Jeshi lijitathimini kuhusu uadilifu na uaminifu wake kwa Watanzania wote

Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
375
500
Ndg wanajamvi habari za jumapili.
Niende kwenye mada moja kwa moja, “Jeshi lijitathimini” ndiyo Jeshi letu kwa macho ya nje limejivika vazi nzuri la uaminifu macho pa Watanzania wote lakini kwa ndani linapokuja suala la Ajira ndani ya Jeshi hasa hili tunaloliona la vijana wa JKT siyo Waaminifu kabisa. Wakuu wetu hawa wajitathimini tena kwanini wanazipoka haki za vijana wetu hawa hasa ambao hawana mahala pakuegemea.

Sakata la “Uasi wa Vijana wa JKT”
Jambo hili litazamwe upya na hawa vijana wasaidiwe hata km siyo ndani ya JWTZ lkn wapewe ajira maana hii ilikuwa ahadi ya Rais wa awamu ya tano. Kuna michezo mibaya sana labda kama Rais Samia hajui atadanganywa. Kabla vijana hawa kuna vijana ambao walishiriki shughuli mbalimbali za ujenzi kuanzia ngerengere, Dodoma nk ambao km ilivyo kwa hawa “Waasi”, wao walipewa ahadi nawakatimiziwa lakini haikuwa rahisi.
Ilianza kama ilivyokuwa kwa hawa “waasi” wakarejeshwa vikosini nakupewa Vyeti vyakumaliza mkataba wakatakiwa kuondoka huku wakipewa maagizo kuwa watatafutwa kukiwa na mabadiliko. Vijana wale wakafanya jitihada za kuwasiliana na uongozi lkn wakapewa maagizo kuwa waondoke hatua ya mwisho wakahangaika kupata mawasiliano ya alikuwa Rais Marehemu JPM wakafanikiwa, wakamweleza kuwa tumerudishwa nyumbani, JPM alishangaa kwann warudishwe wakati taarifa aliyonayo wanafanyiwa mchakato wa ajira na ana list amepelekewa? Ndipo alipomwagiza Brigedia Mbuge ampelekea list ya vijana walioshiriki ujenzi kuanzia ukuta wa mererani, Ngerengere na Dodoma, uzuri Mbuge alishtuka akapeleka list iliyohalisi ndipo JPM akagundua kuna waliochomekwa. Akaagizwa vijana waliositishiwa mkataba warejeshwe na hatimaye sasa ni Wanajeshi.

Natoa hii historia ili kwa wale ambao hawaelewi figisu zilipopo Jeshini linapokuja suala la Ajira watambue kuwa vijana wale walijua wazi kuwa wanaondolewa kijanja ili wengine wachomekewe. Rais wangu Samia wangalie vizuri hao wakuu na uchukue hatua vijana hawa wanapigania haki zao walioahidiwa na Rais JPM. Pili, Jeshi linaongozwa na binadamu usije fikiria hakuna maovu huku ndani hapana yapo tu.

Linapokuja suala la maslahi huwa kuna misemo kama “Mbanga na Mbuyu” linakuwa na nguvu. Wakuu wetu katika hili siyo waaminifu wala waadilifu wao wanaangalia ndugu zao na watoto wao kwanza linapokuja suala la kuingia Jeshini.

Mjitathimini, Mjisahihishe “Jeshi la Ulinzi Wawananchi wa Tanzania” siyo vizuri kulisha nyumbu yako kwa jasho na damu za wengine
 
Muite

JF-Expert Member
Sep 10, 2013
707
1,000
Wewe nadhani ni kati ya hao waliolazimisha ikaamriwa mrudishwe ilihali hamkidhi kulingana na vigezo, sasa mpo na ni Askari tayari. Kwahiyo unapigania na hawa walioonyesha migomo na kuandamana nao warejeshwe na kuingizwa Jeshini!!!!!.

Msitake kutuharibia Nchi yetu.
 
wa stendi

JF-Expert Member
Jul 7, 2016
19,907
2,000
Na wakupewa fursa na wale wote walioko mtaani nao wafikiriwe hivi serikali kwa nini isiwapeleke hata mbungani huko wakalinde nyumbu mbona tuna mapori kibao tuu ya hifadhi za taifa?
 
Detective J

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
13,260
2,000
Na wakupewa fursa na wale wote walioko mtaani nao wafikiriwe hivi serikali kwa nini isiwapeleke hata mbungani huko wakalinde nyumbu mbona tuna mapori kibao tuu ya hifadhi za taifa?

Sent using Jamii Forums mobile app
kulinda mbuga ni zaidi ya mafunzo ya kijeshi. ndio maana taasis zilizoko chini ya wizara ya maliasili tanapa ,tawa,tfs huchukua vijana jkt na kuwapeleka kozi maalumu kwa miezi sita..
kozi ina include paramilitary training na uhifadhi wa wanyama pori.

and yes hizo taasisi zinachukua vijana kila mwaka jkt.
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,680
2,000
Mabeyo kutoka hadharani, tena mbele ya Rais na kutoa tamko la kuwatimua haikuwa bahati mbaya!

Kwenye hafla moja hivi, Mabeyo alisema jeshi lipo tayari kumtii Rais ambaye ni Mama Samia, lakini akataka kusema kitu mwishoni akamezea kuwa atamwasilishia Rais ofisini, ni nani anayejua alichotaka kusema...!?
Kuna waliong'amua kuwa kuna nyuma ya pazia!

Hivyo hao vijana hawajatimuliwa kwa bahati mbaya, jeshi linataratibu zake!
 
Kwani si nao watapelekwa kozi kwani shida iko wapi
 
Prem 96

JF-Expert Member
Jul 19, 2019
632
1,000
Hao vijana wamejitakia wenyewe kufukuzwa kwa maelezo ya ndugu yangu ambae ni muhanga wa hilo sakata ni kuwa waligoma kupelekwa kwenye ujenzi sehemu nyingine na wakaandamana kutaka waajiriwe that why walipelekwa kwanza msata

na waligoma kuongea na kiongozi yoyote ispokuwa
Rais
makamu
CDF tu
Mabeyo kutoka hadharani, tena mbele ya Rais na kutoa tamko la kuwatimua haikuwa bahati mbaya!

Kwenye hafla moja hivi, Mabeyo alisema jeshi lipo tayari kumtii Rais ambaye ni Mama Samia, lakini akataka kusema kitu mwishoni akamezea kuwa atamwasilishia Rais ofisini, ni nani anayejua alichotaka kusema...!?
Kuna waliong'amua kuwa kuna nyuma ya pazia!

Hivyo hao vijana hawajatimuliwa kwa bahati mbaya, jeshi linataratibu zake!
 
Freyzem

JF-Expert Member
Jun 29, 2013
8,680
2,000
Hao vijana wamejitakia wenyewe kufukuzwa kwa maelezo ya ndugu yangu ambae ni muhanga wa hilo sakata ni kuwa waligoma kupelekwa kwenye ujenzi sehemu nyingine na wakaandamana kutaka waajiriwe that why walipelekwa kwanza msata

na waligoma kuongea na kiongozi yoyote ispokuwa
Rais
makamu
CDF tu

Sure, kuna watu wanawatetea bila kujua undani wa hilo jambo!

Hoja zao ni kwamba sijui wamefundishwa kutumia silaha so watajiingiza kwenye uhalifu!
 
mrangi

JF-Expert Member
Feb 19, 2014
54,569
2,000
Hao madogo wenge tu limewasumbua
Na wangekuwa wanajeshi full na kwa kitendo
Hicho wangefanywa kitu mbaya

Ova
 
Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
375
500
Hao vijana wamejitakia wenyewe kufukuzwa kwa maelezo ya ndugu yangu ambae ni muhanga wa hilo sakata ni kuwa waligoma kupelekwa kwenye ujenzi sehemu nyingine na wakaandamana kutaka waajiriwe that why walipelekwa kwanza msata

na waligoma kuongea na kiongozi yoyote ispokuwa
Rais
makamu
CDF tu
Hilo lakuwahamisha ilikuwa kuwapoteza uelekeo kwasababu JPM alitoa maagizo baada yakukamilika waajiriwe Jeshini moja kwa moja...narudia tena waliowatangulia walipokamilisha mission yao ya ujenzi walianza kutawanywa vikosini nakuamriwa warudi nyumbani JPM ndo aliwarudisha, sasa hivi JPM hayupo nani atawatetea?
 
Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
375
500
Wewe nadhani ni kati ya hao waliolazimisha ikaamriwa mrudishwe ilihali hamkidhi kulingana na vigezo, sasa mpo na ni Askari tayari. Kwahiyo unapigania na hawa walioonyesha migomo na kuandamana nao warejeshwe na kuingizwa Jeshini!!!!!.

Msitake kutuharibia Nchi yetu.
 
Whitesmith

JF-Expert Member
Aug 12, 2017
375
500
Wewe nadhani ni kati ya hao waliolazimisha ikaamriwa mrudishwe ilihali hamkidhi kulingana na vigezo, sasa mpo na ni Askari tayari. Kwahiyo unapigania na hawa walioonyesha migomo na kuandamana nao warejeshwe na kuingizwa Jeshini!!!!!.

Msitake kutuharibia Nchi yetu.
Uko kihisia zaidi mzee, wale wamepewa ahadi ya moja kwa moja wakikamilisha mission waajiriwe Jeshini direct sasa labda ndo moja ya maasi kwa Mwendazake
 
masopakyindi

JF-Expert Member
Jul 5, 2011
15,374
2,000
Uko kihisia zaidi mzee, wale wamepewa ahadi ya moja kwa moja wakikamilisha mission waajiriwe Jeshini direct sasa labda ndo moja ya maasi kwa Mwendazake
Magufuli alikosea PERIOD.
Jeshi haliendeshwi kwa hotuba za kuwapendezesha wapiga kura.
Lipo pale kikazi zaidi.
Vyombo vingine vya ulinzi na usalama walijazwa huko kina Makonda, Musiba na wengine.
Wamekuwa kituko.
Vyombo hivi haviingiliwi ili vifanye kazi ya Taifa, siyo ya mtu.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom