figganigga
JF-Expert Member
- Oct 17, 2010
- 25,658
- 55,484
JESCA David Kishoa Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Jimbo la Iramba Magharibi, amesimamishwa kuhudhulia vikao viwili vya bunge. Ni baada ya kuleta bungeni habari kuhusu mabehewa feki na kushindwa kuthibitishia bunge. Ameshindwa kuthibitisha aliyo yasema, hivyo kasimamishwa vikao viwili, alitakiwa asimamishwe vikao vitano.
Siku yenyewe ilikua hivi;
Kishoa alianza kumtaja Dk Mwakyembe kuwa ni jipu linalohitaji kutumbuliwa na Rais na kuwa nafasi aliyonayo hakustahili.
Kishoa alitaja sababu ya kumwita Dk Mwakyembe si msafi kwamba alitumia zaidi ya Sh 238 bilioni kwa ajili ya kununulia mabehewa ambayo yalithibitika kuwa ni mabovu.
Waziri Mwakyembe alikanusha madai yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Jesca Kishoa kuwa ununuzi huo wa mabehewa mabovu uliisababishia sherikali hasara ya shilingi bilioni 238, huku akitaka ripoti ya ukaguzi wa ununuzi huo iwasilishwe bungeni.
Akitumia kanuni ya 63 (3) kuomba kutoa taarifa, Mwakyembe alikanusha kiwango cha fedha kilichotajwa na mbunge huyo wa viti maalum ambaye ni mke wa aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.
“Mbunge aliyesimama kabla, aliyejitambulisha kama mke wa Kafulila, ameeleza kwamba serikali ilitumia zaidi ya shilingi bilioni 238 na kuleta hasara kwa kununua mabehewa mabovu. Mheshimiwa Mwenyekiti nataka kukuthibitishia kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kwa kununua mabehewa 274 haijawahi kutumia zaidi ya shilingi bilioni 60,”alisema Mwakyembe.
Waziri huyo alienda mbali na kueleza kuwa endapo mbunge huyo atawasilisha uthibitisho wa kiwango hicho cha fedha kutumika kununua mabehewa hayo, atajiuzulu nafasi yake ya ubunge.
“Mimi naomba athibitishe hiyo shilingi bilioni 238. Na nitashukuru sana kama akileta hapa. Na akileta hiyo, mimi nitajiuzulu hata ubunge,” alisema Mwakyembe.
Baada ya kauli hiyo ya Mwakyembe, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee naye alisimama na kueleza kuwa Waziri huyo hakutumia kifungu sahihi kutoa taarifa kwa kuwa alipaswa kutumia kifungu cha 63 (4) kutoa ushahidi wa kukanusha kwake kwanza.
Naye Kishoa aliendelea kusisitiza kuwa Serikali inapaswa kuwasilisha bungeni hapo ripoti ya ukaguzi wa manunuzi ya mabehewa hayo.
Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Dk. Mary Mwanjelwa alitoa siku tatu kwa mbunge huyo wa viti maalum kuwasilisha ushahidi kuhusu madai yake. Ambao kashindwa kuwasilisha hadi leo
Hivi leo kutokana na kanuni, Andrew Chenge, kaamua kumfungia vikao viwili asihudhulie bungeni kwani alitakiwa amfungie vikao vitano, lakini kwakuwa bunge limebakiza siku mbili, kaamua kumfungia siku mbili. Kabla ya kufungiwa Jesca alipewa nafasi ya kufuta kauli yake, lakini akakataa na kuendelea kusisitiza kwamba aliyoyasema ni ukweli haoni sababu ya kufuta kauli, ndipo Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge kaamua kumfungia.