Jesca Kishoa, asimamishwa Vikao viwili vya Bunge

Jesca Kishoa, asimamishwa Vikao viwili vya Bunge

Huyo mwenyekiti wa Bunge anafukuza wabunge badala ya kuitaka serikali kuleta Bungeni mkataba wa manunuzi ya mabehewa na riport ya CAG? Hivi chenge anaweza kukemea mafisadi? Post za wana JF humu ndani kuna ushabiki sana wa kisiasa badala ya facts. Je anayoyafanya JPM yangefanywa na uongozi wa upinzani yangesemwa mangapi? Kweli tunaisoma Namba.
HIVI Utategemea Andrew Chenge Apambane Na Ufisadi Na Mafisadi Bungeni Au Nje Ya BUNGE!!! WKT Yeye Mwenyewe Ni FISADI!!!
 
Sasa ukweli uko wapi.....zimetumika B60 sivyo kihalali au vipi.Afadhali Mwakiyembe umeweka mambo sawa ili utumbuaji uishe...
 
Binafsi nachukizwa sn pale mbunge anakurupuka na stori za vijiwe vya kahawa na kuzipeleka bungeni! Hii tabia ya kuwazushia watu uongo lazima ikomeshwe.
 
Kwa hiyo kwa mujibu wa Mwakyembe no kuwa wao hawajapiga hizo bilioni230 Bali walipiga bilioni60 tuu?
Na bado mazoba ya ccm yanaona fahari kupigwa hizo, kweli hizi ni akili za maiti
 
Haki imetendeka!
Ni vyema Kubenea akathibitiwa ili asiwaponze wenzie zaidi.....!
Na Swala la kuhusu Shanga na chupi za kubenea lichunguzwe ili hatua zichukuliwe...

Hongera sana spika kwa kutenda haki.
 
Binafsi nachukizwa sn pale mbunge anakurupuka na stori za vijiwe vya kahawa na kuzipeleka bungeni! Hii tabia ya kuwazushia watu uongo lazima ikomeshwe.
Wakupewa lawama ni kubenea sasa Jesca taratibu ana anza kufata nyayo za mumewe!
 
Mbona kapewa adhabu ndogo hivyo!!!!
Sipendi aina ya watu wanaokurupuka bila vielelezo.
 
Jesca kama Kubenea hawajadili wala kuleta hoja za maslahi kwa taifa zaidi ya hoja za matukio na watu. Qoute: "Simple minds"
 
kwi kwi ccm bwana sita alishatangaza ukweli huo majaliwa kasema ukweli huo ombeni sefue kasema ukeli huo magufuli katimuwa watu kwa kununua mabehewa feki kamuacha mwakyembe geni lipi hapo ccm mutakimbizana lakini ukweli upo wazi ndungai hutaweza ziba watu midomo nchi imewashinda asubuhi kweupe
 
Yani huyu Mke wa Kafulila na elimu yake ana danganywa na mtu mwenye elimu ya hapa na pale kweli?
 
Kwa hiyo kusimamishwa huku kutafuta uhalali wa taarifa ya Mzee Samuel Sitta kuwa yalinunuliwa mabehewa mabovu kitapeli!?
 
DAR ES SALAAM

SIKU chache kupita baada ya Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye kuituhumu serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwafumbia macho Watendaji walio isababishia nchi hasara ya bilioni 230 kwenye ununizi wa Mabehewa yanayotajwa kuwa ni feki.

Naye Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta ameibuka na kusema watendaji wote waliohusika na kashfa hizo wanafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.

Sitta ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema Kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilsiha kazi yake na kuonyesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli ya Kati TRL ambayo imepelekea hadi kununiliwa kwa mabehewa hayo.

Amesema Kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wamabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.

Amesema baada ya Kamati hiyo kubaini kampuni hiyo haina sifa hivyo kamati imebaini pia kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa Shirika la Reli ya Kati TRL kwa kuwa walikiuka kanuni za manunizi ya serikali kwa kitendo cha kutoa fedha zote kwa kampuni hiyo kabla hawajaleta mabehewa.

“Yaani kamati hii ilibaini kuna uzembe kwa watendaji hawa TRL walikuka kanuni za ununuzi wa Umma,yaani sheria inawataka kutoa pesa kwa awamu ,lakini hawa watendaji wametoa pesa zote bila hata ya mabehewa kuletwa yote,inaonekana hapa ni kunauzembe ambao umeitia hasara serikali” amesema Sitta.

Sitta amewataja watendaji hao ambao watafikishwa mahakamani mda wowote ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Kipallo Kisamfu,Mhandisi mkuu wa mitambo Ngosowile Ngosomiles,Mhasibu Mkuu Mbaraka Mchopa,

Wengine ni Mkaguzi mkuu wa ndani wa Kampuni Jasper Kisiraga,pamoja Meneja Mkuu wa Manunuzi Fedinard Soka.

KUHUSU KUHUSIKA KWA MWAKYEMBE.

Sitta alipoulizwa na waaandishi wa Habari juu ya kuhusika aliyekuwa Waziri wa uchukuzi ambapo kipindi hicho ununuzi wa Mabehewa hayo yalifanyika ambaye sasa ni Waziri wa Afrika mashariki Dk Mwakyembe.

Sitta alijibu waziri huyo ahusiki na ufisadi huo akidai waziri wa wizara sio jukumu lake kuhizinisha pesa.

“Sikiliza waziri sio anasehizinisha pesa kutoka kununu kitu chochete kwenye wiizara bali watendaji wa chini ndio jukumu lao kufanya hivyo na hawa ndio wamefanya upuuzi huu ndio maana tunawafikisha mahakamani”

KUHUSU KASHFA YA RICHMOUND

Sitta hakusita kuzungumzia kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond ambayo ndio ilipelekea kujiuzulu kwa Edward Lowasa nafasi ya waziri mkuu,

Ambapo Sitta amesema yeye wakati alipokuwa spika wa Bunge la tatu kamati yake aliyo unda kuchunguza sakata hilo ilifanya kazi nzuri.

Alipobanwa na waandishi wa Habari walipotaka kujua ni kwanini anaibuka sahivi kumtuhumu lowassa yeye na Mwakyembe walikuwa wapi miaka nane imepita toka ajiuzulu kwenye nafasi ya Uwaziri mkuu,

Akajibu kwa kusema mtu wa kulaumiwa ni serikali kwa kushindwa kuwachukulia watu wote waliohusika na kashfa hiyo

“Sisi tuliweka mapendekezo 23 na tuliikabidhi Serikali pamoja na Ofisi ya waziri mkuu kwa hatua zaidi lakini wao hawakuwachukulia hatua,kwahiyo sisi sio kazi yetu kama bunge kumfikisha mahakamani ,kazi hiyo ingetakiwa kufanywa na serikali kwahiyo,haikufanya na sisi hatuna uwezo huo” amesema Sitta.
 
Ndugai ni zero kabisa anakanyagwa na serikali kakabwa koo hana analoweza for the five coming years wananchi tujisimamie hatuna serikali wala bunge vinavyojali mustakabali wa nchi tukilegeza kamba tutabaki kukatana mapanga na kukabana kila kukicha CCM ni wapuuzi wapuuzi sana
 
Kwa hiyo kwa mujibu wa Mwakyembe no kuwa wao hawajapiga hizo bilioni230 Bali walipiga bilioni60 tuu?
Na bado mazoba ya ccm yanaona fahari kupigwa hizo, kweli hizi ni akili za maiti
Wewe ni mgumu kuelewa
 
dah, eti kishoa kawa kishoiya! Watu wanamaneno!!
mumewe amweleze,umaarufu huja taaratibu kwa kujipanga sio kuropoka ili ufahamike haraka mwisho unaaibika.
mtu mzima kuitwa mwongo ni aibu Tena ukiwa kiongozi ni fedheha haswaaa...
Chenge kampendelea,angempiga vikao vitano mpaka bunge lijalo,bunge lisitumiwe kama sehemu ya kupika majungu Ila facts.
 
Back
Top Bottom