Jesca Kishoa, asimamishwa Vikao viwili vya Bunge

Jesca Kishoa, asimamishwa Vikao viwili vya Bunge

Ningeshangaa kama we kigagula usingejitokeza kwenye thread kama hii.....waite na mapumbavu wenzio...Lizaboni, Hamy-D,and the likes. Hizi ndio thread size yenu...
Bavicha acha matusi mtu akisema uongo adhabu yake ni kusimamishwa vikao...
 
Mwakyembe aliwapa chance ya kummaliza kumbe hawana data zaidi ya kuropoka tu!!
Mtu kawaambia Kama mkileta huo ushahidi najiudhuru hata ubunge!
Hizo data zingekuwepo si UKAWA wangeona ndio sehemu ya kupatia sifa???
Wana mtegemea Kubenea kwa data..
 
DAR ES SALAAM

SIKU chache kupita baada ya Waziri mkuu mstaafu, Fredrick Sumaye kuituhumu serikali ya Rais Jakaya Kikwete kuwafumbia macho Watendaji walio isababishia nchi hasara ya bilioni 230 kwenye ununizi wa Mabehewa yanayotajwa kuwa ni feki.

Naye Waziri wa Uchukuzi Samwel Sitta ameibuka na kusema watendaji wote waliohusika na kashfa hizo wanafikishwa mahakamani muda wowote kutoka sasa baada uchunguzi kukamilika.

Sitta ametoa kauli hiyo Jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano na waandishi wa Habari ambapo amesema Kamati iliyoundwa kuchunguza sakata hilo imeshakamilsiha kazi yake na kuonyesha kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa shirika la reli ya Kati TRL ambayo imepelekea hadi kununiliwa kwa mabehewa hayo.

Amesema Kamati hiyo ilikwenda hadi nchini India kuichunguza kampuni ya M/S Hindusthan Engineering and Industrial Limited ambayo ndiyo watengenezaji wamabehewa hayo mabovu na kubaini kampuni hiyo iliyopewa zabuni ilikuwa haina sifa.

Amesema baada ya Kamati hiyo kubaini kampuni hiyo haina sifa hivyo kamati imebaini pia kulikuwa na uzembe kwa watendaji wa Shirika la Reli ya Kati TRL kwa kuwa walikiuka kanuni za manunizi ya serikali kwa kitendo cha kutoa fedha zote kwa kampuni hiyo kabla hawajaleta mabehewa.

“Yaani kamati hii ilibaini kuna uzembe kwa watendaji hawa TRL walikuka kanuni za ununuzi wa Umma,yaani sheria inawataka kutoa pesa kwa awamu ,lakini hawa watendaji wametoa pesa zote bila hata ya mabehewa kuletwa yote,inaonekana hapa ni kunauzembe ambao umeitia hasara serikali” amesema Sitta.

Sitta amewataja watendaji hao ambao watafikishwa mahakamani mda wowote ni Mkurugenzi Mtendaji wa TRL Kipallo Kisamfu,Mhandisi mkuu wa mitambo Ngosowile Ngosomiles,Mhasibu Mkuu Mbaraka Mchopa,

Wengine ni Mkaguzi mkuu wa ndani wa Kampuni Jasper Kisiraga,pamoja Meneja Mkuu wa Manunuzi Fedinard Soka.

KUHUSU KUHUSIKA KWA MWAKYEMBE.

Sitta alipoulizwa na waaandishi wa Habari juu ya kuhusika aliyekuwa Waziri wa uchukuzi ambapo kipindi hicho ununuzi wa Mabehewa hayo yalifanyika ambaye sasa ni Waziri wa Afrika mashariki Dk Mwakyembe.

Sitta alijibu waziri huyo ahusiki na ufisadi huo akidai waziri wa wizara sio jukumu lake kuhizinisha pesa.

“Sikiliza waziri sio anasehizinisha pesa kutoka kununu kitu chochete kwenye wiizara bali watendaji wa chini ndio jukumu lao kufanya hivyo na hawa ndio wamefanya upuuzi huu ndio maana tunawafikisha mahakamani”

KUHUSU KASHFA YA RICHMOUND

Sitta hakusita kuzungumzia kashfa ya kampuni tata ya kufua umeme ya Richmond ambayo ndio ilipelekea kujiuzulu kwa Edward Lowasa nafasi ya waziri mkuu,

Ambapo Sitta amesema yeye wakati alipokuwa spika wa Bunge la tatu kamati yake aliyo unda kuchunguza sakata hilo ilifanya kazi nzuri.

Alipobanwa na waandishi wa Habari walipotaka kujua ni kwanini anaibuka sahivi kumtuhumu lowassa yeye na Mwakyembe walikuwa wapi miaka nane imepita toka ajiuzulu kwenye nafasi ya Uwaziri mkuu,

Akajibu kwa kusema mtu wa kulaumiwa ni serikali kwa kushindwa kuwachukulia watu wote waliohusika na kashfa hiyo

“Sisi tuliweka mapendekezo 23 na tuliikabidhi Serikali pamoja na Ofisi ya waziri mkuu kwa hatua zaidi lakini wao hawakuwachukulia hatua,kwahiyo sisi sio kazi yetu kama bunge kumfikisha mahakamani ,kazi hiyo ingetakiwa kufanywa na serikali kwahiyo,haikufanya na sisi hatuna uwezo huo” amesema Sitta.
Bavicha hiyo habari iliandikwa na gazeti gani?
 
dah, eti kishoa kawa kishoiya! Watu wanamaneno!!
mumewe amweleze,umaarufu huja taaratibu kwa kujipanga sio kuropoka ili ufahamike haraka mwisho unaaibika.
mtu mzima kuitwa mwongo ni aibu Tena ukiwa kiongozi ni fedheha haswaaa...
Chenge kampendelea,angempiga vikao vitano mpaka bunge lijalo,bunge lisitumiwe kama sehemu ya kupika majungu Ila facts.
Kubenea ataendelea kuwaponza UKAWA
 
JESCA David Kishoa Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Jimbo la Iramba Magharibi, amesimamishwa kuhudhulia vikao viwili vya bunge. Ni baada ya kuleta bungeni habari kuhusu mabehewa feki na kushindwa kuthibitishia bunge. Ameshindwa kuthibitisha aliyo yasema, hivyo kasimamishwa vikao viwili, alitakiwa asimamishwe vikao vitano.

Siku yenyewe ilikua hivi;

Kishoa alianza kumtaja Dk Mwakyembe kuwa ni jipu linalohitaji kutumbuliwa na Rais na kuwa nafasi aliyonayo hakustahili.

Kishoa alitaja sababu ya kumwita Dk Mwakyembe si msafi kwamba alitumia zaidi ya Sh 238 bilioni kwa ajili ya kununulia mabehewa ambayo yalithibitika kuwa ni mabovu.

Waziri Mwakyembe alikanusha madai yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Jesca Kishoa kuwa ununuzi huo wa mabehewa mabovu uliisababishia sherikali hasara ya shilingi bilioni 238, huku akitaka ripoti ya ukaguzi wa ununuzi huo iwasilishwe bungeni.

Akitumia kanuni ya 63 (3) kuomba kutoa taarifa, Mwakyembe alikanusha kiwango cha fedha kilichotajwa na mbunge huyo wa viti maalum ambaye ni mke wa aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.

“Mbunge aliyesimama kabla, aliyejitambulisha kama mke wa Kafulila, ameeleza kwamba serikali ilitumia zaidi ya shilingi bilioni 238 na kuleta hasara kwa kununua mabehewa mabovu. Mheshimiwa Mwenyekiti nataka kukuthibitishia kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kwa kununua mabehewa 274 haijawahi kutumia zaidi ya shilingi bilioni 60,”alisema Mwakyembe.

Waziri huyo alienda mbali na kueleza kuwa endapo mbunge huyo atawasilisha uthibitisho wa kiwango hicho cha fedha kutumika kununua mabehewa hayo, atajiuzulu nafasi yake ya ubunge.

“Mimi naomba athibitishe hiyo shilingi bilioni 238. Na nitashukuru sana kama akileta hapa. Na akileta hiyo, mimi nitajiuzulu hata ubunge,” alisema Mwakyembe.

Baada ya kauli hiyo ya Mwakyembe, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee naye alisimama na kueleza kuwa Waziri huyo hakutumia kifungu sahihi kutoa taarifa kwa kuwa alipaswa kutumia kifungu cha 63 (4) kutoa ushahidi wa kukanusha kwake kwanza.

Naye Kishoa aliendelea kusisitiza kuwa Serikali inapaswa kuwasilisha bungeni hapo ripoti ya ukaguzi wa manunuzi ya mabehewa hayo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Dk. Mary Mwanjelwa alitoa siku tatu kwa mbunge huyo wa viti maalum kuwasilisha ushahidi kuhusu madai yake. Ambao kashindwa kuwasilisha hadi leo

Hivi leo kutokana na kanuni, Andrew Chenge, kaamua kumfungia vikao viwili asihudhulie bungeni kwani alitakiwa amfungie vikao vitano, lakini kwakuwa bunge limebakiza siku mbili, kaamua kumfungia siku mbili. Kabla ya kufungiwa Jesca alipewa nafasi ya kufuta kauli yake, lakini akakataa na kuendelea kusisitiza kwamba aliyoyasema ni ukweli haoni sababu ya kufuta kauli, ndipo Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge kaamua kufungia.

Ajifunze madhara ya kuropoka
 
Mbona january makamba alitudanganya enzi zile za kampeni kwamba hakuna helkopta yao iliyoanguka zote zipo salama mida ya jion,ucku ndege ikapatikana mbugani
 
Ameshindwa kuwasilisha ushaidi wa tuhuma dhidi ya Mwakyembe na hata Mwenyekiti alipomtaka afute maneno yake maana ameshindwa kuleta ushaidi aligoma kufuta maneno yake.

Hivyo Mwenyekiti akatangaza kuwa kwa mjibu wa kanuni ilibidi asimamishwe vikao vitano ila kwa sababu bado siku mbili bunge liishe anamsimamisha vikao viwili vilivyobaki kuanzia mchana huu.

NB. Pole Jesca Kishoa Umaarufu gharama.
Alidhani bunge ni kijiwe cha kuropoka ropoka.Acha aisome number akawasimulie wanafamilia.
 
Tatizo la Jesca Kishoa ni kiherehere na kutojua tofauti kati ya mazungumzo ya mtaani na Bunge! Wabunge wa aina yake wanatakiwa wajifunze kwa Dr Slaa ambaye alikuwa anawasilisha hoja au tuhuma akiwa na vielelezo vya uhakika. Jesca yeye kakazana kuengea mipasho ya kwenye vijiwe. Hii inashusha hadhi ya Bunge. Shameful behaviour!
Slaa ni dokta...sio sawa na huyo Shilyolye bana.
 
Habari ya mujini ni nini hapa? ni kuthibitisha kama ni kweli Waziri alisimamia ununuzi wa mabehewa mabovu au ni kiasi gani cha fedha kilichopotea kwa ununuzi wa mabehewa hayo hayo mabovu? Wengine huita "spinning". Ni mchezo mmoja mbaya sana. Je ni nani anasema kweli hapa? Mbona hata serikali yenyewe ilishatamka hadharani kwamba mabehewa yaliyonunuliwa na Mwakyembe yalikuwa chini ya viwango na taratibu hazikufuatwa? Je tuachane na hoja hiyo nzito, na kisha tuhangaike kulinganisha kama Mbunge Kishoa alikuwa na maana ya upotevu wa Bilioni 274 au Bilion 60? Ni upuuzi uliopindukia.
 
Mwakyembe aliwapa chance ya kummaliza kumbe hawana data zaidi ya kuropoka tu!!
Mtu kawaambia Kama mkileta huo ushahidi najiudhuru hata ubunge!
Hizo data zingekuwepo si UKAWA wangeona ndio sehemu ya kupatia sifa???
Nahisi hata nywele nyeupe aliwahimiza wakusanye ushahidi lakini wapi.....wakurupukaji hawa.
 
Tatizo la Jesca Kishoa ni kiherehere na kutojua tofauti kati ya mazungumzo ya mtaani na Bunge! Wabunge wa aina yake wanatakiwa wajifunze kwa Dr Slaa ambaye alikuwa anawasilisha hoja au tuhuma akiwa na vielelezo vya uhakika. Jesca yeye kakazana kuengea mipasho ya kwenye vijiwe. Hii inashusha hadhi ya Bunge. Shameful behaviour!
Acha upuuzi hata slaa na zitto waliambiwa hivyo na baadae wakafungiwa vikao badae ikadhibitika ni kweli! Hivi unajifanya umesahau Epa! buzwagi kusainiwa hotelini! acha upuuzi! Huwa sipendi upuuzi wa kusema lete ushahidi! wakati kila kitu kipo wazi!
 
Aende kwa aliemwambia akamrecord na simu alete bungeni...
Bunge anageuza kijiwe cha kahawa
 
Wale waliosema anao ushahidi wako wapi?

Umewashuka shuu.
Tehe..tehe.. Upo mmbibi?
Wanajamvi walikuwa wanaulizana hapa siku nyingi, oooh! Faiza katumbuliwa..
Mie nikawaambia yupo, amepunguza tu mihemko kwa sasa toka brother kaka alipokabidhi kijiti pale Magogoni. Anasubiri zamu ijayo maana kimfumo kipindi kijacho atakuwa wa dini yetu.
Tehe Tehe.. Chotara Hizbu..
 
Sasa mbona naye Mwakymb hakukanusha kununua mabehew feki? Badala yake alipinga zaidi kiwango cha fedha kilichotajwa..,na kusema si zaidi ya bil60! Kwa hiyo inamaana kweli mabehewa yalikuwa feki lakini ya bil60
 
Aende kwa aliemwambia akamrecord na simu alete bungeni...
Bunge anageuza kijiwe cha kahawa
Hapa ni kwamba mnakiri ufisadi ila tuanapishana tu kwenye kiwango cha pesa kilichotumika kwenye ufisadi wa mabehewa?
 
Kwenye mambo yanayo husu ufisadi ni vyema tukaweka tofauti zetu za kivyama na kiitikadi pembeni tukawa wamoja. Kama Mh.Jesca anadai kuna ufisadi ulifanyika kwenye ununuzi wa mabehewa ni vyema basi kwa umoja wetu tuitake serikali ituletee report husika ili kukata mzizi wa maneno.
 
JESCA David Kishoa Mbunge wa viti Maalum CHADEMA Jimbo la Iramba Magharibi, amesimamishwa kuhudhulia vikao viwili vya bunge. Ni baada ya kuleta bungeni habari kuhusu mabehewa feki na kushindwa kuthibitishia bunge. Ameshindwa kuthibitisha aliyo yasema, hivyo kasimamishwa vikao viwili, alitakiwa asimamishwe vikao vitano.

Siku yenyewe ilikua hivi;

Kishoa alianza kumtaja Dk Mwakyembe kuwa ni jipu linalohitaji kutumbuliwa na Rais na kuwa nafasi aliyonayo hakustahili.

Kishoa alitaja sababu ya kumwita Dk Mwakyembe si msafi kwamba alitumia zaidi ya Sh 238 bilioni kwa ajili ya kununulia mabehewa ambayo yalithibitika kuwa ni mabovu.

Waziri Mwakyembe alikanusha madai yaliyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum (Chadema), Jesca Kishoa kuwa ununuzi huo wa mabehewa mabovu uliisababishia sherikali hasara ya shilingi bilioni 238, huku akitaka ripoti ya ukaguzi wa ununuzi huo iwasilishwe bungeni.

Akitumia kanuni ya 63 (3) kuomba kutoa taarifa, Mwakyembe alikanusha kiwango cha fedha kilichotajwa na mbunge huyo wa viti maalum ambaye ni mke wa aliyekuwa mbunge wa Kigoma Kusini, David Kafulila.

“Mbunge aliyesimama kabla, aliyejitambulisha kama mke wa Kafulila, ameeleza kwamba serikali ilitumia zaidi ya shilingi bilioni 238 na kuleta hasara kwa kununua mabehewa mabovu. Mheshimiwa Mwenyekiti nataka kukuthibitishia kwamba Serikali ya Jamhuri ya Muungano, kwa kununua mabehewa 274 haijawahi kutumia zaidi ya shilingi bilioni 60,”alisema Mwakyembe.

Waziri huyo alienda mbali na kueleza kuwa endapo mbunge huyo atawasilisha uthibitisho wa kiwango hicho cha fedha kutumika kununua mabehewa hayo, atajiuzulu nafasi yake ya ubunge.

“Mimi naomba athibitishe hiyo shilingi bilioni 238. Na nitashukuru sana kama akileta hapa. Na akileta hiyo, mimi nitajiuzulu hata ubunge,” alisema Mwakyembe.

Baada ya kauli hiyo ya Mwakyembe, Mbunge wa Kawe, Halima Mdee naye alisimama na kueleza kuwa Waziri huyo hakutumia kifungu sahihi kutoa taarifa kwa kuwa alipaswa kutumia kifungu cha 63 (4) kutoa ushahidi wa kukanusha kwake kwanza.

Naye Kishoa aliendelea kusisitiza kuwa Serikali inapaswa kuwasilisha bungeni hapo ripoti ya ukaguzi wa manunuzi ya mabehewa hayo.

Hata hivyo, Mwenyekiti wa Bunge, Dk. Mary Mwanjelwa alitoa siku tatu kwa mbunge huyo wa viti maalum kuwasilisha ushahidi kuhusu madai yake. Ambao kashindwa kuwasilisha hadi leo

Hivi leo kutokana na kanuni, Andrew Chenge, kaamua kumfungia vikao viwili asihudhulie bungeni kwani alitakiwa amfungie vikao vitano, lakini kwakuwa bunge limebakiza siku mbili, kaamua kumfungia siku mbili. Kabla ya kufungiwa Jesca alipewa nafasi ya kufuta kauli yake, lakini akakataa na kuendelea kusisitiza kwamba aliyoyasema ni ukweli haoni sababu ya kufuta kauli, ndipo Mwenyekiti wa Bunge Andrew Chenge kaamua kumfungia.

Kubenea alikua sahihi mana hawa wavuliwa chu* i na wakatiwa shanga huwa wanakurupuka tu........

Mfyuuu zake
 
Hata mh Zito alishasimamishwa mikutano mitatu sembuse vikao viwili?
 
Back
Top Bottom