JF Exclusive: Hotuba ya Nyerere 1995 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

JF Exclusive: Hotuba ya Nyerere 1995

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Mzee Mwanakijiji, Apr 29, 2010.

 1. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #1
  Apr 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  [​IMG]
  Mojawapo ya hotuba muhimu sana za Baba wa Taifa ni ile iliyotolewa siku ya Mei Mosi 1995 kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine mjini Mbeya. Ni hotuba ambayo iligusa mambo mengi na kwa ukaribu naweza kusema ni mwendelezo wa fikra zake kuhusu Tanzania na uongozi wetu ambazo alizianza karibu mwaka mmoja kabla yake baada ya kuchapisha kijitabu cha "UONGOZI WETU NA HATIMA YA TANZANIA".


  Ifuatayo ni hotuba muhimu ambayo kila Mtanzania anapaswa kuisoma kwani ni mojawapo ya lulu za fikra zinazotudokeza taifa letu tumefikaje hapa na ni miongoni mwa hotuba ambazo Nyerere hakusita kukubali kuwa kuna mahali chini ya uongozi wake walikosea (kinyume na imani ya watu kwamba Nyerere hajawahi kukubali makosa).

  Hotuba hii vile vile ni muhimu sana wakati huu ambapo Wafanyakazi nchini wanajiandaa kugoma na inaweza kutumika kabisa kama kichocheo cha mgomo huo. Ikumbukwe kuwa ilikuwa ni mara ya kwanza vyama vya wafanyakazi vilimkaribisha mtu ambaye si Rais kuwa mgeni rasmi mzungumzaji katika sherehe hizo.

  Sehemu ya sauti imenisumbua kidogo kwani original file yangu nilishadelete inabidi nihamishe kutoka kwenye CD niliyotengeneza 2007!! so for now enjoy hii ya maandishi.

  Nimegawa katika sehemu sita kutokana na maudhui yake.

  Sura ya 1 - Inahusu wafanyakazi zaidi na haja ya kushikimana kudai haki zao. Ikumbukwe kuwa 1994 wafanyakazi waligoma na wakati ule walimuomba Mwalimu awe mgeni rasmi akawakatalia lakini 1995 alikubali.

  Sura ya 2 - Anazungumzia hali tulipotoka, hasa katika masuala ya kiuchumi ili kuweza kuelewa tulipofika wakati ule. Kauli mbiu yake ni "Tumetoka wapi, tupo wapi, na tunakwenda wapi"? Ndio mbiu anayoirudia katika hotuba nzima.

  Sura ya 3 - Baadhi ya Matunda ya Azimio la Arusha. Hapa anajaribu kuelezea baadhi ya matunda ya Azimio la Arusha hasa akijaribu kuonesha kuwa maamuzi ya Zanzibar yaliyobadili Azimio la Arusha yalibadili kitu cha msingi sana.

  Sura ya 4 - Makosa ya Ubinafsishaji. Nyerere anajenga hoja ya msingi kuwa ubinafsishaji uliokuwa umeanza kufanywa ulikuwa kinyume na sera ya CCM.

  Sura ya 5 - Tunakwenda wapi na sifa za viongozi tunaowataka. Anapofika hapa Nyerere anaendelea mbele kidogo kutokana na kile alichokisema Kilimanjaro alipotoa orodha ya sifa za viongozi tunaowataka. Kwa mwaka huu wa uchaguzi, sehemu hii ni muhimu kuisoma kabla hatujaamua kumuunga mkono mgombea yoyote wa nafasi yoyote.

  Sura ya 6 - Sehemu hii ya mwisho Mwalimu anafanya utetezi wake wa kifalsafa wa wagombea binafsi na anaelezea kwanini serikali ilifanya makosa kufuta haki ya mwananchi kuchaguliwa kwa sababu inakera. Ni muhimu tunapoelekea kusikia uamuzi wa mahakama ya Rufaa kuhusu suala la mgombea binafsi.

  HOTUBA KAMILI
  - Mwishoni hapo nimeweka hotuba kamili. Kwa hiyo una uchaguzi wa kuchukua sehemu sehemu au kudownload hotuba kamili ilivyo.
   

  Attached Files:

 2. Edson

  Edson JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Mar 7, 2009
  Messages: 9,202
  Likes Received: 719
  Trophy Points: 280
  poa mzee we ishushe tu
   
 3. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Baada ya miaka 15 hutba hiyo inabakia kuwa ni valid na relevant. Mze alikuwa anaona mbali sana ila sisi hatukumuelewa tumekuja muelewa baadaye sana tena sio kama kama alivyotaka. Eti ndio tunashituka saa hizi, mungu tusaidie.
   
 4. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #4
  Apr 29, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Huyu mzee alikuwa ananifurahisha sana na hotuba zake. Nilikuwa sikosi kuzisikiliza, alibarikiwa kwa kuhutubia.
  ukizisikiliza utacheka, utatabasamu, utajisikia mtanzania.................... hasa kwa sisi wazalendo. He was a MAN............ Kwa kweli I miss him.. RIP
   
 5. Ngambo Ngali

  Ngambo Ngali JF-Expert Member

  #5
  Apr 29, 2010
  Joined: Apr 17, 2009
  Messages: 3,194
  Likes Received: 134
  Trophy Points: 160
  Fixed Point, Tunafanye nini ili kumuenzi mzee wetu, yote aliyosimamia hayapo, wakulima wa mahindi sumbawanga wanaibiwa vocha za pembejeo, wagonjwa wanaombwa rushwa na dawa za bure wanauziwa, shuleni hamna madaftari, watoto wetu hawapewi mikopo ya kusoma vyuo vya juu, reli haifanyi kazi badala yake mizigo inasafirishwa kwa malori, viwanda vya pamba kwisha vyote. Kulikuwa na kiwanda cha juice mkulima wa matunda alikuwa na sehemu ya kuyauza mazao yake kimeuzwa nacho. Kusikiliza hotuba na kuisoma tu hakusaidii kitu.
   
 6. Ben Saanane

  Ben Saanane Verified User

  #6
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 18, 2007
  Messages: 14,603
  Likes Received: 3,692
  Trophy Points: 280
  Ukimsikiliza mwlimu utaona alikua kiongozi mwenye vision na pi alikua mbele kuliko viongozi wengi
   
 7. K

  Kifimbocheza JF-Expert Member

  #7
  Apr 29, 2010
  Joined: Aug 7, 2008
  Messages: 496
  Likes Received: 92
  Trophy Points: 45
  Mwanakijiji

  Tafadhali ikiwezekana iweke ili tuweze kuishikia kabisa na si kuisoma tu

  Asante
   
 8. Fixed Point

  Fixed Point JF Bronze Member

  #8
  Apr 29, 2010
  Joined: Sep 30, 2009
  Messages: 11,321
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 145
  Kwa kweli anatakiwa kuenziwa kipekee kwa mengi aliyotufanyia. cha ajabu tunaishia kuweka hotuba zake wiki ya kuadhimisha siku yake, vipi kuhusu yale aliyoyasema?
   
 9. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #9
  Apr 29, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  FP, wengine tunayasimamia hayo na hatuoni aibu kuhusishwa naye; tatizo ni watawala wenu ambao wakimnukuu Nyerere inakuwa ni katika "kudumisha amani, umoja, upendo na mshikamano"!
   
 10. b

  buckreef JF-Expert Member

  #10
  Apr 29, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Hayo ya Mwalimu mtayasema mpaka lini? Lini mtaanza kuyatekeleza kwa vitendo?

  Watanzania kila mtu anajifanya anamuunga mkono Nyerere lakini tukipewa hata wajibu mdogo tu, tunashindwa vibaya.

  Badala ya kuimba imba tu Mwalimu kila siku, tuonyeshe angalau tunafanya nini kuisaidia Tanzania na wale maskini huko vijijini?

  Ndio hayo hayo ya CCJ kwenda kulia kwenye kaburi la Mwalimu.
   
 11. F

  Froida JF-Expert Member

  #11
  Apr 29, 2010
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 7,900
  Likes Received: 1,328
  Trophy Points: 280
  Bado hatujapata mwingine kama yeye japo naamini yupo atakayetutoa kwenye lindi la uozo huu
   
 12. Luteni

  Luteni JF-Expert Member

  #12
  Apr 29, 2010
  Joined: Jan 9, 2010
  Messages: 2,274
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  Kuonyesha una-support mawazo ya Nyerere si lazima uitishe mkutano pale jangwani hata kuweka hotuba zake kama hivi na kuwakumbusha watu ni tija tosha kwa wengine panapopungua unaweza kuongezea kwa nafasi yako.
   
 13. m

  magee Senior Member

  #13
  Apr 29, 2010
  Joined: Jun 3, 2009
  Messages: 126
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  ni kweli......ila je niwangapi wanaaccess hapa???na ukishawakumbusha then???its high time kuweka mikutano jangwani....kuwagusa wengi,its high time tuache kusurpport mawazo kwa kutingisha vichwa na kiutikia 'yes....the guy was genius' tuanze kupambana na kujiunga kuelekea ulimwengu wa kiukweli na vitendo.
   
 14. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #14
  Apr 29, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  Unajua muungwana alitaka kujifananisha na JK halisi kwa kujiiita JK lakini ngoma ngumu pale.
  Nyerere bado ni genius leader ever lived.
  Hotuba zake nyingi ukisikiliza unaamini kuwa jamaa alikuwa ni nabii wa kweli

  Mkuu MM nasubiri hiyo hotuba shekhe
   
 15. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #15
  Apr 29, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 0
  Naisubiri kwa hamu.Shukrani Mwanakijiji
   
 16. Suki

  Suki JF-Expert Member

  #16
  Apr 30, 2010
  Joined: Nov 20, 2007
  Messages: 373
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Please do.
  Labda itanipa sababu ya kumkubali.
   
 17. firstcollina

  firstcollina JF-Expert Member

  #17
  Apr 30, 2010
  Joined: Aug 8, 2009
  Messages: 349
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Watafanya nini na wakati hawana jipya? Ile njia ya Upendo Amani na Utulivu ndio imekuwa mkombozi na kiungo kikubwa baina yao na Nyerere. tena hutumiwa kama kitisho kwa walio wengi walio eti kufanya otherwise ni kuvuruga amani na kuleta maafa.

  Nadhani watu hapo May 01 watamuenzi kwa style ya aina yake, nyie ngojeni muone.
   
 18. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #18
  Apr 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  sehemu ya hotuba yake.. inakuja..

  Na anasema tena:

   
 19. nguvumali

  nguvumali JF Bronze Member

  #19
  Apr 30, 2010
  Joined: Sep 3, 2009
  Messages: 4,864
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  hili Genge la watawala lililopo pale Ikulu, Julius Nyerere alilikataa kabisa, walikua na uchu tangu mwanzo , na hakika Tanzania imewashuhudia walivyowalafi, imeshuhudia unabii wa babu ukitimia kwamba mtu mwadilifu hawezi kupakimbilia Ikulu, Ikulu ni Mzigo....walitaka kwenda Ikulu kwa faida yao kama JK Nyerere wa Butiama anavyosema..."Mtu anayetaka kwenda Ikulu kutaka faida ye yote Ikulu pale hatufai hata kidogo" wamekuja na magenge yao kama wacheza disco wameila nnchi yetu, wanaila na wanarudi tena kutuomba ridhaa ili wakamalizie kula.
   
 20. Mzee Mwanakijiji

  Mzee Mwanakijiji Platinum Member

  #20
  Apr 30, 2010
  Joined: Mar 10, 2006
  Messages: 31,361
  Likes Received: 6,380
  Trophy Points: 280
  Haya wananchi iko hewani!!! Angalia posti ya kwanza.
   
Loading...