JF Arusha Wing: Ahsanteni sana...,

JF Arusha Wing: Ahsanteni sana...,

Kitendo kilichofanywa na ndugu zetu wa Arusha Wing, cha kusafiri umbali mrefu kuja kuhani msiba wa mtoto wa KOKUTONA jana ni level ya juu sana ya ubinadamu.

Binafsi nakosa maneno ya kutumia kueleza ukubwa na umuhimu wa kitendo chenu kwa familia ya KOKUTONA sie wana Ta Wing. Tumefarijika sana na tumekubali kwamba nyie ni mfano wa kuigwa ndani na nje ya JF.

MUNGU AWABARIKI SANA!

Babu DC!

Babu Dark City acha kabisa. Unajua babu natafakari upendo huu nabaki kumshangaa Mungu.

Be blessed jamani.
 
Last edited by a moderator:
Aksanteni sana wakuu Dark City na Arabela
Ukweli tulifurahi sana kutimiza ahadi tuliyokuwa tumeiweka mioyoni mwetu, tunajisikia amani sasa!
Safari yetu ilikuwa njema sana na wote tulirudi salama.
Tulijifunza kitu kwenye ile safari!
PakaJimmy jamani, bado sijajua niseme nini

Be blessed sana.
 
Last edited by a moderator:
Nichukue nafasi hii ya pekee kumpongeza sana mdogo wangu Arabela kwa moyo wa upendo wa hali ya juu kwa kusafiri all the way from Tanga kuja kOrogwe kuungana na sisi, lakini pia kwa mchango wa hali na mali alioutoa!
Pokea BIG UPs zangu Arabela!

Nikuibie siri PakaJimmy?
Arabela ni wapekee sana, na ndo maana Arushaone na Filipo km ulivyoona.........Wanajua moyo wa Arabela umejaa mawaridi na majasmine.

Usimwambie mtu........
 
Last edited by a moderator:
Mzee wa Rula kwa kifupi mizimu imekasirika sana kwa kitendo chenu cha kutokulala KOROGWE TANGA.

Rudini fasta mkaitulize.

Mkuu tulia dawa iingie vizuri, fitna zako zote zimeangukia chini ya camera yangu aina ya Samaranda iliyokuwepo eneo la tukio bila wewe kujua. Kuhusu mizimu nampenda sana Yesu kwa hiyo mizimu haileti shida kwa sababu inajua Yesu ni Bwana wa Mwabwana. Ukifika toa taarifa ili file lako tulijadili na tukupe nafasi ya kujitetea tehe tehe.
 
Last edited by a moderator:
PakaJimmy jamani, bado sijajua niseme nini

Be blessed sana.

Jamani yote hii ni katika kuonyesha upendo uliopo ndani ya JF ni tofauti sana na mitandao mingine, na tutazidi kutofautisha mtandao huu na mingine mpaka Mungu atakapotuchukua iwe kwa raha na shida hivyo dada yangu KOKUTONA usiogope.
 
Last edited by a moderator:
Wapendwa Mungu awabariki sana kwa moyo mliouonesha... Pia awazidishie pale mlipopungukiwa...

charminglady dada tushukuru member wote kwa pamoja kutokana na kuitikia wito kwa njia mbali mbali, tupo pamoja na tunasema Amen Mungu awabariki wote hasa waliojitoa kwa hali na mali.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom