Jeshi la Polisi lasitisha vibali vyote vya mbio, jogging, maonesho na maandamano kwa sababu za kiusalama

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
41,833
2,000
Kamanda wa polisi mkoa wa kipolisi Kinondoni afande Kibona amesema jeshi hilo mkoani kwake limesitisha vibali ilivyovitoa na vinavyotegemewa kutolewa kwa shughuli za maandamano, maonesho, jogging na mbio ikiwemo Haki marathon.

Vibali hivyo vimesitishwa kwa sababu za kiusalama.

Chanzo: ITV habari

Maendeleo hayana vyama!

=====

Vibali kwa ajili uendeshaji wa shughuli au maonesho pamoja na maandamano na mbio kama Marathon zinazofanyika katika maeneo mbalimbali yakiwemo Masaki, Oysterbay, Mikocheni na Msasani vimesitishwa kutokana na sababu za kiusalama

Kaimu Kamanda wa Polisi - Kinondoni, ACP Japheth Kibonah amesema, "Tumekuwa tukitoa vibali kwa makundi mbalimbali lakini kutokana na sababu za kiusalama vibali vyote ambavyo vilikuwa vimetolewa kwa ajili ya kufanya shughuli mbalimbali iwe maandamano, mbio (marathon) na maonesho mengineyo vimesitishwa"

Ameeleza kuwa, sababu hizo za usalama zinaendelea kufanyiwa mchakato na kuwataka wananchi kutii matakwa hayo aliyosema yanalenga kuhakikisha hali ya kiusalama katika Mkoa wa Kinondoni inaendelea kuimarishwa
 

Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Oct 25, 2016
1,704
2,000
Polisi waache mambo ya kitoto! Walitakiwa waseme wamesitisha kwa sababu ya hili janga la corona.

Na tunatarajia hata wale fisiemu walio tutishia nyau kutaka kumshinikiza yule mungu wao kutawala milele, wataifyata mikia yao kuanzia sasa.
Misa je! Itasitishwa jumapili?
 

Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
4,905
2,000
Kudhibiti maambukizi ya koona na yenyewe ni sababu ya kiusalama....vipi wale wanaofanya jogging mida ya jioni kwa mtu mmoja mmoja, isifike tukazuiwa hata kutembea barabarani....
 

Undu

JF-Expert Member
May 18, 2013
2,539
2,000
Nil iona JWTZ wakikimbia mchakamchaka hadi nilijiuliza kwamba hawagopi covid 19.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom