Jesca Kishoa, asimamishwa Vikao viwili vya Bunge

Jesca Kishoa, asimamishwa Vikao viwili vya Bunge

Kwenye mambo yanayo husu ufisadi ni vyema tukaweka tofauti zetu za kivyama na kiitikadi pembeni tukawa wamoja. Kama Mh.Jesca anadai kuna ufisadi ulifanyika kwenye ununuzi wa mabehewa ni vyema basi kwa umoja wetu tuitake serikali ituletee report husika ili kukata mzizi wa maneno.
Hao mapro cccm hawatakuelewa mkuu
 
UJINGA WA CHADEMA NA UKAWA NI KUDHAN BUNGEN WAMEENDA KUPANDA CHAT KWENYE MAGAZETI, WATU WENYE AKILI ZAO HAWAROPOKI BILA UTHIBITISHO, AU. NA NYIE MNA MAKENGEZA KAMA BABA YENU?
 
Kuna wakati jamaa zetu wanatutia aibu bungeni, kwanini mbunge asijiridhishe na ushahidi kabla ya kuzungumza?

Angalia sasa tumeumbuka.

Kuna wakati naona aibu kuwa Mwana-UKAWA
 
Kuna wakati jamaa zetu wanatutia aibu bungeni, kwanini mbunge asijiridhishe na ushahidi kabla ya kuzungumza?

Angalia sasa tumeumbuka.

Kuna wakati naona aibu kuwa Mwana-UKAWA
Jitoe ukawa nenda upande wa pili huku tupo kikazi zaidi
 
Huyu katumwa na mumewe nini? Tunafurahi sana kama mbunge yeyote anyetoa tuhuma bungeni anaweza kuthibitisha kwa kutoa objective evidences. Sasa ni ya ku-insist tu hainogi

Serikali ilifanya uchunguzi kwa hiyo wana documents zote!!

Kama bunge lingekuwa liko partial wangeamuru hiyo report iletwe ili ukweli ufahamike. Wanafanya hivyo kwa vile wanajua itakuwa vigumu kwa watu wa nje kuipata hiyo report ............ Kama Kishoka kaja na maneno matu bila ushahidi na Mwakyebe kajibu kwa maneno matupu bila ushahidi, binafsi sioni sababu ya huyo Bi Kishoka kisimamishwa!!!
 
Tatizo la Jesca Kishoa ni kiherehere na kutojua tofauti kati ya mazungumzo ya mtaani na Bunge! Wabunge wa aina yake wanatakiwa wajifunze kwa Dr Slaa ambaye alikuwa anawasilisha hoja au tuhuma akiwa na vielelezo vya uhakika. Jesca yeye kakazana kuengea mipasho ya kwenye vijiwe. Hii inashusha hadhi ya Bunge. Shameful behaviour!
Kumbe ni mke wa Kafulila....!!! Hakupewa taarifa sahihi na mumewe
 
Hivi Kafulila kashindwa kumpa nondo mke wake? Si nilisikia anazo? Mwenzie Mdee alikwepa kuingia kwenye hii hoja ya mabehewa akampambanisha Mwakyembe na Mzee Sitta
Chadema ni chama cha kilaghai siku zote,wamezoea kuwadanganya nyumbu wa bodaboda
 
Wabunge wa upinzani wanahitaji kubadilika katika uwasilishaji hoja......waache kukurupuka kwa kutafuta umaarufu matokeo yake ndio hayo....
 
Uwe na akiba ya maneno kwani wewe ndo mwenyekiti?maana huwezi jua mwenyekiti ataamkaje anaweza mrejesha katibu mkuu utaficha wapi sura?
Nikaifiche wapi, chini ya kabati??? Chadema walimsema lowassa km fisadi halikadhalika zitto km msaliti, leo vipi? Watu wanabadilika kutokana na mzingira, hata akirejea Lazima maisha yataendelea tu,
 
SWALI, Je Ununuzi Wa Mabehewa Yale, Si Waliwahi Kuunda Tume Ya Uchunguzi Na Kuja Na Ripot Ya Madudu Kibao!!! Why Hiyo Ripot Haifanyiwi Kazi Kwa Miaka Yote Hiyo!! SASA Iwe Hesabu Sio Sahihi Au Sahihi, LKN Ndani Ya Mchakato Huo Tumeambiwa Na Tume Kuna Ufisadi Umefanyika!!!

LETENI USHAHIDI MKUU
 
Alisafirishwa Twiga mzima na hakuna ushahidi sembuse hii ya mabehewa ipo siku Mungu atawalipia wenye uchungu na nchi hii shame on you Chenge na Mafisadi wenzako wa CCM
 
Kweli CCM mmetegwa mkategeka! Huyu binti anao ushahidi wa kutosha, hakuupeleka makusudi ili kuvuta hisia za watu! Sasa CCM wamenasa na umma tayari unataka kujua kulikua na nini kwenye mabehewa hayo.Ushahidi sasa ndio utaletwa inawezekana kupitiabunge mwingine na siyo Kishoa Jesca. CCM wameshamshika Simba mkia sasa wale wapole!Mwakyembe ameshindwa kujinasua na msala huu mapema sasa awe mpole.
Cheap politics, kumbe lengo ni kukomoana
 
MH. JESCA KISHOA ATIKISA BUNGE SWALA LA KASHIFA YA MABEHEWA.

Na Kilawa the Iron

Bunge limeamua kumsimamisha Mh Jesca Kishoa kwa madai ya kwamba kashindwa kuthibitisha juu ya swala la kashifa ya mabehewa. Huu ni udhaifu uliojidhihirisha bungeni.

Awali ya yote sina budi kumpongeza Mh Jesca Kishoa kwa kutudhihirishia kwamba viatu alivyokuwa akivivaa Mh Kafulila na yeye vinamtosha. Ameonesha wazi kwamba hayumbushwi na uzembe wa viongozi wa bunge.

Ikumbukwe kashifa hii ya mabehewa iliibuliwa na Mh Kafulila na alieleza mwaka jana(2015) kwa kina juu ya Riport ya PPRA na Mamlaka nyinginezo zenye ripoti ya kashifa ya mabehewa.

Katika hali isiyoyakawaida bunge letu limedhihirisha kwamba halina meno ya kuutafuna mfupa uliopo mbele yake na si kushindwa kutafuna mfupa tu bali hata mnofu uliopo bunge limeshindwa kuutafuna badala yake linang'oa meno

Kumtoa Jesca kishoa bungeni ni sawa na kung'oa meno ya mbele na meno chonge halafu ukabakiwa na meno ya Nyuma tu.

Nini kilipaswa kufanyika na bunge kabla ya maamuzi ya kumsimamisha Jeska Kishoa kuhudhuria bungeni kwa siku mbili?

Mosi, Bunge lilipaswa kuhakikisha serikali inaleta riport iliyopo kutoka mamlaka husika bungeni ili wabunge waisome na waijadili kwa kina ili waone ni wapi pakuisimamia serikali.

Pili,Bunge lilipaswa kutoa ushirikiano wa kutosha kwa Mh Jesca Kishoa na Kafulila ili waweze kupata undani wa swala hilo na kuweza kulifanyia kazi bungeni kwa ufasaha.

Tatu, bunge lisifanye kazi ya kuitetea serikali badala yake lifanye kazi ya kuisimamia serikali. Bunge hili lifanye kazi kama mhimili unaojitegemea.

Nne, wabunge wote waache uvyama ndani ya bunge badala yake waoneshe ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha wanatekeleza majukumu yao kwa mjibu wa katiba na sheria za nchi yetu.

Naamini katika hayo machache bunge linaweza kufanya kazi kwa ufasaha, linaweza kuisimamia serikali badala ya kufukuza wabunge wa upinzani.

Kwanini udhaifu huu wa bunge unajitokeza?

Mosi, Ni vigumu sana kesi ya ngedere kuhulumiwa na Nyani. Kiujumla washiriki wakuu wa kashifa za ufisadi wengi wao ndio viongozi wa bunge na ndio viongozi wa serikali hivyo hali hii inapelekea ugumu kuwajibisha serikali kwakuwa wahusika ni walewale wenye mamlaka.

Pili, Wabunge kuendekeza uvyama ndani ya bunge, chuki binafsi, ubinafsi n.k

Tatu, baadhi ya wabunge pia hawajui majukumu yao yaliyowapeleka pale, wanadhani wamekwenda kuunga mkono hoja na kupiga makofi na sio vinginevyo

Hayo yote yakifanyiwa ukarabati naamini bunge linaweza kuwa na usimamizi mzuri wa serikali, uwakirishi mzuri wa wananchi.

Msema ukweli ni adui wa watenda maovu.
 
Huyo mwenyekiti wa Bunge anafukuza wabunge badala ya kuitaka serikali kuleta Bungeni mkataba wa manunuzi ya mabehewa na riport ya CAG? Hivi chenge anaweza kukemea mafisadi? Post za wana JF humu ndani kuna ushabiki sana wa kisiasa badala ya facts. Je anayoyafanya JPM yangefanywa na uongozi wa upinzani yangesemwa mangapi? Kweli tunaisoma Namba.

Mimi nimemsikia leo raisi Magufuli akiitaka mamlaka au tume inayohusika na uundwaji wa hiyo mahakama ya mafisadi kuharakisha uundwaji huo tena akisema wala haina haja ya kulifikisha suala hili bungeni. Amesema ana imani kubwa na jaji mkuu na pamoja na mahela menfi ya kuhonga waliyo nayo mafisadi hawawezi kupenya kwa jaji mkuu.Tukirudi kwenye topic ni kama zilivyo sheria zetu ukishatuhumiwa ni wajibu wa mtuhumiwa kuthibitisha usafi wake.Kwa maana nyingine ni kuwa ulikuwa wajibu wa spika au aliekalia kiti kwa niaba yake aagize wizara husika kuleta bungeni taarifa zote zinazoonyeaha mchakato mzima wa uagizaji mabehewa hayo ambako wabunge wangeona idadi ya walioomba tender na bei zake hadi uteuzi,idadi iliyoagizwa na iliyopokelewa,aina iliyoagizwa na iliyopokelewa ikionyesha na viwango,ripoti ya mkaguzi wao wa ndani,ripoti ya ukaguzi wa serikali na ripoti ya evaluator baada ya mabehewa kuingizwa relini na kubeba mzigo na sio tu kumkalia m-bunge Kishoa kooni alete ushahidi. Haya ni mapungufu makubwa ya viongozi wa ccm na ukichukulia watuhumiwa ni miongoni mwa mafisadi wenyewe hiyo haki inapatikanaje?
 
Ndio ubaya wa Shanga-zi-kikatika na akili huwa zinakatika
 
Tanzania ni nchi ya wajinga sana kwani asipo wasilisha kuna shida gani,,? Mwambie mama Makimda asome lipoti ya mbunge Lema, au mlikuwa hamjazaliwa bado, ndo shida ya watoto wa mama, kula kulala.
Du. Akosee mmke wa mtu jumba bovu unawapa wa TZ!
 
Hivi huyu jesca aliishia darasa la ngapi? Hivi ana akili kweli? Hivi huwa havuti bangi?
Nime yauliza hayo maswali baada ya kuona alicho kifanya bungeni leo baada ya kutakiwa kutoka nje ya bunge. .!

Huyu ni bure kabisa yani yeye alisema serikali ilipoteza billion 234 kumbe hakuwa na ushahidi halafu anatakiwa kuleta ushahidi halafu ana waandikia PPRA wampe document za manunuzi ya mabehewa ....sasa najiuliza ikiwa alisema anao ushahidi sasa kinacho mfanya kuwaandikia PPRA kuhitaji document ni nini? Kwanini hakuwaomba kabla ya kuropoka?
 
Back
Top Bottom