Jesca Kishoa, asimamishwa Vikao viwili vya Bunge

Jesca Kishoa, asimamishwa Vikao viwili vya Bunge

MH. JESCA KISHOA ATIKISA BUNGE SWALA LA KASHIFA YA MABEHEWA.

Na Kilawa the Iron

Bunge limeamua kumsimamisha Mh Jesca Kishoa kwa madai ya kwamba kashindwa kuthibitisha juu ya swala la kashifa ya mabehewa. Huu ni udhaifu uliojidhihirisha bungeni.

Awali ya yote sina budi kumpongeza Mh Jesca Kishoa kwa kutudhihirishia kwamba viatu alivyokuwa akivivaa Mh Kafulila na yeye vinamtosha. Ameonesha wazi kwamba hayumbushwi na uzembe wa viongozi wa bunge.

Ikumbukwe kashifa hii ya mabehewa iliibuliwa na Mh Kafulila na alieleza mwaka jana(2015) kwa kina juu ya Riport ya PPRA na Mamlaka nyinginezo zenye ripoti ya kashifa ya mabehewa.

Katika hali isiyoyakawaida bunge letu limedhihirisha kwamba halina meno ya kuutafuna mfupa uliopo mbele yake na si kushindwa kutafuna mfupa tu bali hata mnofu uliopo bunge limeshindwa kuutafuna badala yake linang'oa meno

Kumtoa Jesca kishoa bungeni ni sawa na kung'oa meno ya mbele na meno chonge halafu ukabakiwa na meno ya Nyuma tu.

Nini kilipaswa kufanyika na bunge kabla ya maamuzi ya kumsimamisha Jeska Kishoa kuhudhuria bungeni kwa siku mbili?

Mosi, Bunge lilipaswa kuhakikisha serikali inaleta riport iliyopo kutoka mamlaka husika bungeni ili wabunge waisome na waijadili kwa kina ili waone ni wapi pakuisimamia serikali.

Pili,Bunge lilipaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mh Jesca Kishoa na Kafulila ili waweze kupata undani wa swala hilo na kuweza kulifanyia kazi bungeni kwa ufasaha.

Tatu, bunge lisifanye kazi ya kuitetea serikali badala yake lifanye kazi ya kuisimamia serikali. Bunge hili lifanye kazi kama mhimili unaojitegemea.

Nne, wabunge wote waache uvyama ndani ya bunge badala yake waoneshe ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mjibu wa katiba na sheria za nchi yetu.

Naamini katika hayo machache bunge linaweza kufanya kazi kwa ufasaha, linaweza kuisimamia serikali badala ya kufukuza wabunge wa upinzani.

Kwanini udhaifu huu wa bunge unajitokeza?

Mosi, Ni vigumu sana kesi ya ngedere kuhulumiwa na Nyani. Kiujumla washiriki wakuu wa kashifa za ufisadi wengi wao ndio viongozi wa bunge na ndio viongozi wa serikali hivyo hali hii inapelekea ugumu kuwajibisha serikali kwakuwa wahusika ni walewale wenye mamlaka.

Pili, Wabunge kuendekeza uvyama ndani ya bunge, chuki binafsi, ubinafsi n.k

Tatu, baadhi ya wabunge pia hawajui majukumu yao yaliyowapeleka pale, wanadhani wamekwenda kuunga mkono hoja na kupiga makofi na sio vinginevyo

Hayo yote yakifanyiwa ukarabati naamini bunge linaweza kuwa na usimamizi mzuri wa serikali, uwakirishi mzuri wa wananchi.

Msema ukweli ni adui wa watenda maovu.
Hivi wewe kweli unajua kilicho mfanya asimamishwe?
 
Serikali ilifanya uchunguzi kwa hiyo wana documents zote!!

Kama bunge lingekuwa liko partial wangeamuru hiyo report iletwe ili ukweli ufahamike. Wanafanya hivyo kwa vile wanajua itakuwa vigumu kwa watu wa nje kuipata hiyo report ............ Kama Kishoka kaja na maneno matu bila ushahidi na Mwakyebe kajibu kwa maneno matupu bila ushahidi, binafsi sioni sababu ya huyo Bi Kishoka kisimamishwa!!!
Swala hapa lilikuwa ni Binti kishoa kusema ilipotea billion 234 na akashindwa kuthibitisha....
 
Sasa huyu huyu mwanamke mkwala wote ule aliyokuwa anapiga kumbe ushahidi hana au alikuwa anamtegemea Kubenea ampe ushahidi wa Mwanahalisi.
 
Kubenea si ana ushahidi angempa mbuge mwenzake???? Teh Teh Teh Teh😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀😀
Kubenea ana ushahidi wa ufisadi wa Lowassa tu kwani huyu alimshughulikia for 10+ years. Hawa mafisadi wengine ni habari za hapa na pale tu kama ilivyo elimu yake!
 
Kweli CCM mmetegwa mkategeka! Huyu binti anao ushahidi wa kutosha, hakuupeleka makusudi ili kuvuta hisia za watu! Sasa CCM wamenasa na umma tayari unataka kujua kulikua na nini kwenye mabehewa hayo.Ushahidi sasa ndio utaletwa inawezekana kupitiabunge mwingine na siyo Kishoa Jesca. CCM wameshamshika Simba mkia sasa wale wapole!Mwakyembe ameshindwa kujinasua na msala huu mapema sasa awe mpole.
Kwi kwi kwi kwi! Kwa nini asiulete Mwakyembe ajiuzulu au anabaki nao kama Mbowe na ushahidi wake wa mabomu ya Arusha.
 
Funzo zuri kwangu na kwako ....natuyapime maneno yetu katika mizani isiyo na choyo wala upunjufu.
 
Wanacha kuadhibu mafisadi wa Escrow walioko Bungeni wanahangaika na wazalendo wa nchi hii!
Kwa upeo wako huo, nadhani huyo mzalendo wako ndo alitakiwa kutoa nondo za ukweli kwani alipata fursa nzuri sana, lakini inaonekana kachukua maneno kwemye vijiwe vya kahawa na tangawizi ndo kaamua kufanyia kazi Bungeni ila akasahau kwamba vinatakiwa vielelezo vya kutosha.
 
Tena angechezea mvua ya vikao 5 ndio ingemfanya ajitambue kua awapo bungeni atakiwi kukurupuka bali ni facts tu ndio zinafanya kazi.
Vipi kauli ya Lusinde kuwa chama kikishindwa uchaguzi kinakuwa magaidi aliambiwa alete ushahidi?
 
Chadema imejaza wabunge vilaza bungeni!
Hii imechangiwa na elimu zao za 'hapa na pale'
 
Binafsi nachukizwa sn pale mbunge anakurupuka na stori za vijiwe vya kahawa na kuzipeleka bungeni! Hii tabia ya kuwazushia watu uongo lazima ikomeshwe.
Haiishindi Wale Wanaoomba Kuhararisha Matumizi Ya Bangi Na Mirungi!!!!
 
Chadema imejaza wabunge vilaza bungeni!
Hii imechangiwa na elimu zao za 'hapa na pale'
Hawashindi CCM, Walioleta Wauza Bangi Na Mirungi, Ambao Wanataka Serikali Biashara Ihararishwe Rasmi Na Mafisadi Wakubwa!!! TENA Wamepewa Uongozi Wa BUNGE Na SERIKALI!!!
 
Hili ni funzo kwa Wabunge wanaofikiri Bunge ni sehemu ya Kuropoka tu...


Wajifunze kwa Zitto, Mnyika na Lissu... Wanakusanya Ushahidi kabla ya kupeleka Bungeni.
 
Hawashindi CCM, Walioleta Wauza Bangi Na Mirungi, Ambao Wanataka Serikali Biashara Ihararishwe Rasmi Na Mafisadi Wakubwa!!! TENA Wamepewa Uongozi Wa BUNGE Na SERIKALI!!!
Tukiingia madarakani tutahararisha gongo-Chadema. Au umesahau?
 
Back
Top Bottom