Jeshi La Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Lakanusha Wanajeshi wa Ngazi ya Juu Kuongezewa Mshahara

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) linatoa taarifa kuwa kuna habari ya uzushi iliyosambazwa na mtandao wa kiiamii wa Tanzania Abroad TV (TAT) kwamba Wanajeshi wa ngazi za juu wa JWTZ wameongezewa mshahara. Taarifa hiyo imeeleza kuwa ongezeko hilo limelipwa tarehe 18 Agosti 2023.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaujulisha Umma kuwa taarifa hiyo ni ya uzushi na upotoshaji kwa jamii. Watanzania waelewe kuwa taarifa hiyo ina nia ovu, hivyo ipuuzwe.

Ukweli ni kwamba had leo tarehe 19 Agosti 2023 kwa JWTZ haijafika tarehe ya kulipwa mshahara. Aidha, hakuna ongezeko lolote la mshahara au malipo yoyote kwa Wanajeshi wa ngazi yoyote wa JWTZ yaliyofanyika tarehe 18 Agosti 2023 kama ilivyotajwa na mtandao huo wa kijamii.

Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania linaendelea kufuatilia na kuchunguza kwa kina aliyehusika na upotoshaji huo ili hatua za kisheria zichukuliwe dhidi yake.​

JWTZ.jpeg
 
Kuna issue nyingine unapojitokeza kuzijibu ndio unasaidia kuzisambaza kwa jamii kubwa zaidi na hata kuwafanya waamini kuwa hilo jambo lipo kweli.

Other rumours dissolve by itself
 
Kwani payee si ishatoka!!
Kila mtu anajua ameongezewa sh.ngapi?
Mpaka sasa ma HR wanajua kila kitu.
Inamaana hata nyongeza ikija JWTZ wataipata kwa kushitukiza?
Utawala dhalimu mwaka jana waliwaongezea 23% kamili ilhali watumishi wengine walipata 02%
 
Watu wanasoma mitandaoni kuwa wameongezewa hela wakati hata mshahara hawajapokea 🤣🤣🤣🤣🤣

Huyo mzushi kayatafuta mwenyewe, wakimdaka watamfundisha uzalendo.
 
Au wanapoozwa sababu jeshi limekataa mkataba mbovu piaa..limeshauri wasikilize wananchi ....vifungu vibadilishwe k2a manufaa ya Taifa
 
Kumbe ni uzushi.kuna mjeshi alinitongoza nilishamkubalia kwa ajili ya ongezeko
Ngoja nimblock
Asante mkuu wa jeshi kwa kuongea hilo mapema.
Utajikosesha bahati kwa kulishwa matango na hao "wasemaji" binti.

Kwani mshahara ukitoka kesho ukiwa na nyongeza pamoja na mapunjo yao ya mwezi July, huyo "msemaji" atarudi na kujitokeza tena kurewind taarifa kwa umma kuwa: ..."kilichokuwa ni uzushi sasa kimefanyiwa kazi na ku geuzwa kuwa ni ukweli na leo tumezinyaka"..., atasemaaa? Thubutu!
 
Utajikosesha bahati kwa kulishwa matango na hao "wasemaji" binti.

Kwani mshahara ukitoka kesho ukiwa na nyongeza pamoja na mapunjo yao ya mwezi July, huyo "msemaji" atarudi na kujitokeza tena kurewind taarifa kwa umma kuwa: ..."kilichokuwa ni uzushi sasa kimefanyiwa kazi na ku geuzwa kuwa ni ukweli na leo tumezinyaka"..., atasemaaa? Thubutu!
Mkuu kwa sasa ngoja tutembelee taarifa iliyopo.unataka niende kwa kubet??
 
Back
Top Bottom