JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

JF Exclusive: CAG Report on IPTL/Tegeta Escrow Account

Hata mie napata shida zinapigwa kelele nyingi sana lakini ukisoma document hizi sioni shida hata page 59 inayosemwa imeondolewa tumeiona wala haina majina ya watu nchi hii umbea umezidi.
Kama shilingi zinapata tabu itakuwa wewe senti!!!!!
 
Sasa wewe unashangaa wakati kamati yote PAC wanayo hiyo ripoti, zipo, lakini hazina mshiko ndiyo maana huzioni humu.

te!



Wakuu,

Dodoma kumekucha. Naomba kwa ufupi niwafahamishe kinachojiri maeneo haya (nimepiga kambi huku).

MOSI:
Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa anataka PM Pinda atoke kwa sababu mbili, moja ili njia ya kupata Urais iwe nyeupe lakini pili ili asiwe PM peke yake aliyewahi kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa. Watu wake Edward wanahangaika sana kushawishi watu ili azma hii itimie.

PILI:
Membe naye anataka PM ang'oke kwa sababu kuu mbili, moja ili njia ya Urais iwe rahisi lakini pia kwa matumaini kwamba anaweza kupata yeye uPM japo kwa muda tu ili nyota ing'are zaidi.

TATU:
Wassira naye anatakaPinda aanguke ili njia iwe rahisi lakini pia kwa matumaini kwamba anaweza kupata yeye uPM.
Mwandosya naye anataka PM adondoke kwa matumaini ya kupata uPM kutokana na utu uzima.

Sitta naye vivyo hivyo.

NNE:
Mawaziri walioondolewa huko nyuma wakiongozwa na Kagasheki, Nchimbi na Maige nao wanaomba Serikali idondoke kwa sababu wanaamini Pinda aliwatosa ili apone yeye na sasa wanataka na yeye awajibike kwa udhaifu wake. Yupo mtu kama Mwigulu ambaye anautaka Uwaziri kamili kwa udi na uvumba na anataka Serikali ianguke ili Baraza la Mawaziri lisukwe upya awe Waziri kamili.
 
..... tara tara tunaanza kufunuliwa !!!

WAANZE HUKO KUCHAPA LAPA !!!
 
te!



Wakuu,

Dodoma kumekucha. Naomba kwa ufupi niwafahamishe kinachojiri maeneo haya (nimepiga kambi huku).

MOSI:
Waziri Mkuu aliyejiuzulu kwa kashfa ya Richmond, Edward Lowassa anataka PM Pinda atoke kwa sababu mbili, moja ili njia ya kupata Urais iwe nyeupe lakini pili ili asiwe PM peke yake aliyewahi kujiuzulu kwa tuhuma za rushwa. Watu wake Edward wanahangaika sana kushawishi watu ili azma hii itimie.

PILI:
Membe naye anataka PM ang'oke kwa sababu kuu mbili, moja ili njia ya Urais iwe rahisi lakini pia kwa matumaini kwamba anaweza kupata yeye uPM japo kwa muda tu ili nyota ing'are zaidi.

TATU:
Wassira naye anatakaPinda aanguke ili njia iwe rahisi lakini pia kwa matumaini kwamba anaweza kupata yeye uPM.
Mwandosya naye anataka PM adondoke kwa matumaini ya kupata uPM kutokana na utu uzima.

Sitta naye vivyo hivyo.

NNE:
Mawaziri walioondolewa huko nyuma wakiongozwa na Kagasheki, Nchimbi na Maige nao wanaomba Serikali idondoke kwa sababu wanaamini Pinda aliwatosa ili apone yeye na sasa wanataka na yeye awajibike kwa udhaifu wake. Yupo mtu kama Mwigulu ambaye anautaka Uwaziri kamili kwa udi na uvumba na anataka Serikali ianguke ili Baraza la Mawaziri lisukwe upya awe Waziri kamili.

Umesahau kimoja muhimu sana, UKAWA wanataka CCM ingo'ke watawale wao.
 
Fanya kazi sasa acha malumbano tu toka saa 9 usiku unawaingizia pesa (internet charges) tu watu.

Jenga uchumi wako macho kope weee.


Naona sasa hoja zimekuishia unaanza kuhororoja na kubwabwaja.

Subiri ripoti ya Zitto Kabwe, Mwenyekiti wa Kamati ya PAC bungeni, kupitia tiketi ya chadema (au mahakama?) aiwasilishe, tuone mbichi na mbivu.

Au unasemaje?
 
..Labda tuwajibu wale wanaosema kuwa hawaoni kitu kwenye attachments za invisible.....

..kwa wanaofatilia kwa makini sakata hili watakua wamebaini kuwa hawa PAP waliolipwa pesa za escrow tayari si wamiliki halali wa IPTL bali ni matapeli...

..Ni matapeli kwa kuwa tayari wamegundulika kuwa wamefoji hati miliki ya 70% share za mechmar ili waweze kuchota hela za escrow...Wamefoji hatimiliki hiyo kwa kuonyesha TRA kuwa eti wamenunua 70% ya share za mechmar (aliyekua mmiliki halali) kwa sh. mil.6 tu toka kwa piperlink.....yaani sh.mil.6 kununua 70% ya share zote za IPTL(pamoja na mitambo yote!!)..

.Piperlink ni kampuni iliyodai kukabidhiwa jukumu la muflisi wa mechmar...Hawa piperlink nao hawana hti miliki ya share za mechmar kwani walinyang'anywa miliki hiyo kwenye kesi kule Virgin islands baada ya kugundulika kuwa walitaka kumiliki share za mechmar kitapeli.....na hivyo mahakama ikaamuru kuwa ati miliki hiyo wapewe SCBHK waliokuwa wanawakopesha hela IPTL wakati huo.....

..that said..kwa kwa kuwa imethibitika kuwa PAP si wamiliki halali wa IPTL....maana hata hizo 30% ya share walizowalipa VIP(kina James Rugemarila)zimetokana na pesa walizolipwa na BoT baada ya pesa za escrow kukwapuliwa nao...


..Sasa basi..hata nyaraka PAP walizosainishana na serikali(GoT)...yaani ile agreement ya release of funds na pia ile indemnity deed (kinga ya madai)..zoote hizi zinakua batili automatically na hazina nguvu ya kisheria tena....maana hawa PAP si wamiliki halali wa IPTL...na kwa mana hiyo hata makubaliano yao na serikali yanakosa uhalali wa kisheria automatically..

..that said...ile wanayodai ni kinga kwa serikali (indemnity)haitakua na nguvu ya kisheria panapo madai .....maana aliyesaini deed(yaani PAP)tayari kagundulika ni tapeli.....sasa umeona wapi tapeli/mwizi anatoa kinga ya kisheria kwa anaemtapeli????...kama imefika mahali watu wanasema hawa PAP wakamatwe na mitambo itaifishwe....watapataje hawa nguvu ya kisheria kwa madai kwa serikali??

...that said...kutokana na yote hapo juu..tayari SCBHK(kupitia wanasheria wao) wameshawaandikia tanesco wakiwapa siku 30 wawe wamerudisha pesa yote kwenye escrow account..maana wamegundua kuwa tanesco wamevunja makubaliano ya mkataba wa awali walipofungua escrow account...kwamba tanescow wamekubali pesa ya escrow kulipwa kwa third party (PAP)ambae hatambuliki kwenye mkataba wa awali wa ufunguzi wa acc. hiyo...


....Angalizo..... kuna watu kama Muhongo na Maswi...wamekua wanabeza ushiriki wa SCBHK kwenye sakata hili ....huku wakisahau kuwa hawa SCBHK ndio wamepelekana na tanesco hadi Mahakama ya kimataifa kuhusu tarrifs za umeme wa IPTL...leo eti kina Maswi wanasema hawawatambui???haya ni maajabu mengine ya watendaji hawa wa utawala huu....

.....Labda niwahoji wanaowatetea hawa PAP....kwamba PAP walikuja TZ na mtaji kiasi gani ili wainunue IPTL iliyokuwa na matatizo??mana tunaambiwa eti hawa PAP ni wawekezaji...mtuambie je walikuja TZ na mtaji kiasi gani ili kununua hisa zote za IPTL iliyokuwa na mgogoro???


.jibu hamtakua nalo aslani....maana PAP hawakuja na mtaji TZ..bali walipanga wapige hela za escrow ndipo wazitumie kununua hisa za IPTL...na wamefanikiwa kununua 30% ya hisa za kina Rugemarila(VIP) kwa kutumia hela ya escrow waliyolipwa na BoT. ...Huu ni utapeli wa kiwango cha juu..


....PAP wameshindwa kuzipata kihalali 70% share za mechmar....kwa kuwa walikosa hati miliki halisi....ikabidi wafanye forgery ili wachote hela BoT....napo wakafanikiwa....Lakini sasa wamebambwa...


,....Tutafakari...huu mchezo waliofanya PAP ni kama ilivyokua kwa Richmond..methodology za wizi wao hazitofautiani sana...
 
Standard Chartered Bank lazima wadai pesa zao...ndio maana waingereza wamegoma kutoa support ya budget
 
Hao mechmar walikuwa wapi hadi mtambo ukachukuliwa na paperlink ama PAP?.ndo kusema hawakua hata na watchman wa kuangalia mtambo wao?.
sisi tunachotaka kujua pesa za escrow ni za iptl ama za umma na kama ni za umma zimefikaje escrow kwani kama kulikua na matatizo ya overcharging kwanini tanesco wakaendelea kulundika pesa escrow.
pia kingine inasemwa pesa zote za escrow bila kuacha hata senti ni za umma,sasa hapa zile za halali kuilipa iptl ziliwekwa katika mfuko upi?na je zililipwa lini?
 
daah haatari sana aisee halafu bado unang'an'ania kubakia madarakani?hii taarifa inabidi hata mtu mmoja ajinyonge
 
Hatareeee, ila ngoja tusubiri siku ya kusomwa kwa ripoti nzima, hapa bado hatujaelewa vizuri.
 
Umesahau kimoja muhimu sana, UKAWA wanataka CCM ingo'ke watawale wao.

No CCM wanataka watawale milele kwa vile wamegundua kuwa Watanzania ni mazuzu ............................!!! Hili ni Upepo tu, utapita....................!!
 
Ripoti ya CAG ya IPTL imevuja. Sasa swali la kujiuliza ni kuwa hii ni ripoti halisi ya CAG au ni ripoti feki ambayo inadaiwa imechakachuliwa?

Ripoti inapatikana hapa na unaweza kuidownload au kuiprint moja kwa moja:

https://drive.google.com/file/d/0B1VlvdgNu6ibVEtHNmtMZTEtRGM/view

Mkuu asante kwa hiki ulichotubandikia lakini kina mapungufu imeishia kurasa ya 56 na hakuna kurasa za 57-59 ambazo ndio tunaambiwa zimewekwa yale majina ya waliojichotea fedha hizo kwa hiyo kama una uwezo wa kupata hizo kurasa tubandikie.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom