Twilumba
Platinum Member
- Dec 5, 2010
- 13,472
- 16,177
Miaka ya 90's EU na IMF waliupinga sana mkataba wa IPTL wakisema wazi ni mzigo usio wa lazima kwa uchumi wetu mdogo.
Canada ikajitolea gharama dola mil 200 za mradi wa Songas badala ya iptl,wakubwa bado wakang'ang'ana na iptl,yaani mtu anakataa hadi msaada na kulazimisha mkataba ghali kama iptl!
Walipobanwa sana,wakasema miradi yote miwili songas na iptl iende pamoja!
Washauri wa Tanesco wakati huo,Hunton and Williams wakaeleza wazi kuwa mkataba wa iptl haufai kwa kuwa;
-ni wa kipindi kirefu wakati tatizo lilikuwa la kipindi kifupi.
-ulikuwa na gharama kubwa zisizo na sababu.
-ulizidi mahitaji ya umeme na hivyo watumiaji na walipa kodi wangelipia gharama kubwa kuzalisha umeme wasioutumia.
-mkataba uliwapendelea mno iptl
-hakukuwa na ukomo wa muda wa kukamilisha ujenzi hivyo Tanesco kulipishwa gharama kubwa kutokana na ujenzi kuwa prolonged.Gharama zilipaswa kujadiliwa baada ya ujenzi kukamilika.
Nikipitia ushauri huu wa Hunton and Williams,na kwa kuzingatia mazingira ya kifisadi ya nchi yetu,naanza kupatwa na mashaka kama kweli matatizo ya umeme tuliyo nayo yalipaswa kuwa makubwa hivi.
Napata mashaka hata na data tunazopewa kama zina ukweli,hasa kwenye ukubwa wa tatizo,je,ni kweli mahitaji ya umeme au consuption ya umeme ya gridi nzima tunayoambiwa ni ya kweli au imezidishwa ili kuonyesha demand kubwa na hivyo kuhalalisha supply kubwa ambayo mafisadi ndimo wamewekeza?
Napata mashaka kuwa huenda tunao watu wenye ujasiri wa kufikiria kuhujumu mitambo na shirika la Tanesco ili lipate shida ambayo haikuwepo au ilikuwa ndogo na kulikuwa na alternative za kuitatua zenye gharama nafuu,lakini kwa kuwa hazikutoa maslahi kwa certain individuals,zikapigwa chini,tatizo likakuzwa na kuhakikisha linakuwa la muda mrefu ili watu wapige hela,na hivi ndivyo mashirika yetu mengi ya umma yalikufa,hata TTCL nakumbuka ilikuwa inajiendesha kwa faida kubwa,ghafla ikahujumiwa,tukaambiwa inajiendesha kwa hasara,ibinafsishwe.
Wakuu mnaukumbuka ule mgomo wa staff wa Tanesco wakipinga ubinafsishaji na kusema madai ya serikali kuwa Tanesco inajiendesha kwa hasara yalikuwa uongo mtupu?wakaishia kuzunguukwa na FFU!
Mnakumbuka net group solution ilivyokuja kuivuruga Tanesco zaidi?
1997 hazina ilikataa kutoa ushuru wa mafuta ya kuendesha mitambo ya Tanesco,lakini hazina hiyo hiyo ikatoa msamaha kwa wafanyabiashara waagizaji mafuta nje,matokeo yake mgao wa umeme ukafuatia baada ya Tanesco kushindwa gharama za ununuzi mafuta mazito kwa ajili ya mitambo ya iptl.
Hizi zote ni coicidence?
Inaogopesha sana kugundua tunao watz wenzetu wenye roho mbaya hivi,inatisha na kuondoa kuaminiana,na kutoaminiana kukikomaa,huzaa matabaka na makundi,mwishowe civil wars,kila mtu akitaka achukue chake.
Bunge hili litambue Tanzania kwanza,kabla ya vyama na maslahi binafsi.
Shughulikieni hao wezi bila huruma.
juve2012 Very good analysis. Jf ni hazina!
Last edited by a moderator: