa na unaweza kupingwa mahakamani kwa vile hauna "Seal ya Serikali ya Tanzania," na wala hakuna shahidi independent aliyethibistha kuwa ulisainiwa kihalali bila kulazimishana kwa vitisho. Mtu yeyote anaweza kuandika document kama hiyo na kudai kuwa ni mkataba wa serikali.


Pole kwa kuuguza

Nafarijika na maneno yako hawa mafirauni wanafikiri Tanzania ni ya kwao peke yao na familia zao . Tutakula nao sahani moja.

BTW umeongelea seal ya serikali ni kweli kabisa serikali haiwezi kuwa na mikataba ambayo haina seal hili lilinishangaza sana na kuona kwamba kuna mambo ambayo yanaendeshwa kishkaji kishkaji tu kama pale Kariakoo kwa wauza unga n.k. Hatulali hapa na hii mikataba lazima ifutwe ni batili na wabunge waamke kwenye usingizi wa pono. TZ sio mahali pa kunufaisha mataifa mengine wala sio kwa wageni ambao wanatudharai na kufikiria sisi ni jalala.

Ukipata nafasi endelea kutupatia yanayojiri Bongo. Thanks
 
FMES... pamoja na hilo hebu angalia mstari wa mwisho unavyosema:

provided that the Government shall have made legislative changes to ensure that this provision is applicable under the laws of Tanzania

Unawezaje kuingiza kipengele kwenye mkataba ambapo kisheria hakipo? Yaani tutunge sheria itakayohalalisha kipengele hicho!!
 
4.3 Local Government rates and taxes shall not be:

4.3.1 in excess of those generally applicable on Tanzania, or

4.3.2 based on profit, turnover, sales or output from mining
operations, or

4.3.3 based on the value of land used for the mine, mining
infrastructure or installations,

provided that the aggregate of such local Government rates and
taxes charged shall not exceed United States Dollars Two Hundred
Thousand (US$ 200,000) in any one calendar year.


Katika mkataba mzima so far hakuna mahalai nimezimia kama kwenye hiki kifungu, hebu check this out, hebu naomba wakuu mksome tena hiki kipande halafu mtoe maana zake maana ziko nyingi sana za kutufanya wananchi na serikali yetu kuwa ni majuha!
 
Samahani sikuona kuwa kulikuwa na thread hii. Nilianzisha thread ambayo ninategemea kuanza kuichangia kuhusu mkataba huu kuannzia jumatatu ijayo nikisharudi nyumbani. kwa vile mmeshaanza, basi nitakuja kutoa mchangu hapa hapa.

Usijali nimeunganisha tayari.
 
Sasa kama huu sio uhujumu uchumi ni nini? Huyu waziri siyo tu kwamba anastahili kufukuzwa kazi. Anastahili kufungwa jela.

Pia anastahili achapwe viboko 100 hadharani akiwa makalio matupu!
 
JE NA MKATABA HUU muungwana atasema alidanganywa?
wana wa watanzania naendelea kuwaomba sana msiwakumbatie hawa wanyang'anyi,najua wanapita kujisafisha kwa pesa ya kodi zetu..muwazomea na kuwakataa kwa moyo mmoja,
naendelea kuwasihi tena na tena,kila mtu na mwenzake,msiwaombee hawa wasanii wa boys 2 MEN-Wachukieni na mashabiki wao..
wazee na wajukuu wa jambo,mapambano ya kifkra ndio yameanza..
leteni memorandum na AOA ya TANZANIA EXPLORERS LTD
 
Nasikia kizungu zungu kwenye huu Wizi aliosaini Karamagi kwenye casino london.Ngoja niangalie kwanza wanaJF mnasemaje
 
Wanachama wenzangu wa JF,
Naanza kwa kuwapa hongera kemkem kutokana na jinsi mnavyomwaga ukweli wenye kuuma pande zote. Baada ya hapo nawaombeni samahani sana kwa kutoweka bila kuaga; wakati mwingine mihangaiko ya maisha haitabiriki. Nimefurahi kukuta mijadala kemkem kibao inaendelea hapa kijiweni. Bado nipo hapa Dar nilipokuja kwa muda mfupi kwa mambo ya kifamilia, jana nilipata bahati ya kukata kinywaji na rafiki zangu wachache ambao wana nyadhifa kubwa serikalini. Nilishangaa sana kugundua kuwa wanaiogopa sana Jambo Forum to death. Wanasema inatoa vijembe vikali ambavyo wakati mwingine huwa vinahusu mambo waliyoshiriki katika kufanyia maamuzi. Nilichojifunza ni kuwa vijembe vya hapa kumbe kweli vinawafundisha adabu baadhi ya vihgogo wetu.

Kwa hapa mtaani nimefanikiwa kupata nakala ya mkataba wa Buzwagi, na kweli kile ni kichekesho kabisa wala siyo mkataba unaweza kuwa umeingiwa na serikali ya watu wenye akili zao. Inawezekana mmekisha ujadili mkataba huo hapa , lakini nitarudi na uchambuzi wangu kipengele kwa kipengele kupitia articles zote 18 ambazo nyingi zinaweka masharti ya kuinufaisha kampuni tu wala wala hakuna masharti ya kuinufaisha serikali. La muhimu ni kutambua kuwa mkataba ule siyo binding kabisa na unaweza kupingwa mahakamani kwa vile hauna "Seal ya Serikali ya Tanzania," na wala hakuna shahidi independent aliyethibistha kuwa ulisainiwa kihalali bila kulazimishana kwa vitisho. Mtu yeyote anaweza kuandika document kama hiyo na kudai kuwa ni mkataba wa serikali.

Asante Kichuguu,
Haya maneno yamenifariji, siyo siri nilipo sikia majibu ya kwamba uwezekano wa kujinasua katika mkenge huu ni mdogo sana niliumia sana! Hayo maneno yako yamenipa matumaini mapya. Jamani wenye kuelewa zaidi tufanyeje ili kuupiga chini huu mkataba tafadhari saidia mawazo. Naamini ambao mapigo ya moyo wao yameongezeka ghafla kwa kuusoma huu mkataba na kutoamini macho yao hasa baada ya kuambiwa huu ndio ulioboreshwa tupo wengi!
 
Hayo mambo ya empowerment fund hata kwenye uanzishwaji wa PSRC wakati wa privatisation wa SUs yalikuwapo. Nia ya fund hiyo ilikuwa ni kuwawezesha wazawa (walalahoi?) kuyanunua mashirika yaliyokuwa yakiuzwa.

Kisichoeleweka ni kuwa hiyo fund ilianzishwa au la; na kama ilianzishwa, ni kiasi gani kilikusanywa; na ni wazawa wangapi walifaidika nazo; majina yao ni kina nani na vilevile, kiasi ambacho hakijatumika na kitatumika vipi.

Nadhani ni uvivu wa kusoma na kufuatilia mambo ya nchi kwa undani na kwa uzalendo, kulisema taifa lako kwa mabaya sio jambo la kusheherekea, mbona Bush anaboronga vita ya Iraq lakini wananchi wake wako naye karibu;
Kwa mawazo yangu mimi nisiyesoma sheria kujadili taarifa ambayo taifa letu limesaini kwamba itakuwa ya siri sio jambo la kujivunia sana, ingawa sisemi kilichomo ndani ni kizuri ama la kwa kuwa sio mtaalamu wa madini wala wa sheria.

Kwa majibu ya swali lako yako hapa http://www.parliament.go.tz/Polis/PAMS/Docs/16-2004.pdf

Nenda moja kwa moja PART IV: Section 16; Title "Establishment of the National Economic Epowerment Fund

Tujaribu kuwa wazalendo kwa kutendea taifa letu haki kwa kusema mambo kwa research zaidi, kumbuka munayoandika hapa yatakaa kwenye computer za watu wengi wa maitaifa mengi, miaka na miaka... let no think you are chating with kilitime and it will end there!

Hili jambo nalifananisha na kukata tawi ulilokalia!!! Sisi ni Watanzania na Tutaendea kuwa watanzania aidha chini ya waziri X, au Waziri Y, au Waziri Z, au etc... so let be fair to our nation,
 
I know this is alil off topic but>>>>

Can U call our president, PM and ministers tourists because they don't stay ofisini???

"""""" Minister of State in the President’s Office –Public Service Management, Hawa Ghasia, issued the warning here on Tuesday.........

...........She likened some officials with tourists as they are always out of office attending seminars and workshops that do not help their performance, noting that such officials would want everything to wait until they are through with the seminars. ""

The irony as this was said while she was out for 7 days for no reason.

http://www.dailynews-tsn.com/page.php?id=8936
 
Nadhani ni uvivu wa kusoma na kufuatilia mambo ya nchi kwa undani na kwa uzalendo, kulisema taifa lako kwa mabaya sio jambo la kusheherekea, mbona Busha anaboronga vita ya Iraq lakini wananchi wake wako naye karibu;

Mkuu approval rating ya Bush ni less than 30% so approval ipi unaongelea???

Why did the democratic party capture both senate & House in 2006?? thought so
 
Nadhani ni uvivu wa kusoma na kufuatilia mambo ya nchi kwa undani na kwa uzalendo, kulisema taifa lako kwa mabaya sio jambo la kusheherekea, mbona Busha anaboronga vita ya Iraq lakini wananchi wake wako naye karibu;

Opinion poll iliyotoka leo inaonyesha less than 30% ya American wanasupport kazi ya Bush! sijui wamarekani gani hao unawasema wewe?

Tujaribu kuwa wazalendo kwa kutendea taifa letu haki kwa kusema mambo kwa research zaidi,

Uzalendo ni kutoingiza Taifa kwenye mikataba mibovu in the first place na wala sio kukaa kimya eti kulinda serikali na image ya taifa!

kumbuka munayoandika hapa yatakaa kwenye computer za watu wengi wa maitaifa mengi, miaka na miaka... let no think you are chating with kilitime and it will end there!

Hili jambo nalifananisha na kukata tawi ulilokalia!!! Sisi ni Watanzania na Tutaendea kuwa watanzania aidha chini ya waziri X, au Waziri Y, au Waziri Z, au etc... so let be fair to our nation,


Kazi unayo mwaka huu..... mkataba huu utaifilisi nchi mali zake na wala sio issue ya kilitime... wewe ni sehemu tu ya mamilioni ya watanzania wanaoumia kila siku kutokana na vitendo vya serikali hii... ikiwemo hii mikataba mibovu!
 
Minister lashes out at bureaucracy in local govts
RICHARD MWANGULUBE in Arusha
Daily News; Thursday,October 04, 2007 @00:03


She likened some officials with tourists as they are always out of office attending seminars and workshops that do not help their performance,

Okay, exactly anmuongelea nani, wakati yeye mwenyewe hayupo ofisini kwa siku saba akizunguka zunguka tu, kwa nini asiongelee orodha ya wabadhirifu basi kama kweli amechoshwa na ubadhirifu wa hela za walipa kodi?
 
Dah!
Kwa Mujibu wa maelezo ya kichuguu kwamba Mkataba huo tunaouona Hauna seal ya serikali. hivi serikali wakija na hoja kwamba huo mkataba tuliouona ni feki, ni uzushi wa wapinzani,na kwamba yeyote anayetaka kuona mkataba halali afuate taratibu zilizowekwa ataupata.
Hivi hii si inaweza kubadirisha upepo wa siasa kwa sasa?
 
Back
Top Bottom