chakii
JF-Expert Member
- Sep 15, 2013
- 21,365
- 27,750
Habari wakuu.
Kuna hali ambayo siyo ya kawaida hapa Songea kwani asubuhi ya leo kila kona hapa Mjini na nje ya Mji Wanajeshi wametapakaa mitaani na hakuna taarifa yoyote ya uhakika iliyopatikana, watu wameingiwa hofu hata vyombo vya usafiri ikiwemo bodaboda kama ilivyozoeleka hakuna.
Mji umepoa sana.
Kwa mwenye taarifa zaidi tujuzane waungwana.

Nimepita na bodaboda naona njia nzima za mjini kuna wanajeshi wenye silaha na magari mengi sana, naambiwa njia ya Namtumbo wameweka road blocks za kutosha, Ruhuwiko kule kuna bodaboda wamesimamishwa, mbele ya hospital ya mkoa (Homso) zimepaki defender za kutosha zenye bendera nyekundu, kila anayehisiwa vibaya anasimamishwa hasa wa magari anasimamishwa na kuhojiwa/kupekuliwa...nasogea karibu na bank ya NMB naona wameanza kupiga mabomu ya machozi sijajua chanzo, nimeamua kusogea Mambo Leo kidogo kula, nitarudi mjini baadaye kupata taarifa kamili.
mapichapicha
![]()
![]()
![]()