johnthebaptist
JF-Expert Member
- May 27, 2014
- 83,934
- 141,905
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni afande Kibona amesema jeshi hilo mkoani kwake limesitisha vibali ilivyovitoa na vinavyotegemewa kutolewa kwa shughuli za maandamano, maonesho, jogging na mbio ikiwemo Haki marathon.
Vibali hivyo vimesitishwa kwa sababu za kiusalama.
Chanzo: ITV habari
Maendeleo hayana vyama!
=====
Vibali kwa ajili uendeshaji wa shughuli au maonesho pamoja na maandamano na mbio kama Marathon zinazofanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo Masaki, Oysterbay, Mikocheni na Msasani vimesitishwa kutokana na sababu za kiusalama
Kaimu Kamanda wa Polisi - Kinondoni, ACP Japheth Kibonah amesema, "Tumekuwa tukitoa vibali kwa makundi mbalimbali lakini kutokana na sababu za kiusalama vibali vyote ambavyo vilikuwa vimetolewa kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali iwe maandamano, mbio (marathon) na maonesho mengineyo vimesitishwa"
Ameeleza kuwa, sababu hizo za usalama zinaendelea kufanyiwa mchakato na kuwataka wananchi kutii matakwa hayo aliyosema yanalenga kuhakikisha hali ya kiusalama katika Mkoa wa Kinondoni inaendelea kuimarishwa