JF Arusha Wing: Ahsanteni sana...,

JF Arusha Wing: Ahsanteni sana...,

Binafsi niwashukuru wanaJF wote kwa ujumla kwa wale waliojitolea kuungana na sisi kwa hali na mali. Aidha kuna wale ambao nao walikuwa pamoja nasi kwa maombi tokea tunaondoka hadi tunarudi, kila mara walikuwa wakifuatilia wapi tumefika hadi tunaingia majumbani.

Wote kwa pamoja Mungu awabariki sana.

Pamoja na hayo tunashukuru sana KOKUTONA kwa maandalizi mazuri pamoja na wenzake ambao kwa kweli walijiandaa na ugeni wetu kiasi cha kutosha sana, Mungu awabariki wote.

Mwisho tunamrudishia shukrani Almight God kwa kutupa ulinzi na kukubali dua /zetu/zenu maana bila yeye kukubali dua/maombi yetu/yenu basi naamini tusingekuwa salama.

Mzee wa Rula hakika ujio wenu umekuwa baraka katika familia yetu. Yaani haipiti saa hatujawaongelea. Mmetufundisha mengi ya kujenga. Pia tunafurah kusikia kidogo tulichoandaa mlikipenda. Mungu awabariki sana.TUNAWAPENDA SANA.
 
Last edited by a moderator:
dah! PakaJimmy, na ARUshone you are good people ever.........
huwaga najiuliza watu wa aina yenu bado wpo hapa dunian kweli?? naupenda moyo wenu wa mapenzi mema mema kwa wenzenu na zaid ya yote napenda sana ushirikiano wenu.

i owe you zawadi kwa kweli.

Babu Dark City wewe mie sisemi sana ila tu naomba umwambie Arabela kwamba nampenda sana na nampend zaid kwa moyo wake wa kujitolea. wewe babu salam zako nitazituma kwenye barua nyingine nitakayoituma.

Maneno yako matamu ticha. Thanks kwa faraja yako.
 
Last edited by a moderator:
Dark City
Hakika tu pamoja mwanzo mwisho,Ndg siyo wa kuzaliwa ila kufaana Ndg zanguni! Ni hakika mambo yaliingiliana kwani mngetuona Arusha wing wote hapo Tanga ila kwa kuwa ndiyo hivyo hakika waliofika wamefika kwa niaba ya sisi Wana A town wing.

Pamoja sana na salaam sana CHUAKACHARA popote pale alipo!

Kitendo kilichofanywa na ndugu zetu wa Arusha Wing, cha kusafiri umbali mrefu kuja kuhani msiba wa mtoto wa KOKUTONA jana ni level ya juu sana ya ubinadamu.

Binafsi nakosa maneno ya kutumia kueleza ukubwa na umuhimu wa kitendo chenu kwa familia ya KOKUTONA sie wana Ta Wing. Tumefarijika sana na tumekubali kwamba nyie ni mfano wa kuigwa ndani na nje ya JF.

MUNGU AWABARIKI SANA!

Babu DC!
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom