Sn2139
JF-Expert Member
- Apr 9, 2010
- 834
- 251
"Off the cuff" umejuaje? Umejuaje kwamba hotuba ya Nyerere aliitoa "off the cuff"? Ndo maana nakwambia unajivisha mamlaka ya usemaji wa ofisi ya Marehemu Mwalimu Nyerere. Umejuaje Nyerere alibwabwaja tu "off the cuff"?
Aidha, wanaotoa hati ya hotuba rasmi sio walioisikia uwanjani au kwenye radio kama wewe na mimi. Bali ofisi ya mtoa hotuba, tena mara nyingi kabla ya tukio. Wewe unajivika kilemba ukoka kama mamlaka ya nyaraka za rais mstaafu.
Kizazi kipya unachosema unakiandikia historia watakaposoma hayo yako na wakute rekodi za wengine zikionyesha kuwa Mwanakijiji hakuwa mamlaka ya alichoandika na kukisema Julius Nyerere kwa sababu anaongeza chumvi zake.
Hakuna sababu ya kulaumiana. Huyo aliyetoa hii hotuba ni bora zaidi kuliko kutokuwa nayo. Hii iliyohaliliwa bado ina nguvu ya kuamsha hamasa ya ukombozi mpya wa Tanzania yetu. Kama wewe unayo isiyohaliliwa weka hapa tusome. Kama kuna neno limeongezwa hapo ambalo limepotosha mawazo ya Nyerere liseme tukusikie na sisi tutakuunga mkono ili lirekebishwe.
Mawazo ya Mwalimu bado yana nguvu inayogusa moyo na akili ya kila mtu mwenye moyo wa ufahamu. Wasomi, Wachungaji na Mashe, Wanajeshi na Wafanya biashara, wakulima na wafugaji...wote wameendelea kuguswa na hotuba za Nyerere. Nyerere alikuwa amejitoa mhanga kuongoza nchi hii, alijitoa kutafuta majibu ya matatizo ya nchi yetu. Aliipenda nchi na watu wake wote. Ndio maana tunaomfahamu bado tunamkubali na kumheshimu kama binadamu aliyejitahidi kutumikia watu wake kwa nguvu zake zote.
Sasa ninaomba tuwe tunatoa hitimisho la mambo tunayojadili ili kama siku ingine yakirudi kujadiliwa, yaanzie kwenye hitimisho. Kwa mfano Je tunapokuwa na raisi aliyenunuliwa na anatumia ikulu kulipa fadhira au madeni ya wafadhiri wake je tufanyeje? Je tukubali kutembea naye kama mkristo anavyotembea na msalaba shingoni? Mfano mwingine ni mashirika ya umma yanayofanya vizuri kisha yakauzwa au yakaandaliwa mazingira ya kuuzwa, je tunawezaje kurekebisha tatizo hio? Nk.