Jeshi lijitathimini kuhusu uadilifu na uaminifu wake kwa Watanzania wote

Sure, kuna watu wanawatetea bila kujua undani wa hilo jambo!

Hoja zao ni kwamba sijui wamefundishwa kutumia silaha so watajiingiza kwenye uhalifu!
Jeshini sio shuleni kule ni kazi moja.
 
Hilo lakuwahamisha ilikuwa kuwapoteza uelekeo kwasababu JPM alitoa maagizo baada yakukamilika waajiriwe Jeshini moja kwa moja...narudia tena waliowatangulia walipokamilisha mission yao ya ujenzi walianza kutawanywa vikosini nakuamriwa warudi nyumbani JPM ndo aliwarudisha, sasa hivi JPM hayupo nani atawatetea?
Acha wenge la JPM, kumbuka yeye ndo kachelewesha ajira au kuzuia ajira za vijana wengi wa JKT waliokuwa wanajiliwa katika majeshi yetu. Yeye kutambua tu wale waliojenga uzio among many others ni ubaguzi, pili mtoa kibali cha kuajili ni ikulu ambaye alikuwa yeye kama kweli alikuwa na niya ya kuwaajili kwnn hakufanya hivyo tangu alipotoa tamuko miezi 8 imepita. Matamuko mengine yalikuwa siasa na kutaguta cheap popularity.
 
Umesema mwenyewe hapo kuwa hao wa awali kuna njia walitumia wakarejeshwa. Sasa hawa wanaleta migomo jeshini. Hawafai waasi hao
 
Umesema mwenyewe hapo kuwa hao wa awali kuna njia walitumia wakarejeshwa. Sasa hawa wanaleta migomo jeshini. Hawafai waasi hao
Hata hawa kuna sehemu walikanyaga waya vibaya. Ndomaana walikua 2400 ila waliofukuzwa ni 854 pekeyake

Hahahaaa halafu hawa walifurahisha sana kulazimisha kwenda kihangaiko na wakaletewa magari kweli wakapanda kwenda kule

Hawakujua......hawakujua😂😂
 
Hilo lakuwahamisha ilikuwa kuwapoteza uelekeo kwasababu JPM alitoa maagizo baada yakukamilika waajiriwe Jeshini moja kwa moja...narudia tena waliowatangulia walipokamilisha mission yao ya ujenzi walianza kutawanywa vikosini nakuamriwa warudi nyumbani JPM ndo aliwarudisha, sasa hivi JPM hayupo nani atawatetea?
JPM is dead. live with it man. hakunaga orders za rais alifariki. once he is gone he is gone.
Labda mama samia aje atilie mkazo.

lakin hao vijana walikuwa kubadilishiwa eneo la kazi isingetakiwa kuwa nongwa.
wasingegoma.. ila wangetumia utaratib qa kijeshi kufikisha malalamiko yao.
na utaratib uko fair kabisa.
 
Uko kihisia zaidi mzee, wale wamepewa ahadi ya moja kwa moja wakikamilisha mission waajiriwe Jeshini direct sasa labda ndo moja ya maasi kwa Mwendazake
jeshi aliendeshwi kwa ahadi. hapa late pres jpm alikosea sana sana.
kuna utaratib wa kuajiriwa
 
Ndg wanajamvi habari za jumapili.
Niende kwenye mada moja kwa moja, “Jeshi lijitathimini” ndiyo Jeshi letu kwa macho ya nje limejivika vazi nzuri la uaminifu macho pa Watanzania wote lakini kwa ndani linapokuja suala la Ajira ndani ya Jeshi hasa hili tunaloliona la vijana wa JKT siyo Waaminifu kabisa. Wakuu wetu hawa wajitathimini tena kwanini wanazipoka haki za vijana wetu hawa hasa ambao hawana mahala pakuegemea.

Sakata la “Uasi wa Vijana wa JKT”
Jambo hili litazamwe upya na hawa vijana wasaidiwe hata km siyo ndani ya JWTZ lkn wapewe ajira maana hii ilikuwa ahadi ya Rais wa awamu ya tano. Kuna michezo mibaya sana labda kama Rais Samia hajui atadanganywa. Kabla vijana hawa kuna vijana ambao walishiriki shughuli mbalimbali za ujenzi kuanzia ngerengere, Dodoma nk ambao km ilivyo kwa hawa “Waasi”, wao walipewa ahadi nawakatimiziwa lakini haikuwa rahisi.
Ilianza kama ilivyokuwa kwa hawa “waasi” wakarejeshwa vikosini nakupewa Vyeti vyakumaliza mkataba wakatakiwa kuondoka huku wakipewa maagizo kuwa watatafutwa kukiwa na mabadiliko. Vijana wale wakafanya jitihada za kuwasiliana na uongozi lkn wakapewa maagizo kuwa waondoke hatua ya mwisho wakahangaika kupata mawasiliano ya alikuwa Rais Marehemu JPM wakafanikiwa, wakamweleza kuwa tumerudishwa nyumbani, JPM alishangaa kwann warudishwe wakati taarifa aliyonayo wanafanyiwa mchakato wa ajira na ana list amepelekewa? Ndipo alipomwagiza Brigedia Mbuge ampelekea list ya vijana walioshiriki ujenzi kuanzia ukuta wa mererani, Ngerengere na Dodoma, uzuri Mbuge alishtuka akapeleka list iliyohalisi ndipo JPM akagundua kuna waliochomekwa. Akaagizwa vijana waliositishiwa mkataba warejeshwe na hatimaye sasa ni Wanajeshi.

Natoa hii historia ili kwa wale ambao hawaelewi figisu zilipopo Jeshini linapokuja suala la Ajira watambue kuwa vijana wale walijua wazi kuwa wanaondolewa kijanja ili wengine wachomekewe. Rais wangu Samia wangalie vizuri hao wakuu na uchukue hatua vijana hawa wanapigania haki zao walioahidiwa na Rais JPM. Pili, Jeshi linaongozwa na binadamu usije fikiria hakuna maovu huku ndani hapana yapo tu.

Linapokuja suala la maslahi huwa kuna misemo kama “Mbanga na Mbuyu” linakuwa na nguvu. Wakuu wetu katika hili siyo waaminifu wala waadilifu wao wanaangalia ndugu zao na watoto wao kwanza linapokuja suala la kuingia Jeshini.

Mjitathimini, Mjisahihishe “Jeshi la Ulinzi Wawananchi wa Tanzania” siyo vizuri kulisha nyumbu yako kwa jasho na damu za wengine
Ushauru mzuri.
 
Tatizo deep kabisa ni ukosefu wa ajira
Why mtu ulilie kuajiriwa jeshini?

Au serikalini?

Uchumi Una tatizo kubwa.
 
Shida ni utovu wa nidhamu

Kama ni kweli Mkuu wa JKT alienda "kuwaomba" wasitishe mgomo na bado wakakataa, hawafai kuwa wanajeshi, hata kama walijaza maji kwenye ziwa Victoria.
 
Mabeyo kutoka hadharani, tena mbele ya Rais na kutoa tamko la kuwatimua haikuwa bahati mbaya!

Kwenye hafla moja hivi, Mabeyo alisema jeshi lipo tayari kumtii Rais ambaye ni Mama Samia, lakini akataka kusema kitu mwishoni akamezea kuwa atamwasilishia Rais ofisini, ni nani anayejua alichotaka kusema...!?
Kuna waliong'amua kuwa kuna nyuma ya pazia!

Hivyo hao vijana hawajatimuliwa kwa bahati mbaya, jeshi linataratibu zake!
Ni wachache sana watakuelewa mkuu lakini nina uhakika hata hao waliotimuliwa wanajua kosa lao lilipo.
 
Back
Top Bottom